Nini tatizo la Nape Nnauye?

Nini tatizo la Nape Nnauye?

Msafiri Kasian

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2011
Posts
2,134
Reaction score
664
Mi najiuliza, huyu Nape anashida gani na CHADEMA? Mara kwa mara nimekuwa nikimsikia akiizungumzia CHADEMA kwa mabaya.

Nimesikia kwenye magazeti leo asubuhi kuwa; eti CHADEMA isitafute mchawi anaeihangamiza, akidai kuwa tatizo lipo ndani ya chama. Kwani yeye ni msemaji wa matatizo ya CHADEMA?

Au hii ni mbinu ya kuihangamiza CHADEMA kisaikolojia?
Mtazamo wangu ni kwamba, huyu ndiye mchawi wa kwanza kwa sababu anaifuatilia sana CHADEMA na kutoa shutuma za uongo dhidi yake katika vyombo vya habari. Ajiweke karibu zaidi na chama chake cha CCM na kutatua matatzo kibao ya kabla ya kifo chao rasmi 2015.
 
Cha ajabu hapo ni nini? Kwani Dr Slaa au Mbowe wanaisema vipi CCM?? Hiyo ndio kazi yake, kama kiongozi wa chama kilichopinzani na Chadema!!
 
Huyu kijana ni mnafiki sana na uzeeni ataishia kua mchawi
 
Ndio kazi aliyotumwa na CCM kuiangamiza CDM ili waendelee kuifisadi nchi.
 
Tunaoujua udhaifu wa ccm na viongozi wake hatupati shida nao.Walilobakiza wao kwa sasa ni vita dhidi ya CHADEMA. kila kiongozi wao akipata nafasi ya kuongea maneno matano halitakosa neno CHADEMA, kinawanyima usingizi and now they are at war with it!
 
hata kama nikazi yake lakini aseme vitu vya ukweli siyo vya kutunga kama mwegulu mchemba
 
Wametumwa na mwenyekiti wao kwenda mikoani kujibu hoja baada ya kushindwa kujibu hoja.hoja walinayo kwa sasa ni kuota kifo cha chadema.
 
Hiyo ndio aina ya "demokrasia" ambayo nchi yetu imeamua kuifuata...
Kusimangana baina ya chama na chama, kiongozi na kiongozi wao ndio huona wamefanya jambo la maana...
Wote huo ni usanii tu!!!
 
Huo ndio unafiki wa viongozi wa Kitanzania hasa CCM
 
Aliisha kunywa cdm hivyo si rahisi kuongea bila kuitaja ila ipo siku atahamia cdm
 
Huyu mpk sasa hivi lazima atakuwa mchawi tuu
 
Nilimuuona kwa macho kwenye kipindi cha mikasi cha salama jabir akiidis chadema,
tena nasema haki ya nani nape ngoja chama chako kife uone utakavyoumbuka.
 
Wenye akili na tuanoweza kusoma between the lines huwa tunapata majibu kutoka kwa viongozi wanaobwbwaja kama nape na mwigulu. Mpaka sasa tumegundua haya:
1. Maalim Seif alihongwa na kuhadaiwa kujiunga na serikali ya umoja wa kitaifa. Huku akiwa na akili timamu anawahadaa wana CUF na wanzanzibar kwamba yeye ni upinzani kumbe sivyo -Shahidi Jerry Slaa[
2. Mwalimu Nyerere alikilaani CHADEMA kwa ukabila lakini(through deconstructionist theory) akaibariki CCM kwa ufisadi, wizi, udini, uongozi wa kikaya, ubinafsishaji usiokuwa na tija wa raslimali za watanzania, mauaji ya raia wasiokuwa na hatia, wizi wa tembo, twiga, uuzaji wa ndege 3 kwa sh. milioni moja na nusu na hivyo mwalimu ni muasisi wa mambo yote yanayofanywa na CCM ndio mana kila mara wanaimba kumuenzi mwalimu- Shahidi ni Nape Moses Nnauye.
Waendelee kubwwbwaja sisi tunaendelea kujenga ushahidi turudi kwa wananchi kuwaambia ukweli. Kuna na wengine walianza kusema watu fulani si wa ukoo fulani ilimradi tu kuijhalalishia nafasi ya kuendelea kuwaibia watanzania. Muda utaamua....QUOTE=Msafiri Kasian;5502970]Mi najiuliza, huyu Nape anashida gani na CHADEMA? Mara kwa mara nimekuwa nikimsikia akiizungumzia CHADEMA kwa mabaya.

Nimesikia kwenye magazeti leo asubuhi kuwa; eti CHADEMA isitafute mchawi anaeihangamiza, akidai kuwa tatizo lipo ndani ya chama. Kwani yeye ni msemaji wa matatizo ya CHADEMA?

Au hii ni mbinu ya kuihangamiza CHADEMA kisaikolojia?
Mtazamo wangu ni kwamba, huyu ndiye mchawi wa kwanza kwa sababu anaifuatilia sana CHADEMA na kutoa shutuma za uongo dhidi yake katika vyombo vya habari. Ajiweke karibu zaidi na chama chake cha CCM na kutatua matatzo kibao ya kabla ya kifo chao rasmi 2015.[/QUOTE]
 
Nape ni katibu mwenezi wa CCM. Kazi yake mojawapo ni kuieneza CCM kadri ya uwezo wake, hii inajumuisha kuipamba CCM kwa wananchi na kuviponda vyama vya upinzani especially CHADEMA kwa sababu CHADEMA kwa sasa ndio tishio kwa ccm. Yeye anatimiza wajibu aliopewa na CCM.
 
Mi najiuliza, huyu Nape anashida gani na CHADEMA? Mara kwa mara nimekuwa nikimsikia akiizungumzia CHADEMA kwa mabaya.

Nimesikia kwenye magazeti leo asubuhi kuwa; eti CHADEMA isitafute mchawi anaeihangamiza, akidai kuwa tatizo lipo ndani ya chama. Kwani yeye ni msemaji wa matatizo ya CHADEMA?

Au hii ni mbinu ya kuihangamiza CHADEMA kisaikolojia?
Mtazamo wangu ni kwamba, huyu ndiye mchawi wa kwanza kwa sababu anaifuatilia sana CHADEMA na kutoa shutuma za uongo dhidi yake katika vyombo vya habari. Ajiweke karibu zaidi na chama chake cha CCM na kutatua matatzo kibao ya kabla ya kifo chao rasmi 2015.
NAPE: UBAGUZI UNAWAMALIZA CHADEMASunday, January 20, 2013

[h=3]*Asema kwa dhambi hiyo hakuna dawa lazima Chadema kife.
*Adai ni laana ya Mwalimu wasimtafute mchawi nje.
*Awaasa waandae mazishi mapema.[/h]

[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Nape akizungumza Nyamagana leo[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
MWANZA, Tanzania
KATIBU wa wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amewataka Chadema wamsitafute nje mchawi anayewamaliza kwa kuwa ubaguzi ulioota mizizi kwa muda mrefu ndani ya chama hicho ndio sumu inayowaua.

Alisema kwa kukumbatia ubaguzi aliodai kulelewa na waasisi na viongozi wa kitaifa ndani ya Chadema, sasa iliyobaki waandae mapema, mazishi ya chama hicho kwa kuwa hakuna jinsi ambavyo kitanusurika kufa kutokana na dhmabi hiyo mbayo hata Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliikemea akisema ni mbaya sawa na kula nyama ya mtu.

Nape aliyasema hayo leo Januari 20, 2013, jijini Mwanza kwenye mkutano wa hadhara wa Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula na baadhi ya mawaziri, uliohudhuriwa na maelfu ya wanachi wa jiji hilo na vitongoji vyake kwenye Uwanja wa mpira wa Nyamagana.

Nape alisema anashangazwa na viongozi wa Chadema kuendelea kunyooshea vidole CCM kuwa eti inahusika na mtafaruku na umahututi wa chama chao wakati CCM walishajitahidi kuwataadharisha mapema kuwa ubaguzi wanaoukumbatia, licha ya kuathiri umoja na mshikamano ni dhambi ambayo itakisambaratisha chama hicho.

"Hamuwezi kuwa na chama ambacho ili kiongozi wake adumu na kuheshimika lazima awe anatoka ukanda fulani au ukoo fulani ndio adumu, vinginevyo anasukiwa mizengwe na mwisho kutimuliwa" alisema Nape na kuongeza "walianza na kina Chacha Wangwe na Watanzania wote wanajua leo kilichompata Chacha Wangwe, sasa wameanza kumwandama Zitto na wanaoitwa vijana wake, na pia nasikia wamejipanga kumfukuza Shibuda wiki ijayo."

"Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alishasema dhambi ya ubaguzi ni kubwa, na ni sawa na kula nyama ya mtu, ambapo mtu akishaila anazoea kiasi kwamba haachi, basi nao Chadema hawana namna ya kuachana na ubaguzi unaoendelea ndani ya chama chao, hivyo watasambaratika kwa laana hiyo ya Mwalimu", alisema Nape.

Nape alilionya kwamba, ikiwa Chadema wanabaguana kiasi hicho ndani ya alichokiita kichama kidogo, kama hicho watafanyaje wakipewa dhamana ya kutawala nchi. " Ikiwa wanabaguana ndani ya kichama kidogo kiasi hichi ambacho hakijai hata mkononi, watafanyaje wakipewa dhamana ya kuongoza hata kipande cha nchi yetu?" alihoji.

Nape alidai kuwa ubaguzi ndani ya Chadema umejikita kwenye ukanda, ukabila na hata udini na kwamba ubaguzi huo unajionyesha zaidi kwenye safu ya uongozi wa chama hicho na maeneo mengine. "Sasa leo nimeamua kuwapa ushauri wa bure kabisa Chadema wasiendelee kutafuta mchawi nje ya chama chao", alisema.

Mkutano huo ambao umehusisha wananchi kutoka Wilaya za Ilelema na Nyamagana, ni moja ya mikutano ya Mangula ambayo amekuwa akiifanya tangu aanze ziara ya kwanza katika mkoa wa Mwanza ambapo tayari ameshapita katika wilaya za Magu, Ukerewe na Sengerema
 
Mimi huyu jamaa simwelewi, akiwa anaongea yacyohusu siasa yupo smart sana na makini lakini likija suala la siasa anageuka frm hero 2 zero na kuongea kama amekatwa kichwa, huwa cjui ccm huwa inaharibu ubongo au kuna siri gani mi cjui
 
If people are trying to pull you down....Be proud about it, because it only confirms that you are above them. Chadema wanapaswa wajue wako juu sana
 
Mi najiuliza, huyu Nape anashida gani na CHADEMA? Mara kwa mara nimekuwa nikimsikia akiizungumzia CHADEMA kwa mabaya.

Nimesikia kwenye magazeti leo asubuhi kuwa; eti CHADEMA isitafute mchawi anaeihangamiza, akidai kuwa tatizo lipo ndani ya chama. Kwani yeye ni msemaji wa matatizo ya CHADEMA?

Au hii ni mbinu ya kuihangamiza CHADEMA kisaikolojia?
Mtazamo wangu ni kwamba, huyu ndiye mchawi wa kwanza kwa sababu anaifuatilia sana CHADEMA na kutoa shutuma za uongo dhidi yake katika vyombo vya habari. Ajiweke karibu zaidi na chama chake cha CCM na kutatua matatzo kibao ya kabla ya kifo chao rasmi 2015.
Nahisi una vichwa cha panzi wewe..! Yaani ulitegemea Nape aisifie cdm?
 
Actually Nape is suffering from Uropokajiosis which is the results of Umbumbuostomy and may end into uchawiology. The only prognosis of this syndrome in Tanzania is to apply Chademaquine.
 
CCM iandae nishani ya kumwenzi huyu jamaa maana anavuma kana kwamba hakuna wanachama wala viongozi wengine wa chama. Hongera unafanya kazi nzuri lakini je matatizo ya wananchi na utendaji mbovu wa serikali yako hatujakusikia ukisema au hiyo siyo kazi yako?
 
Back
Top Bottom