Nini tofauti ya neno "kuvuma" na" Kuvurumisha"?

Kwa mujibu wa kamusi ya TUKI 2013

Vuma¹: toa sauti nzito,mfano upepo,ngoma, nyuki, maji

Vuma²: zungumziwa/julikana na watu wengi

Vuma³: enda kwa kupita Haraka.

Vurumisha/vurumiza/ngurumiza/vungumiza: tupa kitu kwa nguvu

Kutokana na maana hizo vuma ni kama nomino ya tukio na vurumisha ni utendekaji wa tukio(kitenzi).

Hivyo sentensi Zako Zina makosa kidogo. Zilitakiwa ziwe

1:Makombora yalivuma

2:Wanajeshi walivurumisha makombora

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa maelezo ya kina,ila bado sijelewa kwanini sentensi yangu ya kwanza ina makosa kwa sababu umetoa tafsiri ya

Vuma³: enda kwa kupita Haraka

maana yake hicho ni kitenzi hivyo kusema
Wanajeshi 'walivuma' makombora maana yake waliyarusha/kufanya yaende kwa kupita haraka.

Ukisema makombora yalivuma
maana yake umetumia tafsiri uliyotoa mwenyewe namba 1,ambapo umesema

Vuma¹: toa sauti nzito,mfano upepo,ngoma, nyuki, maji

Hapo maana yake makombora yalitoa sauti nzito kama upepo,ngoma nk

Hivyo naamini sentensi yangu ya kwanza ipo sahihi ukitumia tafsiri ya tatu na pia sentensi yako ipo sahihi ukitumia tafsiri ya kwanza.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Farolito,
Ukitumia tafsiri ya tatu kwa sentensi yako si fahafu Kwanza haina upatanisho wa Kisarufi.
Vuma³ : Enda kwa kupita haraka
1. Makombora yalivuma✔
2. Wanajeshi walivuma makombora✖
Sentensi ya Kwanza Ni sahihi Kwa sababu kinachopita kwa haraka Ni makombora na si wanajeshi. Pia, imefata arudhi ya lugha.
 
Mods nyuzi za kitoto hizi.

Maswali ya kidato cha pili haya.. kama akili ikiwa sawasawa hili ni lakujiuliza binafsi.
🤔That why now days nyuzi nyingi lakini nyepesi nyepesi sana.
 
Back
Top Bottom