Nini Tofauti kati ya Mazishi na Maziko??

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,145
13,216
Naona haya maneno yanatumika ndivyo sivyo, wataalamu tujuzeni kinagaubaga........
 
Mwali hii Avatar yako kama uko kwenye sanda tayari..afu nahisi u mwanaume????
poa tu, siwezi kukuziwia kuona au kuhisi hivo, nami niko huru kupendekeza jinsia niitakayo, na avatar niitakayo, sio?. lol
 
Mi nadhani mazishi ni maandalizi (mpaka wakati wakufika makaburini) ya kumzika marehemu.
Maziko ni kitendo cha kuanza kuweka mwili makaburini.

Sio kudhani kaka, ndio jibu lake. Nafarijika kuona kuna watu bado wanafahamu kiswahili kwa ufasaha wake, safi sana.
 
Mi nadhani mazishi ni maandalizi (mpaka wakati wakufika makaburini) ya kumzika marehemu.
Maziko ni kitendo cha kuanza kuweka mwili makaburini.
Malizia na ufafanuzi wa
Msiba
kilioni
Matanga

Na je mtu ana kufa au anafariki
 
Malizia na ufafanuzi wa
Msiba
kilioni
Matanga

Na je mtu ana kufa au anafariki

Msiba ni kuelezea shuguli ya mfu.
Kilioni ni sehemu watu wanapo lia.
Matanga ni shuguli baada ya kutoka makaburini.
Kufa na kufariki naona ni maana moja.
 
Ni namna ya kujenga seentensi na utamu wa lugha.

"Nnakwenda mazikoni" makes more sense kuliko "nnakwenda mazishini".

Tulikuwa kwenye mazishi ya..." makes more sense kuliko "tulikuwa kwenye maziko ya..."

Utamu wa lugha.
 
nilijua lazima ufike hapa, habari yako lakini!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom