Ninyi wasichana, kwa nini hii tabia lakini?

Ninyi wasichana, kwa nini hii tabia lakini?

B.G TANTAWI

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2013
Posts
496
Reaction score
379
Mabinti wanakera sana, am very sorry for ladies!

kwa sasa nimefikisha wasichana kama wanne hivi kuwachumbia na kama kawaida kuna swali wananiuliza "Una kazi"? wakati huo huo kati ya hao wanne, ni mmoja tu ndiye ana kazi but the rest ni jobless, sasa wa kwanza nilimjibu kuwa "sina kazi" nikamuuliza "wewe una kazi"? akasema hana khaaa!! nilijisikia vibaya sana kwa swali lake hilo, akasema kama huna kazi "nipotezee" kumbuka wakati huo ki-uhalisia mimi nina kazi na nimeajiriwa! wa pili hivo hivo, wa tatu hivo hivo ila yeye nikamwambia kuwa mimi ni mmachinga tu na nilikuwa nimevaa hovyo hovyo, akasema "sipo tayari" ss wa nne yeye akaniuliza una kazi gani? nikamwambia mimi ni "mkulima tu" nalima mboga mboga nauza soko kuu hapa kariakoo, akasema Mhh! haya bwana nidanganye tu, naye siku hiyo nilikuwa nimevaa hovyo hovyo sana, akasema yeye haangalii "kazi ya mtu" na yupo tayari. kweli kabisa ndo mchumba wangu na mwezi ujao tunaoana.

My take: wasichana muwe makini sana.
 
unatakiwa umshukuru Mwenyezi Mungu wako kwa kuwa waliokusumbua ni hao wawili watatu tu...wangekuwa wengi wangekupa kichaa...hongera sana kwa kupata mchumba...ubwabwa twala lini?lol!
 
unatakiwa umshukuru Mwenyezi Mungu wako kwa kuwa waliokusumbua ni hao wawili watatu tu...wangekuwa wengi wangekupa kichaa...hongera sana kwa kupata mchumba...ubwabwa twala lini?lol!
Hilo nalo la msingi asije akawa anabwabwaja hapa kumbe huo ubwabwa siyo leo wala kesho halafu aje atuambie na huyo amemsumbua kama wengine!
 
we unatongoza bwana kuchumbia ni hatua kubwa,,.... ki ukweli mwanaume kama huna kazi utaishije kwel.i utakula nyasi hata kama ni me siwezi kukubali... mwanaume kazi msemo wa nipende kama nilivyo ni zamani wakati hata usipokuwa na kazi unaweza lima na kupata chakula kwa kipindi hichi huna hata kibarua sijui utaishije may be uwe omba omba,...
 
Labda walifikiria kuwa kama wao hawana kazi na wewe huna kazi maisha yatakuwaje!
Ingawa fikra hizo zinaweza kuwa si sahihi na si maamuzi ya busara kwa wale ambao ni ma-fighters lakini wamekosa bahati ya kupata kazi ai mitaji ya kuendeleza shughuli zao. Mapenzi hayapaswi kuchanganywa na pesa!
 
Inamaana ulikua unawaona siku hiyo hiyo na kuwatangazia uchumba... wewe ni noma!!!!!!!!!!!!
 
SERA YA MUJINI....Mkono mtupu haulambwi.... Kazi inaashiria nguvukazi na bila kazi inaashiria mvivu.
 
we unatongoza bwana kuchumbia ni hatua kubwa,,.... ki ukweli mwanaume kama huna kazi utaishije kwel.i utakula nyasi hata kama ni me siwezi kukubali... mwanaume kazi msemo wa nipende kama nilivyo ni zamani wakati hata usipokuwa na kazi unaweza lima na kupata chakula kwa kipindi hichi huna hata kibarua sijui utaishije may be uwe omba omba,...
Mh!. Kwa hiyo unataka kuolewa na vitu viwili kwa pamoja, unahitaji mwanaume na at the same time you need his job. Kweli kwa mtindo huo mtaishia kupigwa mimba tu na hakuna kuolewa
 
umeona eeh!
Mh!. Kwa hiyo unataka kuolewa na vitu viwili kwa pamoja, unahitaji mwanaume na at the same time you need his job. Kweli kwa mtindo huo mtaishia kupigwa mimba tu na hakuna kuolewa
 
Daaanh ndio imefikia huko???!!!!

Haya bana sie wengine tulibahatika basi!!!!!!
 
Ngoja na mimi nitafute mmoja nimtongoze tuone na ubaba paroko wangu kama atanikatalia...lol!

Eti kondoo wangu na mhudumu wa mahitaji yangu ya kichungaji Husninyo nitakataliwa?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom