Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,516
Mimi ni mkazi wa jiji la Dar es Salaam. Mahali ninapoishi, kwa siku hizi za karibuni ikiwemo jana, kumekuwepo na kukatika kwa umeme kuanzia asubuhi au mchana hadi usiku. Jana, umeme ulirudi, ukakatika na kurudi tena. Mgawo wa umeme ndani ya jiji la Dar es Salaam na sehemu nyinginezo za nchi limekuwa ni tatizo sugu.
Mawaziri wanaingia na kutoka lakini mgawo uko pale pale. Nilizipongeza na naendelea kuzipongeza juhudi za Serikali ya Rais Magufuli katika kuimarisha huduma ya umeme nchini. Moja ya juhudi kubwa ni kutenganisha iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini kupata Wizara ya Madini na Wizara ya Nishati ambayo ndiyo inayosimamia umeme.
Nilifarijika niliposoma:Serikali: Tatizo la umeme mwisho Desemba 15. Tarehe 15 iliyotajwa imepita na mgawo unaendelea. Nawakaribisha hata TANESCO tutafakari pamoja swali hili: nini na nani hasa ni chanzo cha mgawo wa umeme usiokwisha? Nini kinafanyika kumaliza kadhia hii?