Salaam
Nimesikiliza kipindi kilichokuwa kinarushwa na Clouds radio leo katika kuadhimisha siku ya ufahamu kuhusu ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi " albinism awareness day".
Pamoja na kujifunza vitu vingi kuwahusu nimevutiwa na wito alioutoa mgeni wa kipindi kwa Mh. Rais Magufuli kwamba aharakishe kusaini adhabu za kunyongwa hadi kufa wale waliopatikana na hatia ya kuwauwa hawa ndugu zetu kwa imani za kishirikina.
Binafsi naunga mkono jitihada za kupinga kwa nguvu zote mauaji yao(Nasikia wauaji wameshaingia Malawi na kuna mauaji yametokea huko).
Pamoja na yote nimepata shida kidogo baada ya mgeni wa kipindi kusema Zeruzeru sio jina zuri kuwaita wenzetu hao ila akapendekeza tuwaite Albino sasa najiuliza nini tofauti ya majina hayo?
Hebu wajuzi wa lugha mnidadavulie!