Nini vipaumbele vya Serikali ya awamu ya sita?

Nimekuwa nikifuatilia Hotuba za Rais kila kukicha ila sijaelewa vipaumbele vya serikali ya awamu ya sita. Mara madarasa, mara zahanati, mara kwenda ulaya. Kwa ufupi ninaona kwama tumepoteza uelekeo
Ngoja nikusaidie kujibu swali lako.
Kipaumbele alikitamka mara tu alipotembelea nchi jirani kwamba ni "Kufungua nchi," akiwa na mategemeo kwamba hao anaowafungulia ndio watakaotuletea maendeleo.
Hili amelisisitiza mara kadhaa ila nadhani wewe hukulitilia maanani. Machinga wanaondollewa sehemu zao za kazi, kumbe sio kwa sababu nyingine bali wanawatisha tunaotegemea watuletee maendeleo.
Binafsi sijamsikia kwa masikio yangu akisisitiza uwezo wetu wa kujiendeleza, na wala sijaona mipango ikifanyika ili juhudi zetu mbalimbali huko mashambani au mitaani ziweze kuungwa mkono ili zifanikiwe kutuletea maendeleo.

Si unaona jinsi anavyohaha na kuomba omba misaada kila anapopata nafasi ya kufanya hivyo? Anaamini kabisa kwamba bila ya misaada hii hatuwezi kamwe kupiga hatua ya maendeleo. Tukipewa misaada tutaendelea!

Kwa hiyo swali linalofuatia hapo baada ya kujuwa kipaumbele chake ni kukubali au kukataa hiyo dhana anayoiamini yeye.
 
Hizo CT scanner anazonunua mikoa yote ni kipaumbele chako?

Miradi ya kimkakati SGR,NYERERE HYDROELECTRIC DAM vyote havinakamilika wewe unataka vipaumbele vingine kwa pesa zipi?

Mama ametoa pesa kila wilaya miradi lukuki, halafu wewe unakurupuka na k-vant imekujaa kichwani unaleta maswali ya kilevi humu?
Acha upuuuz ww katoa pesa zake anapesa za kutoa kwenye mfuko wake wa Dela? Pesa za walipa kodi acha kuwa chai maharage ww
 
Vipaumbele vipo vingi sana mfano tu.
1. Mapambano dhidi ya UVIKo
2 Mapambano dhidi ya Wapinzani
3 Kupanda mapipa
4 kufuata nyayo za marehemu japo sijui hadi wapi
5 Uchaguzi 25
 
Hahahaaaa, WACHAWI bwana!
Sasa tufanye hivi, hana vipaumbele vyovyote hivyo nendeni tu mkamtoe na mumuweke huyo polepole tupumzike kelele
Na atakiangusha chama chenu 2025 endeleeni kumsifia
Refer to Joyce Banda
 
Vipaumbele vya awamu ya sita ni kumalizia miradi yote ya awamu ya tano ili isiishie njiani na kubakia magofu.

Kipaumbele cha pili ni kuwa rafiki na jumuiya ya kimataifa, ndio maana Mulamula akapewa nafasi ya uwaziri wa mambo ya nje ili uzoefu wake urudishe uhusiano mwema na mataifa haswa yale makubwa duniani.

Kipaumbele cha tatu ni kuhakikisha nchi nzima inapata maji, miradi mikubwa inafunguliwa miaka ya sasa.

Huo ni mueleko tosha kabisa. Kikao kama kile cha COP26 kuhudhuriwa na rais mwenyewe ni sehemu tu ya umakini wa muelekeo mzima wa awamu ya sita.
Utakua ni mtoto wa diwani wa ccm
 
Nimekuwa nikifuatilia Hotuba za Rais kila kukicha ila sijaelewa vipaumbele vya serikali ya awamu ya sita. Mara madarasa, mara zahanati, mara kwenda ulaya. Kwa ufupi ninaona kwama tumepoteza uelekeo
unapenda sana mipasho- Rais alitaja vipaumbele vyake alipolihutubia taifa kupita bunge la JMT
 
Back
Top Bottom