Nini utafanya kama ni wewe?

jaffari yogo

JF-Expert Member
Apr 3, 2014
687
225
Mke alimuaga mumewe anaenda kumsalimia mama yake mgonjwa kijijini. Akaondoka Ijumaa na kurudi Jumatatu na matunda kibao na vyakula vingine toka kijijini akisema ni mama kanipa kwa ajili yako mume wangu na watoto, mume akamuuliza kwa upole mama anaendeleaje? Mke akajibu amempeleka hospitali ila anaendelea vema, mke aliongezea kwamba mama yake amemsisitiza amtembelee tena baada ya siku chache akae naye wiki, nina hofu na afya ya mama mke aliongea kwa uchungu huku machozi yanamtoka.
Mume akamjibu kwa huruma atapona mpenzi usijali. Mume akamwambia kwa hekima ingiza vitu ulivyoleta jikoni. Mke ile anaingia jikoni anamkuta mama yake mzazi akiandaa chakula jikoni. Kumbe mama ake alikuja kumtembelea tangu Ijumaa yeye alivyoondoka. Mke akabaki ameduwaa mlangoni mwa jiko asijue apeleke vitu jikoni au arudi sebuleni kwa mume wake.
Je ingekuwa wewe ungefanyaje....?
Toa maoni ama mawazo yako ya busara yanahitajika.
 

mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,401
2,000
Ningelikaa sebuleni niangalie TV. Baadaye, nile chakula alichonipikia mama mkwe bila kusema chochote. Nikimaliza kula, naenda kulala kimya kabisaaa.
Asubuhi, hatakuwepo ndani ya nyumba hiyo kwani atajipa talaka mwenyewe. Mwanamume kelele ndio mwisho wa hasira. Kimya kingi, ndio ushindi mkuu
 

Joseverest

Verified Member
Sep 25, 2013
42,855
2,000
Ningesubiri nione mke wangu atanidanganya vipi... asipotoa maelezo ya kutosha mbona kitaeleweka
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom