Nini tofauti kati ya mzimu na pepo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini tofauti kati ya mzimu na pepo

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by LIKUD, Jul 10, 2013.

 1. LIKUD

  LIKUD JF-Expert Member

  #1
  Jul 10, 2013
  Joined: Dec 26, 2012
  Messages: 3,854
  Likes Received: 781
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Picha ya mzimu.  [​IMG]

  Picha ya Pepo ( Demon )


  NINI TOFAUTI KATI YA MZIMU NA PEPO ?

  Watu wengi hawajui tofauti iliyopo kati ya mzimu ( Ghost ) na pepo ( Demon ). Tofauti ni hii hapa.
  MZIMU NI NINI?
  Zipo nadharia nyingi zinazo elezea mzimu ni kitu gani, nadharia iliyo zoeleka ni ile inayosema mzimu ni roho ya mtu aliye kwisha kufa. Mtu huyo anaweza kuwa amekufa zamani sana, ama muda mfupi ulio pita. Sitaizungumzia sana nadharia hii leo, isipokuwa nitazungumzia kwa ufupi nadharia nyingine inayo jibu mzimu ni kitu gani.
  Mzimu ni nishati ( energy), roho au haiba ( personality) ya mtu ambaye amefariki dunia lakini imekwama katika sehemu iliyo kati ya duniani ( ulimwengu wa nyama/ulimwengu unao onekana ) na mahali ambapo roho hiyo inatakiwa kwenda kuishi baada ya maisha ya hapa duniani kukamilika ( ulimwengu usio onekana/ afterlife/ land of the souls )
  . Watafiti wengi wana amini kuwa roho hizi zinakuwa hazijui kama zimekufa katika ulimwengu wa nyama ama hazitaki kuamini kama zimekufa katika ulimwengu wa nyama ama hazikubaliani na kifo chao katika ulimwengu wa nyama. Mara nyingi roho hizi huwa ni roho za watu ambao walikufa katika mazingira yanayo tatanisha kama vile kufa kwa kuuliwa bila sababu ( cold blood), kutolewa kafara, ama kufa baada ya maisha ya msukuleni. Kwa ufupi hizi huwa ni roho za watu ambao walidhulumiwa haki yao ya kuishi hapa duniani. Mizimu inaweza kujidhirisha na kuonwa na wanadamu ama wanyama katika namna tofauti tofauti kama vile muonekano ( hapa mizimu ,huwatokea ndugu, jamaa na marafiki zao wakiwa katika maumbo ya sura zao wakati wanaishi duniani na mara nyingi huwatokea wakiwa na nguo walizo penda kuzivaa wakati wa uhai wao ), sauti, harufu( hapa kwenye harufu mzimu unapo mtokea muhusika,hujidhihirisha kwa harufu yake ya mwili ( kila mtu ana harufu yake ya mwili, watu huweza kuwatambua watu wao wa karibu kwa harufu zao za mwili ), ama pafyumu ( katika pafyumu, mzimu utamtokea mtu kwa harufu ya marashi ambayo alikuwa anapenda kuyatumia wakati yupo duniani katika ulimwengu wa nyama. Wakati mwingine, mzimu huweza kuwatokea ndugu jamaa na marafiki zake kwa kuwashika.

  Kwa ufupi mzimu huwa ni roho ambayo imewahi kuishi katika ulimwengu wa nyama kama mwanadamu ama mnyama.

  PEPO ( DEMON ) Hawa ni roho waovu ambao hawajawahi kuwa wanadamu .Mara nyingi mapepo huwa na mitego mingi na huwa na tabia za kitoto kitoto sana ( Nitalizungumzia hili hapo baadaye ). Haiwezekani kuwazungumzia mapepo kwa parandesi moja pekee, hii ni kwa sababu kuna mambo mengi sana ambayo yanatakiwa kuzungumzwa kuhusu mapepo, maelezo ninayo yatoa hapa yanawazungumzia mapepo katika namna ambayo wanatofautiana na mizimu.

  N.B: Mapepo ni wajanja sana, wakati mwingine huweza kuwatokea ndugu, jamaa, na marafiki wa mtu ambaye amekufa wakijifanya wao ndio roho wa mtu huyo na hivyo kuanza kutoa maelekezo ya kufanya kwa ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu ambapo mwisho wa siku, wahusika wanajikuta wakiwa wamefungwa na nguvu za giza zitendazo kazi zake kutoka kuzimu. Ni muhimu sana kujua namna unavyo weza kutofautisha kati ya roho ya mtu aliyekuwa anaishi na roho za mapepo hawa ambazo huwatokea wahusika kwa ajili ya kuwadanganya..

  TOFAUTI kubwa kati ya mizimu na mapepo ni kwamba, mizimu ni roho za watu ambao waliwahi kuishi hapa duniani kama binadamu ilihali mapepo ni roho ovu ambazo hazijawahi kuishi duniani kama wanadamu.
  MASWALI MENGINE

  1. Kuna aina ngapi za mizimu? ( Kuna mizimu mibaya na mizuri )
  2. Mizimu inaishi wapi, inakula nini?
  3. Mizimu ina nguvu kiasi gani na nguvu za mizimu zinaweza vipi kuwaathiri wanadamu?
  4. Je wanyama kama mbuzi, mbwa, nÂ’gombe, nyau, samba, chui, tembo n.k,. nao huwa wana mizimu?
  5. Kati ya mizimu na mapepo nani mwenye nguvu kubwa kuliko mwenzake?

  Kwa majibu ya maswali haya na mengine, tafadhali tembelea: ULIMWENGU USIONEKANA

  Kama una swali lolote kuhusiana na masuala haya ya kiimani, tafadhali niandikie : mungwakabili@gmail.com

  " MIMI NI MUNGU NIKUFUNDISHAYE ILI UPATE FAIDA........ISAYA 48;17 "
   
 2. T

  Truth Matters JF-Expert Member

  #2
  Jul 10, 2013
  Joined: Apr 12, 2013
  Messages: 832
  Likes Received: 257
  Trophy Points: 80
  Holy Ghost je? Ni mzimu au pepo?
   
 3. LIKUD

  LIKUD JF-Expert Member

  #3
  Jul 10, 2013
  Joined: Dec 26, 2012
  Messages: 3,854
  Likes Received: 781
  Trophy Points: 280
  Holy GHOST sio mzimu wala sio pepo. He is the MOST HIGHEST LEVEL OF EXISTENCE. Ninaomba tusimzungumzie hapa kabisa. Sawa ?
   
 4. T

  Truth Matters JF-Expert Member

  #4
  Jul 10, 2013
  Joined: Apr 12, 2013
  Messages: 832
  Likes Received: 257
  Trophy Points: 80
  Hii thread inahusu GHOSTS na DEMONS lazima tujadili bila woga! Kama vipi iondoe thread
   
 5. LIKUD

  LIKUD JF-Expert Member

  #5
  Jul 10, 2013
  Joined: Dec 26, 2012
  Messages: 3,854
  Likes Received: 781
  Trophy Points: 280
  Nimeshakujibu.
   
 6. T

  The Prezident JF-Expert Member

  #6
  Jul 10, 2013
  Joined: Jul 2, 2013
  Messages: 461
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  .... Bila kutafuna maneno ... Mzimu inahusu Mwanadamu aliyewahi kuishi sasa amekufa na anajitokeza kwa njia mbalimbali.

  Pepo haina uhusiano na mwandamu aliye mfu ....!!
   
 7. LIKUD

  LIKUD JF-Expert Member

  #7
  Jul 10, 2013
  Joined: Dec 26, 2012
  Messages: 3,854
  Likes Received: 781
  Trophy Points: 280
  Asante kwa kunielewa
   
 8. dibwinhe

  dibwinhe Senior Member

  #8
  Jul 10, 2013
  Joined: Feb 12, 2013
  Messages: 102
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  acha nitoe elimu,mzimu ni mashetani yaliyoishi katika vichwa vya mababu na mababa yanayodumisha mila za ukoo huo au kabila hilo,yanatoa maelekezo kupitia ndoto,yanauwezo wa kujigeuza sura ya mababu zako na mababa zako waliopita na kutoa maelekezo ndotoni,Pepo ni mashetani waasi wanaomshawishi mwanadamu kwenda kinyume na maamrisho ya mungu muumba,si pepo wala si mzimu ambao wana asili ya binadam
   
 9. dibwinhe

  dibwinhe Senior Member

  #9
  Jul 10, 2013
  Joined: Feb 12, 2013
  Messages: 102
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  life span yao ni kubwa zaidi ya mwanadamu,wanauwezo wa kuishi mara 5 zaidi ya umri wa binadamu
   
 10. Ibambasi

  Ibambasi JF-Expert Member

  #10
  Jul 11, 2013
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 6,634
  Likes Received: 2,444
  Trophy Points: 280
  Holy Ghost, malaika, majini, mizimu, pepo, wote ni wale wale tu. inategemea wewe unayewatazama unasimamia upande gani.
   
 11. Christine1

  Christine1 JF-Expert Member

  #11
  Jul 11, 2013
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 12,259
  Likes Received: 1,195
  Trophy Points: 280
  U a ryt!...bt pia hao wazee walikuwa wakiyaabudu,mf kwa kufanya matambiko! ndo maana utasikia mizimu ya ukoo! Simply ni tawi la lucifer(shetani/ibilisi)wanacontrol mambo ya ukoo!..na sio kwamba wanatokana na binadamu ila hyo ni kazi ya lucifer, amewagawanya kwa kazi mbalimbali, so walikuwepo b4 binadam....waliowahi kuishi! Bt wanatumia sura zao kuwatokea watu wao wanapowapa maelekezo kwa njia ya ndoto nk.
   
 12. Christine1

  Christine1 JF-Expert Member

  #12
  Jul 11, 2013
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 12,259
  Likes Received: 1,195
  Trophy Points: 280
  Mkuu,kwa uelewa wangu, ukitoa malaika wanaobaki ndo wamoja!
   
 13. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #13
  Jul 11, 2013
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Holy Ghost na Malaika wanasimama upande mmoja; majini na mapepo ni wale wale tu......, kwa lugha nyingine wanaitwa Shetani!! Hawa MIZIMU hawa....dah, cjui bhana coz' hadi naandika haya bado nimekuwa nikiwachukulia ni sawa na simulizi za Samaki Nguva kuwa na matiti kama mwanadamu mwanamke! Sincerely, siamini kabisa what's so called MIZIMU do exist.
   
 14. Ibambasi

  Ibambasi JF-Expert Member

  #14
  Jul 13, 2013
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 6,634
  Likes Received: 2,444
  Trophy Points: 280
  Kwa nini uwatoe malaika?
   
 15. Ibambasi

  Ibambasi JF-Expert Member

  #15
  Jul 13, 2013
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 6,634
  Likes Received: 2,444
  Trophy Points: 280
  Ni upande upi huo wanaosimama malaika?

  Ni kwa nini majini na mapepo wawe wale wale ila malaika sio wale wale?

  Ni kwa nini malaika wasiitwe shetani?

  Kwa nini mizimu wasi-exist wakati malaika, mapepo na majini wa-exist? Kwa maana nyingine, ulishawahi kuwaona malaika, majini na mapepo?
   
 16. babe S

  babe S JF-Expert Member

  #16
  Jul 13, 2013
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 3,703
  Likes Received: 19,819
  Trophy Points: 280
  Yap Christine, n ukoo au familia inapoacha kufanya hizo ibada au mitambiko mizimu huanza kuwatesa, n it is soo true kua yote ni matawi ya shetani ili tu kuwafunga na kutumikisha tu watu vibaya.
   
 17. LIKUD

  LIKUD JF-Expert Member

  #17
  Jul 13, 2013
  Joined: Dec 26, 2012
  Messages: 3,854
  Likes Received: 781
  Trophy Points: 280
  Umewahi kusikia kisa chochote kuhusu mtu kuteswa kwa kutokewa mara kwa mara na roho ya mtu ama watu alio waua kwa makusudi? Ama una amini ukidhulumu nafsi ya mtu roho ya mtu huyo itakuandama ili kulipiza kisasi? Unazungumziaje kisa cha kwenye bible pale Kaini alipo muua Habili, halafu roho ya kaini ikaanza kumlilia Mungu ikinu'ngunika kwa kudhulumiwa uhai wake? Unazungumzia vipi kisa cha kwenye bible pale Yesu alipotokewa na Mussa na Eliya ambao walikuwa wamekufa maelfu ya miaka iliyopita?. Na unadhani ni kwa nini stori kuhusu mizimu wanao watokea watu zinawahusu watu ambao wameuwawa?
   
 18. Access Denied

  Access Denied JF-Expert Member

  #18
  Jul 22, 2013
  Joined: Aug 10, 2012
  Messages: 640
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  Mimi ngoja niwahi kwenye hiyo blog maana nina mengi ya kujua kuhusu hili jambo kabla hata ya kuuliza swali.
   
 19. Access Denied

  Access Denied JF-Expert Member

  #19
  Jul 22, 2013
  Joined: Aug 10, 2012
  Messages: 640
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  Mimi ngoja niwahi kwenye hiyo blog maana nina mengi ya kujua kuhusu hili jambo kabla hata ya kuuliza swali.
   
 20. m

  mwalimu tajiri Member

  #20
  Aug 3, 2013
  Joined: Jul 21, 2013
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mapepo ni nini? Ni mali ya shetani anbaye ni mtawala wao, yesu anasema ibilisi na malaika zake, ni malaika walioanguka au kuasi.
  'na malaika wasio ilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu. Yuda 1;6"
  mapepo wawapo katika mwili wa mtu wanaweza kumfanyia vituko mbalimbali kama vile
  1. Kuku vunjia ndoa
  2. Kukufungia kipato chako
  3.wanaweza kukufungia ufahamu ukiwa darasani,nyumbani nk.
  Muzimu ni aina ya mapepo yatumiayo sura au kivuli cha mtu fulani mashuhuri aliyekufa ndani ya ukoo husika ndio maana baada ya yeye kufa huanza kujitafutia mtu mwingine ndani ya ukoo huo atakaye umiliki. Nao waweza kuja kwa mtu kwa njia ya uvamizi wa ndoto au sura ya mtu furani aliyekufa ndani ya ukoo.
  Kwa maana nyingine niseme kwamba ndani ya ukoo wako yuko mtu aliyefunga mkataba na mizimu akafungamanishwa na roho hiyo kwa agano la kutambika au kupeana zawadi fulani au kwa kufanyiana sherehe fulani kwa bahati mbaya mtu yule amefariki nndani ya ukoo huo lakini kumbuka ameacha amefunga mikataba na mizimu ndani ya ukoo huo hivyo ule mzimu unaanza kutembea ndani ya ukoo ukijitafutia mtu wa kulinyuu upya mkataba.
  "kutoka 20;5..........nawapatiliza wana maovu ya baba zao hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao;
  kumbe kwa kuwa babu yako aliingia katika maagano na mizimu, roho hiyo imefungamanishwa na ukoo huo....................
  MUNGU AKUBARIKI KWA SWALI LAKO ZURI...........
   
Loading...