Nisaidieni jamani

Nisaidieni jamani

Mie mwenyewe nashangaa, eti bado anataka ushauri, umeshaongea hadi na mke wake, umeshajua mbivu na mbichi bado unataka ushauri, upi huo bidada

Pole sana, ushauri gani unaotaka hapa baada ya kudanganywa kiasi hiki!? Mwambie afungashe virago vyake haraka sana toka kwako. Asikutafute kwa namna yoyote ile.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Afadhari,zingatia na usirudi nyuma.Ninachojua ninyi wadada mnashauriwa vizuri mnakubali,akija jamaa akakupiga sound na kuomba msamaha wa uongo-uongo,Utashangaa msamaha anaomba yeye,machozi unalia wewe
papuchi utampa na utamkopea fedha nyingine.Na baadaye tutakutana humu tena ila naamini utabadilisha ID au utasema shoga angu kafanyiwa hivi na vile.
Lakini kama umeshika ulichoshauriwa shika sana,najua huyo jamaa atarudi tu kukuchuna trust me.
hahahahah mimi nimeamua kaka yangu
 
Acha utoto anaogopa kuachana nae kwa kuwa nae mwaka mmoja wakati sisi tumekaa mpaka minne na tulipoona usaliti tuliacha pia unasema haupo tayari kuwa mke wa pili huo ndio ukweli jaama ana mke na watoto wa nne unadhani utabadili hilo? amua na kata mawasiliano utasahau tu baada ya miezi 6
asante nimeshaamua. asante kwa ushauri
 
ivi kunawanawake wengine kama wamerogwa sijui au ni kitu gani??? kwanza nikuulize ingekuwa wewe ndio huyo dada ungejisikiaje?? maana hapo mwanzo umesema umemwone huruma sana? sasa saivi unataka ndoa na wewe hounekane mke wa fulani au mwizi wa mume wa mtu me sione point yako hasa ni nini dada. sikiza wewe kama umeamua kuwa mtoaa misaada wa familia za watu basi saidia ila helewa mwenye tabia haacha ata achembe baada ya wewe atatafuta mwingine watatu mwenye kipato kikubwa kuzidi wewe ili awasaidie kulea vizuri na maisha yaendelee, alafu jua kwamba umependewe hela za wala hauna lolote la kumzidi huyo mwingine, bidada tafuta wakwako kama yupo yupo tu huyo hakufai jua wala kwenye masika. salt jibu la uyaya wala halimfai huyo kizambina"" bi dada tulia upate wako umri ni namba tu.

asante nimeelewa
 
Pole kwa kutoa uroda kwa mwaka mzima bila kumjua vyema unayempa...
 
Habari zenu hii ni mara yangu ya kwanza kuingia katika mtandao huu naomba mnipokee. licha ya ugeni wangu ila nimekuja nina shida nahitaji mawazo yenu.

Mimi ni msichana wa miaka kati ya 25-30, nimekuwa na mwanaume ambaye tumekuwa na urafiki wa kimapenzi sasa ni muda wa mwaka mmoja na miezi nane, huyo jamaa yeye ni raia wa Kenya.

kwa mara ya kwanza nilivyokutana nae aliniaweka wazi kuwa anawatoto wawili wa kiume na wakike ila akaniambia kuwa mke wake alimkimbia na aliolewa na mwanume mwengine.

Nilimpokea yeye na watoto wake ingawa watoto walikuwa Kenya ila nilichukua nafasi ya mama kwa kuwafanyia hata shopping na kutuma vitu kuwafikia huko walipo.

katika familia yao wanaonifahamu ni wadogo zake na kaka zake na wajomba zake ila plan zetu ilikuwa mwezi wa sita mwaka huu niende nae kwao, lakini ilivyofika aliondoka akaniambia alipata msiba hivyo anakwenda kuzika itakuwa siyo vizuri kuna msiba na yeye ndiyo anipeleke kwa mama yake kama kunitambulisha.

Nilikubaliana naye ila cha ajabu alikaa huko miezi miwili lakini hakukuwa na mawasiliano kama ilivyokawaida katika hiyo miezi miwili alinipigia simu mara tano tuu.

Baadae alirudi na alivyokuja aliniomba msamaha kuwa simu yake ilipata matatizo, sikujibu kitu nikaamua kufanya uchunguzi. mwezi huu wa nane nimegundua kuwa huyu jamaa anamke na watoto wanne, nilijua kwa kuchukua passport yake na kuangalia kule nyuma kuna vitu amejaza.

Nikazipiga zile namba nikaongea na huyo mwanamke aliumia sana mama wa watu alilia sana kwenye simu kiukweli nilijisikia vibaya sana akanimbia huku nilipo inafikia kipindi mimi na watoto tunalala njaa, kumbe yeye anafanya starehe huko, nikamjibu kwa kweli mimi nimekuwa msaada sana kwa watoto wako kwani hata ada za mwaka huu mimi nimetoa kwa kuwa jamaa mambo yake hayakwenda vizuri.

Yule dada akaniambia nimpe muda then atanijibu, ila baadae akanipigia akaniambia yeye ni mama wa nyumbani hana kipato chochote basi niendelee tuu kumsaidia ila hakugusia swala la mume wake.

Baadae nilikaa na huyu mwanaume nikamuuliza kwanini alinificha muda wote huo kama anamke akadai kuwa kuna matatizo ya kifamilia hivyo nimwachie yeye anajua jinsi ya kuyatatua, nilimkomalia sana inabidi aniweke wai kuwa yeye aliplan toka mwanzo kuwa awe na wake wawili mmoja kwa kuwa hana kazi basi wapili akiwa na kazi watasaidiana kwenye maisha.

Wapendwa mimi naombeni ushauri licha ya nyumbani kwetu nikimanisha wazazi wanajua ni rafiki yangu na plan zetu ilikuwa mwezi wa tisa aje kujitambulisha rasmi, sasa wapendwa kwa uongo wote huo huyu ni mwanaume sahihi?

Kitabia ni mpole ila sasa amekuwa na tabia ya kuwa na wasichana wasichana wengine napo nilipo mbona akaniambia ni wasichana anawapata kwenye mtandao wa Twoo na nisipokuwepo kwake anawapeleka hao wasichana hadi kwake.

Naombeni ushauri wenu nifanyeje anadai sheria ya kwao inaruhusu wake wawili ila dini yetu hairuhusu hivyo, na mimi mwenyewe siko tayari kuwa mke wapili, ila muda mwingine naona kwakuwa ameshanipotezea muda simwezi kupata tena mtu mwingine na miaka inakimbia.

Na umri wa huyu mwanaume ni kati ya 40-45

embu achana na uyo mbaba kwnz ushasema ana waschn waschn thn unamtetea ni mpole??uyo ni boko haramu wa mapenzi shost embu achana nae ....km unaona aibu kusema hyo story kwenu ukiulizwa sema amefarik na ajali ya moto uko kwao Kenya
 
sio kusema asante na kuelewa fanya maamuzi sahihi kwa muda huu kuliko uchelewe ndio uuanze kutoa lawama maisha yako yako mikononi mwako mpenzi. wanaume wapo tu sio kila huusiano ulio nao utapata degree mahusiano mengine ni tusheni tu ili ufuzu kuingia kupata degree wangu. na usikae kuaangalia watu watasema nini kuhusu wewe, sio wote wanaokupigia makofi wanakusifia weng wao wanakuhurumia
 
pachambili sikuelewi isee umeamua nini sasa kuwa mlezi wa familia ya huyo mtu au wanawake wengine full kudhalilishana tu
 
embu achana na uyo mbaba kwnz ushasema ana waschn waschn thn unamtetea ni mpole??uyo ni boko haramu wa mapenzi shost embu achana nae ....km unaona aibu kusema hyo story kwenu ukiulizwa sema amefarik na ajali ya moto uko kwao Kenya

hahahahaha asante sana kwa kunichekesha niko wenye foleni ya kumuona doctor nimejikuta nacheka kila mtu kanishangaa
 
haaaaaaaaaaa hilo neno wangu hongera sana fanya yako mwanamke full kujiamini hawa wapo tu
 
Inatia huruma Kweli lkn mapenzi Haya asikwambie mtu. Kwanza shukuru Mungu amekuonyesha Hilo, ilikuwa ni wakati wake wewe kufumbuka macho.

Ushauri: achana na huyo mwanamme na mazoea na huyo mkewe Acha kabisa. Kwa kuwa wazi zaidi elezea wazazi wako ili wasikuone kicheche, maana kama huyo mwanaume kama anapajua kwenu anaweza ata Kwenda kwa ajili ya kujitakasa na kuonekana yeye msafi.

Kama inawezekana badili njia ya mawasiliano kabisa. Kuwa busy na kazi zako. Naamini aliye sahihi kwa wakati sahihi atafika. Usifanywe mtumwa wa mapenzi sasa, usichukulie udhaifu wa kupenda ukateseka.

Nakutakia Kila la kheri.
 
Yani wewe mdada hebu fanya yako huyo hautomuweza maana ana mambo mengi na si mkweli
 
Back
Top Bottom