Nipeni dawa ya kuacha kupenda

happiness win

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
2,461
1,384
Toka mwanzo nilijitahidi nisipende kwa lengo la kukwepa kuumizwa. Kuna walionipenda sana na waliishia kuumia maana sikuwa tayari kupenda. Niliwaacha wakiumia na kulia mimi niliendelea kuishi kwa raha bila majeraha ya mapenzi.

Mmoja kati ya hao niliowahi kuwaumiza alinifata tena kwa machozi, nilijikuta narudiana naye na nilibaini nimempenda kikweli. Shida ikawa hana imani tena na mimi, mara kwa mara hukumbushia niliyomfanyia siku za nyuma. Hata nisipojibu simu kwa wakati ni maneno, kwa kifupi mapenzi yamekuwa kero na nimeshindwa kujizuia nampenda sana. Sijielewi hata imekuwaje nikatekwa kwa mapenzi kiasi hiki. Imefikia hatua nimemuomba aniache maana haniamini, anasema hayuko tayari ila eti mimi niendelee kumvumilia maana nilimharibu nilipomtenda. Cha kutisha ni kwamba ananitishia maisha endapo nitamkimbia na kumuacha. Nisaidieni niwezetoka kwenye mapenzi haya na nisipende tena.
 
anakutesa huyo wala hukepndi,kwenye mapenzi hakuna vitisho,kuna msamaha!kama ulimtenda na akahisi hajkusamehe na bado umerudiana nae unajiumiza tu!na kumpa nafasi ya kurevenge!hebu toke kwenye hayo mahusiano mara moja utakufa keli wala si kwa kuuliwa utajiua mwenyewe!
 
Usinihukumu bana, nipe ushauri niwe huru.

Haya basi ngoja nikushauri...
Jaribu kukaa chini muongee, umueleze jinsi unavyojisikia...mueleze ni nini unahitaji kutoka kwake na kama unahisi ulikua umekosea hapo mwanzoni kuachana naye basi huo ndio utakuwa wasaa wako wa kumuomba msamaha kwa kumaanisha.
Mueleze kuwa unatambua uliumiza moyo wake hapo awali, na kwa kutambua hivyo ulioona ni vyema kusahihisha kwa kurudia naye.
Baada ya hayo, malizia na hitimisho kali kuwa machungu yakizidi huna budi kumuacha(tafadhali sio kuachana), kama atakuwa ni mtu wa kukuhitaji basi itampasa afikirie mara mbili mbili.
 
Mambo si hayo! asante kwa ushauri. Nikiachana naye, sitapenda tena!
 
'matatizo ya mapenzi' ni matatizo ya 'shibe'
sasa ukiona wewe unasumbuliwa saana na mapenzi ujue
tatizo lako ni shibe iliyopitiliza

watu wenye njaa au shida kubwa za dunia hawana matatizo ya mapenzi....

hebu nenda kajiunge shirika la kujitolea
mfano NGO ya ku deal na watoto wa mitaani...
au mashirika ya kisheria yanayo deal na mahabusu na kadhalika
uone utakavyobadilika
 
revenge tatizo mnaamisha miili roho na akili zote mnawapa watembee nazo pooooor lady ,concentrate kwenye mambo muhimu
 
Toka mwanzo nilijitahidi nisipende kwa lengo la kukwepa kuumizwa. Kuna walionipenda sana na waliishia kuumia maana sikuwa tayari kupenda. Niliwaacha wakiumia na kulia mimi niliendelea kuishi kwa raha bila majeraha ya mapenzi.

Mmoja kati ya hao niliowahi kuwaumiza alinifata tena kwa machozi, nilijikuta narudiana naye na nilibaini nimempenda kikweli. Shida ikawa hana imani tena na mimi, mara kwa mara hukumbushia niliyomfanyia siku za nyuma. Hata nisipojibu simu kwa wakati ni maneno, kwa kifupi mapenzi yamekuwa kero na nimeshindwa kujizuia nampenda sana. Sijielewi hata imekuwaje nikatekwa kwa mapenzi kiasi hiki. Imefikia hatua nimemuomba aniache maana haniamini, anasema hayuko tayari ila eti mimi niendelee kumvumilia maana nilimharibu nilipomtenda. Cha kutisha ni kwamba ananitishia maisha endapo nitamkimbia na kumuacha. Nisaidieni niwezetoka kwenye mapenzi haya na nisipende tena.

Fanya lililo lako ndugu yangu maana nakuapia kama ukiishi kwa kwa kuogopa kutishiwa maisha, utateseka sana na mwishowe utayapoteza tu. Mara nyingi watu wenye kuyajari sana maisha huishia kuwa watumwa maisha yao yote na umaskini huwa ni sehemu ya maisha yao.
 
ndo tatizo la kupenda wanaume wenye ghubu na wasiojiamini...........

na ndo tatizo la kutojithamini, kujitambua na kuipa nafsi yako kipaumbele...

Toka mwanzo nilijitahidi nisipende kwa lengo la kukwepa kuumizwa. Kuna walionipenda sana na waliishia kuumia maana sikuwa tayari kupenda. Niliwaacha wakiumia na kulia mimi niliendelea kuishi kwa raha bila majeraha ya mapenzi.

Mmoja kati ya hao niliowahi kuwaumiza alinifata tena kwa machozi, nilijikuta narudiana naye na nilibaini nimempenda kikweli. Shida ikawa hana imani tena na mimi, mara kwa mara hukumbushia niliyomfanyia siku za nyuma. Hata nisipojibu simu kwa wakati ni maneno, kwa kifupi mapenzi yamekuwa kero na nimeshindwa kujizuia nampenda sana. Sijielewi hata imekuwaje nikatekwa kwa mapenzi kiasi hiki. Imefikia hatua nimemuomba aniache maana haniamini, anasema hayuko tayari ila eti mimi niendelee kumvumilia maana nilimharibu nilipomtenda. Cha kutisha ni kwamba ananitishia maisha endapo nitamkimbia na kumuacha. Nisaidieni niwezetoka kwenye mapenzi haya na nisipende tena.
 
mapenzi ni safari ndeefu so ndio kwanza upo stendi so usikate tamaa na wala usiulaumu moyo wako kwa kupenda na hiyo ni nafasi pekee au bahati uliyo pewa na MUNGU kwani hakuna kitu kizuri duniani kama upendo ( wa aina yoyote ile ) na usiombe ukachukia ni bora kupenda
chakufanya tikisa kiberiti jifanye kama humpendi sanaaa atajirudi mwenyewe
 
utapenda tu lol,haya mambo hayaepukiki,sema utakuwa umejifunza mengi

Mapenzi yanaumiza sana. Sidhani kama nitatamani tena kurudia maumivu haya. Ni heri nikawa mpita njia tu kwenye mapenzi kwa lengo la kujiridhisha mwenyewe!
 
Toka mwanzo
nilijitahidi nisipende kwa lengo la kukwepa kuumizwa. Kuna walionipenda
sana na waliishia kuumia maana sikuwa tayari kupenda. Niliwaacha
wakiumia na kulia mimi niliendelea kuishi kwa raha bila majeraha ya
mapenzi.

Mmoja kati ya hao niliowahi kuwaumiza alinifata tena kwa machozi,
nilijikuta narudiana naye na nilibaini nimempenda kikweli. Shida ikawa
hana imani tena na mimi, mara kwa mara hukumbushia niliyomfanyia siku za
nyuma. Hata nisipojibu simu kwa wakati ni maneno, kwa kifupi mapenzi
yamekuwa kero na nimeshindwa kujizuia nampenda sana. Sijielewi hata
imekuwaje nikatekwa kwa mapenzi kiasi hiki. Imefikia hatua nimemuomba
aniache maana haniamini, anasema hayuko tayari ila eti mimi niendelee
kumvumilia maana nilimharibu nilipomtenda. Cha kutisha ni kwamba
ananitishia maisha endapo nitamkimbia na kumuacha. Nisaidieni
niwezetoka kwenye mapenzi haya na nisipende tena.

hapy lol,wewe huwa unapendelea kufanya kitu gani?interest zako i mean
 
Back
Top Bottom