Nipo mkoani Mtwara naomba kujua upatikanaji wa mbuzi

Reality of heaven

Senior Member
Nov 2, 2022
108
350
Habari wakuu?

Mimi nipo mkoani Mtwara, nimefikiria kuanza biashara ya bucha ya mbuzi, changamoto ni upatikanaji wake! Na utaratibu wa kuanza hii biashara upoje! Naomba kwa mwenye uzoefu anisaidie! Namna ya kuwasafirisha, lakini vibali vyake, na mpaka kupata leseni! Naweza kuanza halafu nikashugulikia lesseni au mpaka uwe na kila kinachohitajika ndio nianze!

Naomba muongozo!

Natanguliza shukrani!
 
Kibali cha nini kwani we unasafirisha mikoani

Wewe fungua bucha kwa kufuata taratibu zote

Tafuta vijana, kijana wakua wanakutafutia mbuzi mitaani na vijijini kwa wafugaji

Peleka machinjio yaliyo karibu nawe bwana afya na mchinjaji utawakuta huko

Mpaka hapo nyama iko tayari kuuzwa .
 
Kibali cha nini kwani we unasafirisha mikoani

Wewe fungua bucha kwa kufuata taratibu zote

Tafuta vijana,kijana wakua wanakutafutia mbuzi mitaani na vijijini kwa wafugaji

Peleka machinjio yaliyo karibu nawe bwana afya na mchinjaji utawakuta huko

Mpaka hapo nyama iko tayari kuuzwa .
Nashukuru kwa mawazo yako! Ahsante Sana! Changamoto yangu kubwa ni upatikanaji wake!!ngoja nifanyie kazi wazo lako mkuu
 
Njoo uchukue nina Mbuzi 23 Dar kijana wa usimamizi chizi kabisa. Nawauza wote kama walivyo
 
Back
Top Bottom