Nini NHC??

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,578
8,600
Hivi watanzania tumelalaa??au niustarabu??ulishawahi kuwa nashahuku yakupanga NHC??Je ulijiuliza swali gani??nadhani ulikata tamaa kwa jinsi ambavyo ungelianza ukaona nindoto za mchana kwakuwa uliona nikitu kisichowezekana kwa mtanzania mwenye ngozi nyeusi, Kwa taarifa yako wahindi akitoka leo India anapata kwa nini sisi watanzania!!??
Nini tatizo??Je wahindi ndio walengwa kwa NHC??Je viongozi wa NHC hawana uchungu na watanzania wenzao??
Je tuandamane kuwakurupua huko katika mjengo??wakati walengwa tunaumizwa nakodi za sh.50.000 kwa kachumba kwa mwezi wahindi wenye pesa wanatanua kwa sh.20.000 vyumba viwili choo bafu jiko sebule je serikali hipo kwa ajiri ya watanzania??je waziri kazi yake nini??je kwa hali hiyo utairudisha madarakani??:painkiller:
 
NHC wenyewe nao sio wabunifu nyumba zile zile tu wakati idadi ya watanzania inaongezeka inabidi wajenge nyumba mpya sasa ili watanzania wengi waweze kufaidika.
 
Jamani hilo sio swala, tatizo huko NHC mmemuweka mtu ambaye hana uwezo wa kuleta mabadiliko yoyote, nadhani ilijadiliwa hapa JF kwamba huyo mkuu alilazimishiwa wakati hata interview hakufaya kwa vile hakuwa na vigezo, vigezo vikashushwa kwa shinikizo la chief secretary, kabila lake ili apate, sasa leo hii anachakachua hujaona, kaanza kujaza marafiki zake, mtu wa QS anapewa nafasi ya planning,katishia kuwafukuza watu wote aliyowakuta na waziri badala ya kum manage anachofanya ni kumlamba miguu, nafasi ya u director fulani amechakachua anampa mdogo wake karume wa Knight Frank, watu ambao hata swala lao la ku operate bara ni questionnable sababu maswala ya ardhi si sehemu ya muungano, hizo nyumba wamejifanya kufanya usaili wa kujua nani yuko wapi si kwa lengo za ku re allocate, bali kupeana wao na mtandao wao, ndio malipo kwa waliompa kazi asiyo na uwezo nayo. Sasa subirini makubwa zaidi mkome. Nendeni barabarani mkadai nyumba zenu ama shauri yenu kipindi kinachokuja mkiwapa hata huko bunju mtahamishwa muende kuishi msata na kufanyakazi Dar
 
Nyumba nyingi za NHC zilikuwa za wahimndi kabla ya kutaifishwa bila fidia 1967...wana uchungu nazo

Sahihisho kidogo, zilitaifishwa 1971 chini ya sheria ya Acquisition of Buildings Act. Ni kweli nyingi zilikuwa za wahindi kwanni sheria ililenga wamiliki ambao walikuwa hawaishi nchini (abstentee landlordism)

Mpeni Bwana Mdogo muda, nadhani ataweza - ile ni biashara, yeye ni CEO na CEO anapaswa kwa maono yangu awe ni mtu mwenye taaluma isiyoshabihiana na wale watendaji wengine. Unajua Injinia kwa Injinia wanavimbishiana maguvu, Architect humponda architect mwenzie, na the more specialised hawa watu ni kadiri hiyo wanavyopondana. Ukiweka juu yao kiunganishi basi inawezekana umefanya vizuri, ni mapema mno mwache bwana mdogo afanye kazi.

Kama amemchukua mwanae Karume yule wa Knight Frank sio vibaya, kale kabinti ukiacha makidai kama kina dada wengi waliokwisha kula kuku kwa mrija, hakajambo, kanajua kazi yake ni mwana-taaluma yule, usimhukumu kwa kuwa baba yake ni Karume au kwa kuwa katoka Zanzibar, angeweza pia kutoka Nigeria kama alivyokuwa yule Bw wa Tanroads kabla ya Mrema.
 
NHC ni shamba lingine la bibi. Kuna watu wako pale miaka nenda miaka rudi wanaendelea kujikamulia kadri wanavyoweza. Lakini ndivyo yalivyo karibu mashirika yote ya umma...nilikuwa najiuliza juzi nini kimetokea TPDC kwenye ile project ya CGN kwa ajiri ya magari, nikagundua kwamba ni shamba lingine la bibi linaandaliwa na wakamuaji wake wanajipanga kujineemesha na ukamuaji huo.
Tanzania Tanzania Tanzania
 
Hivi watanzania tumelalaa??au niustarabu??ulishawahi kuwa nashahuku yakupanga NHC??Je ulijiuliza swali gani??nadhani ulikata tamaa kwa jinsi ambavyo ungelianza ukaona nindoto za mchana kwakuwa uliona nikitu kisichowezekana kwa mtanzania mwenye ngozi nyeusi, Kwa taarifa yako wahindi akitoka leo India anapata kwa nini sisi watanzania!!??
Nini tatizo??Je wahindi ndio walengwa kwa NHC??Je viongozi wa NHC hawana uchungu na watanzania wenzao??
Je tuandamane kuwakurupua huko katika mjengo??wakati walengwa tunaumizwa nakodi za sh.50.000 kwa kachumba kwa mwezi wahindi wenye pesa wanatanua kwa sh.20.000 vyumba viwili choo bafu jiko sebule je serikali hipo kwa ajiri ya watanzania??je waziri kazi yake nini??je kwa hali hiyo utairudisha madarakani??:painkiller:

NHC waachane na hao wahindi, cha kufanya wajenge nyumba nyingine mpya na ambazo wazawa wanaweza kumudu bei zake, yanakaa tu huko sijui yanafanya nini, mnataka NSSF ndio wajenge kila kitu
 
Sahihisho kidogo, zilitaifishwa 1971 chini ya sheria ya Acquisition of Buildings Act. Ni kweli nyingi zilikuwa za wahindi kwanni sheria ililenga wamiliki ambao walikuwa hawaishi nchini (abstentee landlordism)

Mpeni Bwana Mdogo muda, nadhani ataweza - ile ni biashara, yeye ni CEO na CEO anapaswa kwa maono yangu awe ni mtu mwenye taaluma isiyoshabihiana na wale watendaji wengine. Unajua Injinia kwa Injinia wanavimbishiana maguvu, Architect humponda architect mwenzie, na the more specialised hawa watu ni kadiri hiyo wanavyopondana. Ukiweka juu yao kiunganishi basi inawezekana umefanya vizuri, ni mapema mno mwache bwana mdogo afanye kazi.

Kama amemchukua mwanae Karume yule wa Knight Frank sio vibaya, kale kabinti ukiacha makidai kama kina dada wengi waliokwisha kula kuku kwa mrija, hakajambo, kanajua kazi yake ni mwana-taaluma yule, usimhukumu kwa kuwa baba yake ni Karume au kwa kuwa katoka Zanzibar, angeweza pia kutoka Nigeria kama alivyokuwa yule Bw wa Tanroads kabla ya Mrema.

Bora wewe unajua tofauti ya haya maneno, Architect na Architecture! Inasemekana DG mpya w NHC yanampa kazi kweli haya maneno kuyatofautisha. Yeye anamwita msanifu majengo Architecture badala ya Archtect, basi si vicheko vya chini chini kwenye hizo management meeting zao.

Shirika liko mbioni kufa kama jitihada za makusudi hazitachukuliwa. DG anapandikiza washikaji zake bila kuangalia competency ya mtu ukiachia mbali kuzitangaza hizo posts mwezi mzima karibu kila gazeti (KIINI MACHO) na kuwapa consultants wafanyishe hizo interviews wakati kila kitu ni maelekezo yake. Uchakachuaji ni wa hali ya juu na wengi wanasubiri waone mustakabali wa shirika hili linaloonekana kuwa shamba la bibi.
 
Back
Top Bottom