Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,181
Nakumbuka mwaka 1997 Mkapa alimteua aliyekuwa Waziri wa madini na nishati Dr. Abdallah Kigoda kuwa mweka hazina wa CCM.
Mikataba ya madini ilipewa misamaha ya kodi ya kutisha hata tozo za mafuta wakaondolewa. Mkapa alidai wawekezaji "wasibughudhiwe'
Kipindi hicho ukwasi wa CCM ulichemka wakanunua magari nchi nzima kwa makada wao. Uhusiano wa misamaha ya kodi na utajiri wa kutisha wa CCM ulikuwa wazi.
Kwenye kampeni za ubunge na urais mwaka 2000 CCM walikuwa " loaded" kishenzi na ni hizo ruzuku kwa wawekezaji wakubwa wa dhahabu.
Baadaye, Said Mwema aliyekuwa IGP akageuka kuwa star wa movie ya James Bond " A man with a golden gun" mithili ya Saddam Hussein wa Irak na Muammar Kadaf wa Libya. Naye ni mmiliki wa bastola ya dhahabu!
Mkapa naye alivuna bonge la tufe ya gold. Alipoishia haijulikani hatma ya hilo tufe la dhahabu.
Arusha, mkuu wa mkoa wa enzi zile Njoolay alitishia wakiondolewa Tanzanite One yeye yuko tayari kujiuzulu ukuu wa mkoa huku zikizagaa tetesi kila mwezi alikuwa akipelekewa kilo ya Tanzanite ya grade B yenye thamani ya zaidi ya Tshs 160 mill za wakati ule.
Tukiangalia uzoefu wa mapambano ya ccm na wawekezaji tunaona ni sisi huishia kuumia.
Pitia Dowans, Iptl, Aggrecko n.k utakuta ni.michoro ya kutuachia maumivu.
Hebu tuangalie hii movie ya Acacia.
1) Tume ya Prof. Mruma imekiuka mkataba na Acacia ambao inaelekeza migogoro kusuluhishwa na msuluhishi huru anayekubalika na pande mbili husika na kuifanya taarifa ya Prof. Mruma kuwa ni majungu au soga za mtaani hazina nguvu ya kisheria.
2) Tuliwafukuza Dowans wakaenda kwa msuluhishi huru tukalizwa na hawa Acacia ndiko watakapotufunzia adabu ya kuheshimu mikataba.
3) Kuwazuia kuchimba dhahabu nako ccm inawajengea mazingira mazuri ya kudai fidia ya kukwaza kutekeleza majukumu yao ya kimikataba.
4) Kero za kimikataba na sheria zinapotatuliwa kwa ubabe na vitisho ujue panapofuka moshi kweli panaficha moto.
Nionavyo
Hii ni hela ya uchaguzi wa 2020 ccm inaitafuta kupitia Acacia. Uchaguzi wa 2015, hela ilitokea kwa TEGETA Escrow account sasa ni zamu ya Acacia Gold miners!