Nisaidaeni ushauri wa kisheria na kimaadili wana Jamii forums

Mathematic

Member
May 15, 2011
56
2
Mimi ni kijana wa kiume mwenye miaka 33,nilikuwa na mpenzi wangu alienizidi miaka miwili na ana mtoto wa kike wa miaka 19 sasa. Mapenzi yetu yalidumu kwa miaka 6 lakini kutokana na migongano ilokuwa ikitokea mara kwa mara hatukuweza kutambulishana kwa wazazi wetu hadi 2010 tulipoamua kuachana rasmi nami nikamruhusu aolewe kama ataamua kufanya hivyo.

Hivi ninavyoongea tayari ameshaolewa na anakaa huko kwa mume wake. Kila mtu hana kinyongo na mwenzake. Tatizo ni kuwa nimejikuta nimeingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na yule binti yake ambaye wakati nipo na mama yake alikuwa ananiita UNCLE.

Nimekuwa nae kwa muda wa miezi 7 lakini kinachonitisha ni kwamba ana ujauzito ambao kwa mazingira naona ni kweli unaweza kuwa wakwangu. Kwa sasa mama yake bado hajajua maana ni mimba changa sana.

Je,mama yake akijua kuwa mhusika ni mimi, reaction yake itakuwaje? What will be my position before the eyes of the law?

Nampenda sana huyu binti na sitaki atoe mimba yangu.
Nishaurini tafadhari waungwana.
 
Yaani umekula kuku na mayai yake??halafu unataka mayai yaangue kuku tena mhh kha! Hiv ullianzaje tena na mtoto?

Mhh huyo mama akijua mbona patachimbika!! Ulikosea kukukubal kuwa na huyo mtoto?

Haya ngoja wataalamu wa mambo waje kukushaur
 
Shitii!!!!!!!!! Sasa unaataka ushauriwe nini hapo???????? umeniudhi sana, najuuta kusoma thread yako. Ina maana ulikuwa hujui kama huyo ni sawa na mtoto wako au?? Umeniboa saaaaaaaaaana na umeharibu siku yangu, naomba huyo mama yake ajue haraka iwezekanavyo!
 
All i can say is "shame on both of you":nono::nono:
 
Join Date : 15th May 2011
Posts : 2
Thanks 0 Thanked 0 Times in 0 Posts

Rep Power : 0

Post ya pili tu unakuja na thread kama hii wewe kiboko
 
Binadamu nyie....!
Haya zaeni aliekua mpenzi wako ageuke mama mkwe na bibi wa mwanao!!Kaazi kweli kweli!

Alafu huna aibu eti unaomba msaada wa kimaadili wakati maadili ushayavunja?!UNALO!!
 
Mimi ni kijana wa kiume mwenye miaka 33,nilikuwa na mpenzi wangu alienizidi miaka miwili na ana mtoto wa kike wa miaka 19 sasa. Mapenzi yetu yalidumu kwa miaka 6 lakini kutokana na migongano ilokuwa ikitokea mara kwa mara hatukuweza kutambulishana kwa wazazi wetu hadi 2010 tulipoamua kuachana rasmi nami nikamruhusu aolewe kama ataamua kufanya hivyo.

Hivi ninavyoongea tayari ameshaolewa na anakaa huko kwa mume wake. Kila mtu hana kinyongo na mwenzake. Tatizo ni kuwa nimejikuta nimeingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na yule binti yake ambaye wakati nipo na mama yake alikuwa ananiita UNCLE.

Nimekuwa nae kwa muda wa miezi 7 lakini kinachonitisha ni kwamba ana ujauzito ambao kwa mazingira naona ni kweli unaweza kuwa wakwangu. Kwa sasa mama yake bado hajajua maana ni mimba changa sana.

Je,mama yake akijua kuwa mhusika ni mimi, reaction yake itakuwaje? What will be my position before the eyes of the law?

Nampenda sana huyu binti na sitaki atoe mimba yangu.
Nishaurini tafadhari waungwana.

Mamake lazima akulaani...that ain't fair kabisa!!..huyo mtoto nae, aibu!!
 
Dahhhhh
kwa kweli tayari yametokea
sasa ushauri wangu mtafute lawyer
mzuri tu... baada ya hapo tafuta njia yeyote mama yake afahamu hilo..

maana hapa naona umekuwa selfish kidogo wewe unataka msaada wakati anayeteseka
kupiti kiasi ni binti.. anamuhitaji mama yake kwa wakati huu...

taka usi taka mam atafahamu
akifahamu mapema vizuri itakuwa vema.. kasheshe mpauko utaona lakini naomba usimtese binti wa watu kimawazo ... mwambie mama yake..
 
We wa ajabu kweli yani umekula mtoto na mama yake inauma sana.
Ona sasa ulishazua utata sasa fanya utatue ingekuwa busara ungetuomba ushauri kabra hujala hicho kifaranga
 
Dahhhhh
kwa kweli tayari yametokea
sasa ushauri wangu mtafute lawyer
mzuri tu... baada ya hapo tafuta njia yeyote mama yake afahamu hilo..

maana hapa naona umekuwa selfish kidogo wewe unataka msaada wakati anayeteseka
kupiti kiasi ni binti.. anamuhitaji mama yake kwa wakati huu...

taka usi taka mam atafahamu
akifahamu mapema vizuri itakuwa vema.. kasheshe mpauko utaona lakini naomba usimtese binti wa watu kimawazo ... mwambie mama yake..
asante kaka kwa ushauri wako. maana hapa nilipo sijielewi kichwa kimepiga short ukizingatia baadhi ya waungwana wanalaumu zaidi kuliko kushauri. wakati maji yameshamwgika.....
 
Shitii!!!!!!!!! Sasa unaataka ushauriwe nini hapo???????? umeniudhi sana, najuuta kusoma thread yako. Ina maana ulikuwa hujui kama huyo ni sawa na mtoto wako au?? Umeniboa saaaaaaaaaana na umeharibu siku yangu, naomba huyo mama yake ajue haraka iwezekanavyo!
siku zote mtu anatakiwa ashauriwe ili kutatua tatizo lililopo mbele yake kuliko kumlaumu maana maji yamesha mwagika na nimeamua kuwa wazi kulileta tatizo langu humu jamvini ili kupata mawazo ya watu. maana kadiri siku zinavyokwenda binti ndo anazidi kuchanganykiwa. najitahidi kumsihi asimwambie mtu yoyote kwa sasa. nipe ushauri wa kunijenga kuliko kuzidi kunichanganya....
 
Dahhhhh
kwa kweli tayari yametokea
sasa ushauri wangu mtafute lawyer
mzuri tu... baada ya hapo tafuta njia yeyote mama yake afahamu hilo..

maana hapa naona umekuwa selfish kidogo wewe unataka msaada wakati anayeteseka
kupiti kiasi ni binti.. anamuhitaji mama yake kwa wakati huu...

taka usi taka mam atafahamu
akifahamu mapema vizuri itakuwa vema.. kasheshe mpauko utaona lakini naomba usimtese binti wa watu kimawazo ... mwambie mama yake..

asante kaka kwa ushauri wako. maana hapa nilipo sijielewi kichwa kimepiga short ukizingatia baadhi ya waungwana wanalaumu zaidi kuliko kushauri. wakati maji yameshamwgika.....

Ngoja aje asome mwenyewe
 
Binadamu nyie....!
Haya zaeni aliekua mpenzi wako ageuke mama mkwe na bibi wa mwanao!!Kaazi kweli kweli!

Alafu huna aibu eti unaomba msaada wa kimaadili wakati maadili ushayavunja?!UNALO!!

kumbe alijua kabisa kuwa si maadili! Maana asingejua asingeomba ushauri wa kimaadili,jamaa amekosea sana mpaka nakosa cha kusema khe!
 
Yaani umekula kuku na mayai yake??halafu unataka mayai yaangue kuku tena mhh kha! Hiv ullianzaje tena na mtoto?

Mhh huyo mama akijua mbona patachimbika!! Ulikosea kukukubal kuwa na huyo mtoto?

Haya ngoja wataalamu wa mambo waje kukushaur
nifanyeje sasa baada ya kukosea?
 
Binadamu nyie....!
Haya zaeni aliekua mpenzi wako ageuke mama mkwe na bibi wa mwanao!!Kaazi kweli kweli!

Alafu huna aibu eti unaomba msaada wa kimaadili wakati maadili ushayavunja?!UNALO!!
sikukosea nilipoomba msaada wa kimaadili huku najua nimeyavunja,nimeamua kuwa wazi ili niweze kupata utatuzi baada ya mambo kuharibika. siku zote ushauri nasaha hutolewa kwa waliokosea na sio watakatifu,maana kadiri siku zinavyokwenda banti ndo anazidi kupanic na kichanga ndo kinazidi kukua.......
 
siku zote mtu anatakiwa ashauriwe ili kutatua tatizo lililopo mbele yake kuliko kumlaumu maana maji yamesha mwagika na nimeamua kuwa wazi kulileta tatizo langu humu jamvini ili kupata mawazo ya watu. maana kadiri siku zinavyokwenda binti ndo anazidi kuchanganykiwa. najitahidi kumsihi asimwambie mtu yoyote kwa sasa. nipe ushauri wa kunijenga kuliko kuzidi kunichanganya....

Ungekua unaujua umuhimu wa ushauri ungeomba kabla ya kutembea na huyo binti kuuliza kama ni sawa au la....sio unaenda kula raha huko alafu sasa unga umeanza kuumuka ndo unaomba ushauri!!
Huyo binti nae kwakweli ameniacha hoi....yani analala na mtu aliyewahi kumuita mjomba mpaka mimba???Kweli binadamu tunatofautiana!!

Nwy ni ngumu kukushauri cha kufanya maana bado hatujajua una maleno gani na huyo binti!!
Je mnataka kuoana???
Mnataka kuitwa wazazi ???
Au mlikua mnafurahishana tu kwa muda bila kua na malengo ya kua pamoja huko mbeleni??

Vyovyote vile siwashauri kutoa mimba japo huyo mtoto akija kukua atawashangaa sana siku akigundua kwamba ambae angeweza kua babu yake wa kufikia ndo amekua baba mzazi!!!Tafuta namna ya kumjulisha mama mtu...ushirikishe wazee wako watajua jinsi ya kufikisha na kumaliza yote kiutu uzima kitu ambacho nadhani wewe binafsi huwezi....alafu usirudie tena kufanya ushenzi kama huo mbeleni usije ukaachiwa laana siku si zako...nwy akishajua ataamua yeye kama anatoa msamaha au la!!Ila kujua kwake kutaacha nafasi ya binti kua na mtoto wake maisha yaendelee.Wewe usie na aibu usiendeleze aibu zako kwahiyo ikiwezekana achana na binti maana i can't imagine mmekaa meza moja na mama mkwe/mpenzi wako wa zamani mkipata chakula pamoja kama familia ila malezi ya mtoto uzingatie
 
Kama wewe ni mkristo omba msamaha kwa Mungu kwa unyenyekevu na katubu kanisani tena kwa mchungaji bila kuficha chochote, kisha nenda kwa mpenzi wako wa zamani/mama mkwe wako kamuombe msamaha kwa kumaanisha kabisa as if hamkuwa na mahusiano before
umuambie hali halisi. Kama ni muislam nenda kwa wakuu wako wa dini, ila Muombe Mungu akusamehe kwa dhati. ila kusema ukweli nimesikitika sana!
 
Hata mimi nakulaani , Umekosea sana. Sasa kama unampenda na unataka akuzalie unaomba ushauri wa nini tena?? Sijakuelewa alafu huna busara kabisa.
Ungetakiwa kumkwepa uyo ni mtoto wako kabisa. Alafu nimeshakugundua!
 
Ungekua unaujua umuhimu wa ushauri ungeomba kabla ya kutembea na huyo binti kuuliza kama ni sawa au la....sio unaenda kula raha huko alafu sasa unga umeanza kuumuka ndo unaomba ushauri!!
Huyo binti nae kwakweli ameniacha hoi....yani analala na mtu aliyewahi kumuita mjomba mpaka mimba???Kweli binadamu tunatofautiana!!

Nwy ni ngumu kukushauri cha kufanya maana bado hatujajua una maleno gani na huyo binti!!
Je mnataka kuoana???
Mnataka kuitwa wazazi ???
Au mlikua mnafurahishana tu kwa muda bila kua na malengo ya kua pamoja huko mbeleni??

Vyovyote vile siwashauri kutoa mimba japo huyo mtoto akija kukua atawashangaa sana siku akigundua kwamba ambae angeweza kua babu yake wa kufikia ndo amekua baba mzazi!!!Tafuta namna ya kumjulisha mama mtu...ushirikishe wazee wako watajua jinsi ya kufikisha na kumaliza yote kiutu uzima kitu ambacho nadhani wewe binafsi huwezi....alafu usirudie tena kufanya ushenzi kama huo mbeleni usije ukaachiwa laana siku si zako...nwy akishajua ataamua yeye kama anatoa msamaha au la!!Ila kujua kwake kutaacha nafasi ya binti kua na mtoto wake maisha yaendelee.Wewe usie na aibu usiendeleze aibu zako kwahiyo ikiwezekana achana na binti maana i can't imagine mmekaa meza moja na mama mkwe/mpenzi wako wa zamani mkipata chakula pamoja kama familia ila malezi ya mtoto uzingatie
Waw! waw! waw! waw!.....sasa naanza kupata mwanga. nachukua ushauri wako kwa kushirikisha wazee,japo siwezi kuwashirikisha wazazi wangu maana kama nilivyoeleza mwanzo mimi na mama ya binti tulikuwa hatujatambulishana,nisije ibua aibu nyingine....! itabidi nitafute watu wa pembeni. lengo langu ni endapo mama yake atakubali kunisamehe,nimuoe kabisa na nihamishe makazi nikaishi mbali na mama yake maana nampenda sana binti na sitaki ateseke sababu yangu..... unaonaje hilo......? nishauri tafadhari.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom