Nisaidieni jinsi ya kupunguza kupenda

Kwanini UIDHULUMU nafsi yako jinsi unavyompenda huyo jamaa? Bila ya shaka kuna kitu kinachokufanya umpende kiasi hicho. Mapenzi si sawa na fungu la kitunguu au nyanya kwamba akikupa kilo moja basi nawe umpe kilo moja. Endelea kumpenda kiasi hicho hicho labda kuna siku atakuelewa otherwise it his LOSS. ID yako ya siku zote iweke kwenye PM yangu :cool:

Mimi ni mwanamke nimempenda mwanaume wangu kupita kiasi hata sijui nimempendea nini. Hili jambo linaniathiri sana kwasabu najua yeye hanipend kama ninavyompenda.

Huwa nabishana na mawazo yangu wakati mwingine kwa kuona kwamba ananipenda saana ila haniamini kwasababu anakauli yake kila siku anasema mimi nina mambo mengi bila kufafanua zaidi, huu umekua kama wimbo sasa masikioni mwangu.

Sasa nakua sielewi mambo mengi ni yap? Nachojua tu ana wivu sana. Sikai naye, yeye anakaa kwake na ameajiriwa Serikalini na mimi nakaa kwangu na nimejiajiri ila tupo Mji mmoja.

Nimeshajaribu sana kumuacha nimeshindwa basi angalau nipunguze tu. Nimefungua jina jipya kwasababu maalumu.
 
Binadam tunatofautiana.. kwa mfano mm demu wangu huwa anahisi simpendi na anajihisi yeye anaupendo mkubwa kwangu zaid yangu kutokana na mamb flanflan, Kama vile anataka tuchat na tuongee muda mref kila wakat ila mm nashindwa kuwa hivyo kwasababu ya kazi, Mara nying huwa yeye ndo anaanza kunitafuta kabla yangu.., hiki kitendo pia kinazid kumfanya aamini kuwa mm simpendi lakin sivyo, nampenda Sana tu, yeye huwa Ni muongeaji Sana kuliko mm, kwahiyo mm ule ukimya wangu unamfanya aamini sina furaha nae, hapana ninafuraha nae ila kashindwa kunielewa tu,.

Mapenzi yana changamoto Sana unaweza kujiona hakupendi kumbe anakupenda Sana, na unaweza kuona anakupenda kumbe anakulaghai tu, we kaa nae chin na umwambie akuweke waz Kama kweli anakupenda au yupo mwngne anaempenda zaid, na akwambie ni sababu zipi zinazomfanya awe hivyo, naamin majibu atakayokupa utaweza kugundua kitu Kama unapendwa au unamkera tu.
Baada ya kimya cha siku kadhaa niliamua kumfuata kabisa kazini kwake na nikapiga naye stor kishani kamwambia aniambie kama hanipendi aniambie na mimi nitakubaliana na yeye kama ananipenda pia aniambie..nilimuelewesha vizuri kabisa kuhusu lengo langu la kutaka kujua..yeye akanijibu na tukapanga aje siku fulan na kweli ile siku akaja tukafanya yetu ila baada ya pale sasa kimya tena...aliniambia nisinywe lkn mimi nilikunywa hiyo siku kidogo tu ili kuondoa aibu kwamaa nina aibu sana siwez kwenda kavu.
Sasa cjui ndiyo kilimuudhi?
Maana amekua kimya tena
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nimeshajaribu sana kumuacha nimeshindwa basi angalau nipunguze tu.

mi nakushauri jenga mazoea ya kuonana nae mara kwa mara, tumia muda mwingi kukaa nae, zidisha mawasiliano, kama una kapicha kake chukua uwe unakaangaliaa, hiyo itakusaidia kumzoea na kumuona wa kawaida from then itakuwa rahisi kwako kumuacha sababu atakuwa hana jipya tena.
Yaan nikiwa naangalia picha yake ndiyo huwanachanganyikiwa kabisa bora hata nisimuone...na kuonana naye ni mpaka anipe hiyo nafas kwamaana siyo rahis mimi kumpata sijui ratiba yake
 
Ukisikia mwanaume anakwambia wewe una mambo mengi maana yake hakuamini, anahisi unamcheat. Huenda uko busy sana kwenye social media unachat chat sana unajipost post, una mashost waasioeleweka. Hata mimi ni kauli ambayo uwa ninaitumia.
Sasa nifanyaje aniamin?
Sichat kiasi hicho na kazini kwangu anapajua..huwa namwambia ratiba yangu
 
Kwanini UIDHULUMU nafsi yako jinsi unavyompenda huyo jamaa? Bila ya shaka kuna kitu kinachokufanya umpende kiasi hicho. Mapenzi si sawa na fungu la kitunguu au nyanya kwamba akikupa kilo moja basi nawe umpe kilo moja. Endelea kumpenda kiasi hicho hicho labda kuna siku atakuelewa otherwise it his LOSS. ID yako ya siku zote iweke kwenye PM yangu :cool:

Haahaaa ntaiweka! Ngoja nijitahid lakn mpaka nahis naumia
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Sasa nifanyaje aniamin?
Sichat kiasi hicho na kazini kwangu anapajua..huwa namwambia ratiba yangu
Ukihisi kwaamba kupenda kunakuchanganya basi jitafakari utateseka sana na nafsi. Anza kumchukulia poa tafuta kitu kingine cha kukeep busy maana utateseka sana nafsi.
 
Kwanini uumie? Una vigezo vyako vya kumpenda ME nadhani vyote anavitimiza ndiyo sababu unampenda sana pamoja na kuwa ana wivu uliopitiliza, kutoonyesha hakupendi sana na kudai una mambo mengi

Muulize ana maana gani anaposema una mambo mengi? Akutajie mambo hayo ili uyajue. Pia mwambie unaona hakupendi sana kama unavyostahili, tatizo ni nini?

Baadhi ya ME hufanya makosa kwa kutomwambia GF/Mke kama anampenda sana kwani wanadai baadhi huanza kuleta KIBRI, lakini atawaambia ndugu, jamaa na marafiki kwamba anampenda sana mkewe/GF lakini mhusika haambiwi. Mie naona hayo ni makosa.

Haahaaa ntaiweka! Ngoja nijitahid lakn mpaka nahis naumia
 
Kujibu ombi lako bidada

Muone wa kawaida tu. Mchukulie powa tu. Mdharau kidogo ndani ndani lakini usiionyeshe nje. Chukulia kawaida tu kila kitu anachokufanyia na kwamba hata masela wengine wapo tu kama huyo Jamaa ako.

Mix Love na Ukawaida tu.
Njoo hapa ulete mrejesho
 
Baada ya kimya cha siku kadhaa niliamua kumfuata kabisa kazini kwake na nikapiga naye stor kishani kamwambia aniambie kama hanipendi aniambie na mimi nitakubaliana na yeye kama ananipenda pia aniambie..nilimuelewesha vizuri kabisa kuhusu lengo langu la kutaka kujua..yeye akanijibu na tukapanga aje siku fulan na kweli ile siku akaja tukafanya yetu ila baada ya pale sasa kimya tena...aliniambia nisinywe lkn mimi nilikunywa hiyo siku kidogo tu ili kuondoa aibu kwamaa nina aibu sana siwez kwenda kavu.
Sasa cjui ndiyo kilimuudhi?
Maana amekua kimya tena
nimegundua jamaa inawezekana anakupenda Sana ila ww huenda Kuna mambo mengi unayafanya hayamfurahishi hiyo kitu inamfanya awe na mgogoro wa nafsi, labda pengine unapenda pombe ye hapendi hiyo inaweza kumfanya ikawa sababu ya ww kutokua chaguo lake lakin anakupenda, kinacho mfanya usiwe chaguo pengine no baadhi ya vitu asivyo vipenda kama hivyo pombe na mambo mengne ambayo siyajui, Sasa ongea nae umuulize ni kipi asicho kipenda na kipi anakipenda alaf ujaribu kubadilika kuacha vile asivyo vipenda ikiwa kama kweli anakupenda utaona tu jamaa anabadili na mapenzi yanaongezeka
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom