joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,613
Kwanza niwapongeze wote ambao tumechangia na tunaendelea kuchangia mijadala inayolinganisha bandari ya Mombasa na ile ya Dar, na mjadala kuhusu TRA na KRA.
Katika mijadala yote hii ninawapongeza watanzania kwani wengi wao wamekubali kwamba Kenya inafanya vizuri katika hayo maeneo mawili kuizidi Tanzania, huo ndio uungwana kwa mtu yeyote mwenye busara hapaswi kukubaliana na ukweli japo huo ukweli unamshusha chini, kwa kufanya hivyo ndio mwanzo wa kujifunza kwa aliyefanya vizuri.
Kwa mantiki hiyo hiyo, ningependa tujadili siri ya Tanzania iliyoifanya Tanzania kuwa gumzo dunia nzima na kuwa nchi ya kwanza dunia kuruhusu shughuli zote za maisha kurejea bila kupatwa na athari za Corona kama ilivyotokea katika nchi nyingi duniani ikiwemo Kenya.
Ni ukweli kwamba Tanzania imeshinda au inakaribia kushinda Vita dhidi ya Corona, dunia imeanza kukubali ikiwemo Kenya ambayo kwa muda mrefu sana imekua ikipinga, kitendo cha Kenya kuiweka Tanzania katika kundi la nchi salama ni ushahidi ulio wazi.
Lakini pia ni ukweli kwamba watu wengi duniani wakiwemo watanzania wengi, na wakenya bado hawaelewi hasa kitu gani kilisababisha Tanzania kushinda hii vita, na Corona kudhibitiwa haraka kuliko nchi yoyote ile duniani. Kenya bado inaendelea kusumbuliwa na Corona kiasi cha kuogopa hata kufungua shule na vyuo vya Elimu, wakati kwa upande wa Tanzania, sasa ni takriban miezi 4 tangu shule zote kufunguliwa lakini hakuna taarifa wala dalili za kuwepo kwa maambukizi mashuleni.
Lengo la uzi huu ni kujifunza yale mazuri yalitofanywa na Tanzania kama yapo, na wapi Kenya inapokosea ili Kenya iweze kujirekebisha.
Maswali chachushi:
1) Nini kilichofanywa na Tanzania kilichosababisha kuishinda Corona?
2) Kenya inakosea wapi?
Sent from my TECNO-L8 using JamiiForums mobile app