Nipo kwenye dilema nzima

Andika hapa nini umemkosea Malkia wako tujue tunakusaidiaje?
 
Wewe bwabwaja hapahapa utapata ushauri. Kwani Kuna yeyote anaekufahamu hapa? Funguka
 
Sema kosa ulilofanya ili iwe rahis kusaidiwa, tambua kila kosa na namna yake ya kulizungumzia ili lipate ufumbuzi sio kwamba utatumia njia moja kwa kila kitu
 
hebu tulia kwanza,,kunywa maji kwanza
halafu tueleze nini kimekusibu..
 
niambie mm mdogo wangu...labda utaokota mawili matatu kwangu maana mm ni kaka kwako na sitakosa chochote..jungu kuu halikosi ukoko...njoo pm...ukitaka hata namba nitakupa naumia kuona watu wanajidhuru kwa kukosa ushauri hapa JF...pole na karibu
 
Mkuu unazingua kama sijafanya kosa la kufukwa kazi na kuyumba kimapato au either kwenda jela si hofu, ikiwa ni mahusiano yatakawa sawa tu, jipe shavu mkuu..
 
Wanaanzaga hivi hivi , then muda kidogo unasikia jamaa kajiua,
Wanasaikolojia na washauri nasaha , huu ni muda wenu muafaka kabisa kumsaidia jamaa, Ana stress sio kidogo
 
Siku zote tiba ya kwanza kabisa itayo uweka moyo wako huru na kupata ahueni ni kuweka wazi au kusimulia mzigo uliopo moyoni,utapata ushauri mbali mbali hapa na utachagua ulio sahihi...jaribu ku ongeza kitu hapo juu kwenye ujumbe wako,upate utatuzi wa tatizo lako jomba.
 
Back
Top Bottom