Nisaidieni jamani

Nisaidieni jamani

Kimbia dada yngu,tena usijaribu kurud nyuma kabsaaa,huyo si mwanaume wako amin nakembia,wakwako anakuja wala usiogope stil unamuda wa kutosha as ling as unaweza kujimudu na maisha yako.
 
pole sana,mnapanga mipango yote hiyo bila kwenda kwao wala kuwaona wazazi wake kweli love is blind
NB: OGOPA WANAUME WA KENYA NI SHIDAAAAAAAA
 
Matatizo yanaepukika, kama yanaepukika, basi wewe yaepuke.

Achana nae huyo jamaa
 
Hata kama una utayari wa kuwa mke mwenza tafuta mume aliyenona...acha kutumika...
Mimi nitamwelewa mtu anayeolewa na kijana aso na pesa kama first wife...(wanatafuta wote)

Lakini second wife...hicho kitakuwa ni kituko...maana hata hizo dini zinazoruhusu uke wenza zinaongelea uwezo wa kuwatimizia...
 
Afu jamani muwe makini na hawa so called foreigners...wengi ni liars na huwezi jua ukweli kwani ni ngumu kupeleleza mtu wa nchi nyingine...

Tena wewe una bahati...ungejashtuka tayari una watoto wawili...kujinasua huwezi..
 
Pole sana,nashindwa kuelewa watz tuna tatizo gani,madini yetu yaibiwe,gesi yetu iibiwe dada zetu wanatapeliwa
kweli hata nikikupa ushauri naogopa nao matapeli watautapeli tu yaani ni shida!

hahahahah nimeshashauriwa ndugu na uwamuzi nimeshachukua
 
Unaposema hutapata mtu mwingine sikuelewi! Hapo my dia hamna future, anza maisha mapya. Jamaa anaonekana muongo muongo sana na ameshakusoma kuwa kwake hupindui ndo mana hata anafanya hayo yote. Kimbia mdogo wangu hilo jumba bovu

asante sana Mama yake P nimeshakimbia dada yangu niko kwa mama yangu leo nimerudi kujiweka sawa kidogo nirudi tena kujitegemea
 
mwe! mambo yako waziiii ila waswahili wa daladala wanasema "mkanye akirudi".
 
ifanye iwe historia.... anza maisha mapya..... uongo wake umetukuka maana katika kila plan mliyoshirikiana kuweka mwenzio ana zakwake ambazo hakuhusishi.... yote katka yote tafuta PERFECT LIFE.... hii uliyonayo ina dosari za kutosha
 
Utakuwa umekatwa kichwa wewe si bure...
 
mtu kama huyo ipo siku atakuibia mali zako utakuja kutulilia hapo jf
 
hahahahah nimeshashauriwa ndugu na uwamuzi nimeshachukua
Afadhari,zingatia na usirudi nyuma.Ninachojua ninyi wadada mnashauriwa vizuri mnakubali,akija jamaa akakupiga sound na kuomba msamaha wa uongo-uongo,Utashangaa msamaha anaomba yeye,machozi unalia wewe
papuchi utampa na utamkopea fedha nyingine.Na baadaye tutakutana humu tena ila naamini utabadilisha ID au utasema shoga angu kafanyiwa hivi na vile.
Lakini kama umeshika ulichoshauriwa shika sana,najua huyo jamaa atarudi tu kukuchuna trust me.
 
Habari zenu hii ni mara yangu ya kwanza kuingia katika mtandao huu naomba mnipokee. licha ya ugeni wangu ila nimekuja nina shida nahitaji mawazo yenu.

Mimi ni msichana wa miaka kati ya 25-30, nimekuwa na mwanaume ambaye tumekuwa na urafiki wa kimapenzi sasa ni muda wa mwaka mmoja na miezi nane, huyo jamaa yeye ni raia wa Kenya.

kwa mara ya kwanza nilivyokutana nae aliniaweka wazi kuwa anawatoto wawili wa kiume na wakike ila akaniambia kuwa mke wake alimkimbia na aliolewa na mwanume mwengine.

Nilimpokea yeye na watoto wake ingawa watoto walikuwa Kenya ila nilichukua nafasi ya mama kwa kuwafanyia hata shopping na kutuma vitu kuwafikia huko walipo.

katika familia yao wanaonifahamu ni wadogo zake na kaka zake na wajomba zake ila plan zetu ilikuwa mwezi wa sita mwaka huu niende nae kwao, lakini ilivyofika aliondoka akaniambia alipata msiba hivyo anakwenda kuzika itakuwa siyo vizuri kuna msiba na yeye ndiyo anipeleke kwa mama yake kama kunitambulisha.

Nilikubaliana naye ila cha ajabu alikaa huko miezi miwili lakini hakukuwa na mawasiliano kama ilivyokawaida katika hiyo miezi miwili alinipigia simu mara tano tuu.

Baadae alirudi na alivyokuja aliniomba msamaha kuwa simu yake ilipata matatizo, sikujibu kitu nikaamua kufanya uchunguzi. mwezi huu wa nane nimegundua kuwa huyu jamaa anamke na watoto wanne, nilijua kwa kuchukua passport yake na kuangalia kule nyuma kuna vitu amejaza.

Nikazipiga zile namba nikaongea na huyo mwanamke aliumia sana mama wa watu alilia sana kwenye simu kiukweli nilijisikia vibaya sana akanimbia huku nilipo inafikia kipindi mimi na watoto tunalala njaa, kumbe yeye anafanya starehe huko, nikamjibu kwa kweli mimi nimekuwa msaada sana kwa watoto wako kwani hata ada za mwaka huu mimi nimetoa kwa kuwa jamaa mambo yake hayakwenda vizuri.

Yule dada akaniambia nimpe muda then atanijibu, ila baadae akanipigia akaniambia yeye ni mama wa nyumbani hana kipato chochote basi niendelee tuu kumsaidia ila hakugusia swala la mume wake.

Baadae nilikaa na huyu mwanaume nikamuuliza kwanini alinificha muda wote huo kama anamke akadai kuwa kuna matatizo ya kifamilia hivyo nimwachie yeye anajua jinsi ya kuyatatua, nilimkomalia sana inabidi aniweke wai kuwa yeye aliplan toka mwanzo kuwa awe na wake wawili mmoja kwa kuwa hana kazi basi wapili akiwa na kazi watasaidiana kwenye maisha.

Wapendwa mimi naombeni ushauri licha ya nyumbani kwetu nikimanisha wazazi wanajua ni rafiki yangu na plan zetu ilikuwa mwezi wa tisa aje kujitambulisha rasmi, sasa wapendwa kwa uongo wote huo huyu ni mwanaume sahihi?

Kitabia ni mpole ila sasa amekuwa na tabia ya kuwa na wasichana wasichana wengine napo nilipo mbona akaniambia ni wasichana anawapata kwenye mtandao wa Twoo na nisipokuwepo kwake anawapeleka hao wasichana hadi kwake.

Naombeni ushauri wenu nifanyeje anadai sheria ya kwao inaruhusu wake wawili ila dini yetu hairuhusu hivyo, na mimi mwenyewe siko tayari kuwa mke wapili, ila muda mwingine naona kwakuwa ameshanipotezea muda simwezi kupata tena mtu mwingine na miaka inakimbia.

Na umri wa huyu mwanaume ni kati ya 40-45
Acha utoto anaogopa kuachana nae kwa kuwa nae mwaka mmoja wakati sisi tumekaa mpaka minne na tulipoona usaliti tuliacha pia unasema haupo tayari kuwa mke wa pili huo ndio ukweli jaama ana mke na watoto wa nne unadhani utabadili hilo? amua na kata mawasiliano utasahau tu baada ya miezi 6
 
ivi kunawanawake wengine kama wamerogwa sijui au ni kitu gani??? kwanza nikuulize ingekuwa wewe ndio huyo dada ungejisikiaje?? maana hapo mwanzo umesema umemwone huruma sana? sasa saivi unataka ndoa na wewe hounekane mke wa fulani au mwizi wa mume wa mtu me sione point yako hasa ni nini dada. sikiza wewe kama umeamua kuwa mtoaa misaada wa familia za watu basi saidia ila helewa mwenye tabia haacha ata achembe baada ya wewe atatafuta mwingine watatu mwenye kipato kikubwa kuzidi wewe ili awasaidie kulea vizuri na maisha yaendelee, alafu jua kwamba umependewe hela za wala hauna lolote la kumzidi huyo mwingine, bidada tafuta wakwako kama yupo yupo tu huyo hakufai jua wala kwenye masika. salt jibu la uyaya wala halimfai huyo kizambina"" bi dada tulia upate wako umri ni namba tu.
 
Back
Top Bottom