Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,997
Nini Sababu za Mbowe na Lowassa kukwepa kongamano kumbukumbu ya Mwl.Nyerere?
Haijawahi kutokea kwenu ninyi kuonekana mkishiriki makongamano na midahalo ya wazi yenye kuzungumzia masuala ya utaifa na nchi kwa ujumla. Mara kwa mara Taasisi ya Mwalimu Nyerere imekuwa ikiandaa mada na hoja zenye kubeba changamoto za utaifa hususani maadili,miiko ya uongozi na vita dhidi ya rushwa. Mara kadhaa vingozi wastaafu kama Jaji Warioba, Dr.Salim, Mzee Butiku nk. Wamekuwa wazungumzaji wakubwa kwenye mada hizo.
Mbowe kama KUB amekuwa kimya kuhusu mapambano dhidi ya rushwa, Lowassa kwa upande wake hata kwenye kampeni za uraisi mwaka jana hakuwahi kuongelea mikakati yake kudhibiti maadili ya uongozi na vita dhidi ya rushwa. Kinachoshangaza ni kuwa duniani kote vinara wa upinzani ndio huibana serikali na viongozi wa umma kuhusu masuala ya rushwa ila hapa kwetu angalau chama cha ACT-Wazalendo kwa siku za karibuni wameonyesha njia.
Ninaomba tujadili haya kwa mapana kwani hawa ni viongozi wetu, kama watakwepa kuzungumza na kukemea matatizo ya nchi yetu kupitia makongamano kama hili ya Mwl.Nyerere inatia shaka
Je ni kweli hawana cha kuzungumza jinsi gani Taifa letu linaweza kupiga hatua kwa kupiga vita rushwa na kzingatia maadili ya viongozi wa umma?
Je nao ni miongozi mwa tatizo katika jamii yetu hususan katika vita dhidi ya maadili mabovu,rushwa na ubadhirifu wa mali za umma?