beevenom
JF-Expert Member
- May 1, 2017
- 313
- 428
Aman iwe nanyi ndugu zangu,napenda kushare jambo langu binafsi katika maisha yangu ya kila siku. Sijajua ni tatizo au ni nini kwani tangu nikiwa bado mdogo kabisa(nikiwa shule ya msingi) sijawahi kuwa na rafiki kabisa mpaka umri huu wa thirties.
Lakini pia katika kupindi chote cha makuzi yangu nimekuwa ninaongea na kila mtu kwa sababu maalam yaani baada ya lengo langu kutimia hujikuta sitamani kuendelea kuongea na mhusika kabisa.
Pia kuna wakati huwa sijisikii kabisa kuongea na awaye yeyote labda kuchart kwa SMS tu.
Pia nina changamoto ya kutoamini MTU yoyote yule hivyo nikimkabidhi mtu kazi hujikuta nafuatilia kwa ukaribu haswaa kama vile na mie ninafanya kazi husika. Na mara nyingi nikijaribu kumuamini mtu tu lazima atazingua tu iwe kazi au mapenzi.
Sasa inafika wakati jamii inaniona nina dharau au jeuri kumbe sio kabisa kwani kuna wakati nikisalimia mtu huwa sijisikii kabisaa kuongea nae.
Jamani nisaidieni kuhusu hii hali maana kuna wakati hujikuta mpweke.
Sent using Jamii Forums mobile app