Nini tafsiri ya HALOOWEEN kwa Kiswahili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini tafsiri ya HALOOWEEN kwa Kiswahili?

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Serendipity, Oct 31, 2009.

 1. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Habari za leo wanjf,Leo ni sikukuu ya HALOOWEEN, naomba kufahamishwa tafsiri halisi ya neno HALOOWEEN kwa kiswahili, au maana yake kwa kiswahili tunaweza kufananisha na sherehe za mila ghani za kijadi kwa jamii yetu ya kitanzania?
   
 2. Suki

  Suki JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 373
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  We probably don't have a word for it.
  Ila kwa hali ya sasa ya Bongo,everyday is halloween.
   
 3. Yegomasika

  Yegomasika JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2009
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 7,125
  Likes Received: 23,734
  Trophy Points: 280
  Damn, yaani bongo kila siku ni Halooween-ama kweli kazi tunayo!.
   
 4. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2009
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,168
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Jamani sasa mbona 2najidhalilisha! Navojua mi halloween day wazungu wanaisherehekea kwa kuvaa manguo na ma-mask usoni ya kutisha. Nguo zengine wavaazo ni zile za zamanii. Mfano surual kama zile za juu imebana chini imeachia plus ndevu za bandia. Ili mradi utishe au uonekane wa kale. Wengine wanasema hii inasaidia kuwatisha evils, though sina ushahidi hapa.
  Sasa unaposema bongo halloween kila siku, huku ni kuwa-insult wabongo!
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Huku mikoani hakuna hiyo kitu, na mi ndo naisikia leo... Sa ulimbukeni wa kibongo utakuta watu wanapiga suti kali za kifisadi wanaenda kwenye hiyo mambo, wakati kwa wenzao waanzilishi ni mambo ya kimila...lol!
   
 6. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Huku kwetu halooween haina maana yoyote,bwana mudogo, na ni sikukuu ya kipagani na wengine waaminio mila hizo za wapagani wa kizungu.
  Wewe tazama tu na iga lililo jema kwako.
   
 7. Domenia

  Domenia JF-Expert Member

  #7
  Oct 31, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kweli...angalia avata yangu...ni haloween kama vipi....
   
 8. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #8
  Oct 31, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  Mambo kama haya ndo HALOOWEEN
   
 9. Suki

  Suki JF-Expert Member

  #9
  Oct 31, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 373
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wasn't trying to.
  And still,the Socio-political atmosphere and most of what goes down,is a perfect reincarnation of my childhood Halloween experience.All spooky and gory,without the candies of course!
   
 10. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #10
  Oct 31, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,537
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Haina maana kutafsiri "halloween" kwa sababu ni jina maalum.

  Mfano:
  George Bush ni George Bush au unapenda kumwita "Mkulima Pori"? Hii ingekuwa tafsiri yake kwa sababu
  a) "George" ni jina kutokana na neno la Kigiriki γεωργός = mkulima na
  b) bush ni ama jina la aina ya eneo linaloitwa "pori" kwa Kiswahili (deep in the bush) au jina la miti midogo = kichaka

  Kwa hiyo haina maana kutafsiri majina maalumu. Ila tu kile ambacho wanaJF wengine walieleza ni desturi ya Kimarekani iliyoanza kusambaa hata nje ya Marekani kutokana na filamu za kule zinazoanagliwa kote.

  Siku yenyewe ya Haloween kiasili ni sikukuu ya kikatoliki ya "watakatifu wote" tarehe 1 Novemba ambako marehemu wanakumbukwa.
  Eire walikuwa na desturi ya misa kwenye jioni kabla ya tar. 1. Novemba ("All Hallows' Eve" = evening before All Hallows = All Saints' Day -saint=hallow) na katika lahaja ya Eire ile "All Hallows' Eve" imekuwa "Halloween".

  Ila tu desturi za kuvaa nguo za ajabu pamoja na vinyago si ya kale sana imejitokeza na kusambaa miaka ya nyuma tu.
   
 11. m

  mafanikio Member

  #11
  Nov 1, 2009
  Joined: Jul 23, 2009
  Messages: 51
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 15
  Domenia na Tripo9 walau mmeweza kuonesha maana ya haloween japo bado inahitaji nyongeza ili kueleweka kinagaubaga, ila kwa ushauri wangu kwa muuliza swali yuko sahihi kwakuwa anapenda kufahamu, tatizo langu ni kwa wale wenzangu na mie ambao hawapendi kupitwa na mambo kama hawajui au wanajua wao ni kukurupuka na kutoa maana zinazopotosha na hata kudhalilisha yaani imeniuma sana mtu kusema bongo ni haloween kila siku?
  natamani ningekuwa na uwezo nimpeleke akaone tukio husika alafu arudi na kubatilisha maandishi yake, ila kwa kifupi kwa ambao tuko huku leo mitaani hasa mida ya jioni mpaka usiku huu baadhi ya watu mitaani wamevaa vitu vya kutisha usoni, minguo ya ajabu ajabu yaani ilimradi wao wameadhimisha tukio husika, ila ukifuatilia kwa makini kuna programu ilikuwa ikionyeshwa live mimi kama mimi kwa maoni yangu ni upuuzi tena inadhalilisha wahusika waliokuwa wakishiriki tukio husika.
   
 12. Suki

  Suki JF-Expert Member

  #12
  Nov 1, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 373
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  This is painful!
  You always this shallow?I mean,don't get me wrong,I just can't believe you still miss the point here.

  FYI,Wande ameuliza neno la kiswahili la halloween na si vinginevyo.He might have mentioned needing to know it's meaning in swahili and if at all associated with any traditional ceremonies.

  That aside,the simple answer is NO,we do not have a swahili word for it nor do we associate the event with any traditional ceremonies,at least not in the tribes I am familiar with.

  My comparing halloween with the situation in Tanzania is a whole different issue altogether (kinda brought up by the thought of halloween in a Tanzanian context).I wouldn't go sleepless over this though,it's either you get the point or you don't and by the look of things,you my friend are leaning towards the latter.
   
 13. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #13
  Nov 1, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo wakristo wameiga sikukuu ya kipagani na kuifanya yao?
   
 14. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #14
  Nov 2, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,537
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Sielewi swali lako.
  Katika nukuu yangu hakuna neno kuhusu desturi za kipagani. Kinyume chake nimeeleza ya kwamba jioni ya tar. 1. Novemba kuna uhusiano na sikukuu ya kikatoliki ya "Watakatifu wote" (All Saints).

  Hali halisi ni kinyume cha kile unapolenga. Halloween ni mfano mzuri wa desturi mpya isiyo ya kikristo lakini ilijengwa juu ya msingi wa sikukuu ya kale ya kikristo (kikatoliki) katika nusu ya pili ya karne ya 20.
   
 15. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #15
  Nov 2, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Tumekuelewa mkuu...!kuwa...
   
 16. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #16
  Nov 2, 2009
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,989
  Likes Received: 3,737
  Trophy Points: 280
  This is from wikipedia. self-explanatory........

  Halloween

  From Wikipedia, the free encyclopedia


  Halloween (also spelled Hallowe'en) is an annual [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Holiday"]holiday[/ame] celebrated on [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/October_31"]October 31[/ame]. It has roots in the [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Celts"]Celtic[/ame] festival of [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Samhain"]Samhain[/ame] and the [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Christian"]Christian[/ame] holy day of [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/All_Saints"]All Saints[/ame], but is today largely a [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Secularity"]secular[/ame] celebration.
  Halloween activities include trick-or-treating, wearing [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Halloween_costume"]costumes[/ame] and attending [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Costume_party"]costume parties[/ame], carving jack-o'-lanterns, [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Ghost"]ghost tours[/ame], [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Bonfire"]bonfires[/ame], visiting [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Haunted_attraction"]haunted attractions[/ame], pranks, telling scary stories, and watching [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Horror_film"]horror films[/ame]
  Halloween costumes are traditionally those of monsters such as ghosts, skeletons, witches, and devils. They are said to be used to scare off demons. Costumes are also based on themes other than traditional horror, such as those of characters from television shows, movies, and other pop culture icons.
  ==================================================

  Mpo hapo? Au not reachable??
   
 17. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #17
  Nov 2, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Watanzania kwa kuvamia mambo ya USA basi nao eti nikasikia kuna Halloween Party hapa Dar!.................Yaani siku USA wakianzisha sikukuu ya kutembea uchi nahisi wabongo ndio watakuwa wa kwanza kuiga!

  Hovyo kabisa !!!
   
 18. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #18
  Nov 2, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,537
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Usishangae, kaka! Si tatizo la TZ pekee; hata Ulaya au penginepo mambo yale kutoka Marekani yamesambaa. Naona ni ule utandawazi (globalization) kupitia filamu na intaneti. Hadi sasa athira kubwa ndani yake ilikuwa Marekani (Coca, muziki, vyakula vya haraka...) lakini mengine yameshaanza yataendelea kutoka sehemu nyingine pia.

  Sipendi Halloween lakini ni bure kusikitika maana vijana wakiichagua basi ni kusubiri wakue.

  Ila kuwacheka - tucheke!
   
Loading...