Ninywe Pombe gani wakuu?

NGULI

JF-Expert Member
Mar 31, 2008
4,803
637
Wakuu,

Nimegundua ili ufanikiwe kama mfanya biashara au mfanyakazi wa ofisini inakulazimu kunywa pombe, kwa bahati nzuri au mbaya tangu nimezaliwa 2 decades na ushee ago, sijawahi kunywa pombe aina yeyote kwa sababu hiyo nimekuwa mbali na mafanikio kazini. Katika kudadisi kwangu nimegundua mabosi wengi ni wachapa maji wazuri na wanapenda wanywaji.

e.g juzi nimeomba kazi shirika moja linalohusika na biashara ya fedha, kwenye interview HR aliniuliza "do u normaly drink alcohol ? nikasema no!", akauliza tena no, means.... not at all or u drink ocassionaly nikamwambia hata harufu sinusi, akaniambia sasa utaperform vp kazi wakati unatakiwa ukutane na wazee gymcana club, kilimanjaro hotel na new africa, au utakuwa unapiga chai kila siku? nikajibu kwa tabasamu yes. Na ile kazi nimekosa kabisa.

Wanaokunywa pombe kwa kiasi huwa wanapanda vyeo kila kukicha kwa vile wanakutana na mabosi maeneo ya mabaa na wana motivate-ana hukohuko.

Kwa wafanya biashara deals hufanywa bar na sio kwenye grocery na maji ya kunywa kama nifanyavyo mimi.

Kama nilivyoeleza hapo awali sijawahi kugusa pombe nianze na ipi mdogomdogo ili nisi over dose? au ipi Tamu zaidi?
 
tafuta kidumu cha lita tano.......halafu nenda kitunda kuna gongo moja safi sana inaitwa namba one ukiiwasha na moto inawaka
 
tafuta kidumu cha lita tano.......halafu nenda kitunda kuna gongo moja safi sana inaitwa namba one ukiiwasha na moto inawaka

Kwa hio na mimi si nitawaka kabisa? unataka nife nn?
 
Kiongozi,

Karibu kwenye klabu ya wanywa Serengeti.... Tuna bahati ya kupendwa na mabaamedi pia.
 
Usifate mkumbo.
Kipato chako chenyewe kinaonekana kidogo halafu unataka ukifyeke huko jamani!!
 
Kunywa coctail ya Gongo nusu glass uchanganye na cyanide robo glass. Hii ni guarantee.Bosi wako atakupenda na utapwea Pomotion mara moja:Cry:
 
kuna kile tunachoshirikigi madhabahuni.....hivi huwaga ni nini kile huku uraiani?...kinaitwaje?
 
Changanya Kiroba na Valuu glasi moja kwa siku mara 5 hivi..hii ni kwa kuanzia..
 
Back
Top Bottom