Jenerali QoyoJB
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 304
- 162
Dada achana na huyo mtu muda uliopoteza siyo mwingi kuliko matatizo unayokaribisha kwenye maisha kwa muda mrefu wa maisha yako. Kwanza ni muongo na anakutumia kama kitega uchumi cha kulea watoto wake. Amekwambia watoto wawili kumbe wanne? Sasa wewe utazaa wangapi jumla wawe wangapi na mtalea vipi? Atakutia presha siku ukigundua mengine. Hadi hapo mshukuru Mungu amekufungua macho sasa ukiendelea usimlilie Mungu tena maana utakuwa umekaidi mwenyewe. Kama unaendelea naye endelea kama starehe yako tu usikose dushelele ghafla ila angalia utaratibu mwingine. Kwa umri wako bado unapata mume fresh tena una kazi yako unahofia nini? Jambo la pili nakutahadharisha ni kuhusu uraia. Huyo ni mkenya wewe ni mtanzania je uko tayari kubadili uraia wako kwasababu tu ya kuwa mke wa pili? Je siku ukihamia kenya maisha yatakuwaje na huyo bi mkubwa? Unajua hao watoto wake wanaopata shida na mama yao wanakuona wewe ndo unakula hela za baba yao hivyo wataku treat kama malaya siku wakipata nguvu utajuta kumfahamu huyo mkenya. Kama hajakutia mimba tafuta njia ya kuchomoka. Suala la tatu kwamba huyo mtu hafai ni hiyo unasema ana wasichana wengine kibao anawapeleka hadi kwake siku haupo. Sasa hapo dadangu bado hujiongezi? We kwa huyo mtu ni mchepuko tu kama michepuko mingine wala siyo mke mtarajiwa! Najua sikio la kufa halisikii dawa! Ila uamuzi ni wako sisi tunaishia kushauri kama ulivyoomba.