Ngoja nijikumbushe A Level Physics kidogo...
Mkuu ni hivi kwa utangulizi, Bomu la Atomiki ni moja ya aina ya bomu la Nyuklia.
Kuna aina kuu mbili za Mabomu ya Nyuklia na utofauti huo utofautina kutegemeana ni aina gani ya 'chemical reaction' inayotokea.
1. Aina ya kwanza ni mabomu ya Nyuklia ambayo hutegemea 'Nuclear Fission/atomic fission' na hapa ndio tunapata Bomu la Atomiki 'Atomic bomb'.(Atomic fission inamaanisha kujaribu kuigawanya atomu).
Nishati itokanayo na utengano wa atomu ya elementi kama Uranium au Plutonium ndiyo hutengeneza mlipuko. (Asilimia kubwa ya Atomic bombs hutengenezwa na elementi hizo mbili)
Kwa lugha nyepesi unapotaka kuvunja aina yoyote ya 'chemical bond', huwa kuna mbadiliko wa ghafla wa kinishati ambao hupelekea 'energy emission' ambayo yaweza kuwa ni nishati ya mwanga, sauti au joto.
2. Aina ya pili ya bomu la Kinyuklia hutengenezwa kwa kutumia 'chain reaction' iitwayo 'Nuclear fusion' au 'Atomic Fusion'. Mfano wa aina hii ya bomu ni ile itengenezwayo kwa Haidrojeni na hujulikana kama Bomu la Haidrojeni 'Hydrogen bomb'.
Jua ni mfano mmojawapo unaotumia aina hii ya chain reaction na reaction hii huwa ni ya mfululizo, kwani kiasi cha joto kinachozalishwa hutumika kama kichocheo cha kuendeleza reaction.
Kwa kawaida Atomic fusion huwa inahitaji nishati joto kubwa sana, hivyo mabomu mengi ya haidrojeni huambatanishwa na bomu la atomiki ambalo hutumika kama trigger.
Hitimisho:
Kila bomu la atomiki ni bomu la kinyuklia, lakini sio kila bomu la kinyuklia ni bomu la atomiki.