Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,655
Hatuwezi kumaliza suala la madawa ya kulevya kwa nguvu peke yake. Matatizo ya kijamii ambayo tunayokabiliana nayo sasa ni lazima tuyaangalie katika mifumo yetu ya makuzi na malezi na mahusiano yetu. Lazima tuangalie katika tabia tunazozijenga kwa watoto wetu na vijana wetu. Kuwafunga watu kwasababu ya kutenda visivyo sahihi pasipo kuwa na mifumo mizuri ya malezi na makuzi ni kuendelea kila siku kuongeza gharama katika kujenga vituo vya polisi na jela wakati tunaweza kuzuia haya mambo kama tukiwa na malezi na makuzi mazuri. Na kama tutatoa elimu bora ya maadili kwa watu wetu.
Ni lazima tufanye hivi ili kupunguza uhalifu na matumizi ya hela nyingi kwenye kudhibiti uhalifu. Watoto wetu kama hawamjui Mungu hakuna tutachofanya kuwaokoa kutoka kwenye madawa ya kulevya na tabia nyingine zenye madhara kwa wao wenyewe na kwa jamii. Hakuna tutakacho kijenga. Hakuna kitakacho heshimiwa iwe ndoa au jamii.
We Must return to God.