Nini Mkakati wa Rais Magufuli dhidi ya CAG?

Hapo kwenye nini kilifuata nikujuze tu kuwa mahakama ya wananchi iliazimia kuwa muda utaongea.. Hatukubali dhulma hizi ziendelee tena.

Jimama26, naweka ujumbe wako huu kwenye kumbukumbu zangu mhimu.

Ila nina shaka, ulipoweka maneno "muda utaongea". Mtu anapotumia maneno haya, mara nyingi huwa ana maana ya kinyume cha yale aliyoyasema mwanzo!
 
Heee, naona mimi hili lilinipita pembeni. Sikujua kuwa 'wananchi' walikwisha bainisha hilvyo. Enhee, hibu eleza zaidi, baada ya 'mahakama ya wananchi' kubainisha hivyo,Kama kweli usemavyo ni sahihi ni nini kilifuatia baada ya hapo?

Mi naona hukuelewa nilichoelezea katika bandiko uliloni'quote' hapo juu.
Mahakama ya wananchi ikishaamua ndiyo hivyo tena inabakia hivyo. shida inakuja pale maamuzi ya aina hii yanafuatana, wananchi wanajenga kutokuwa na imani na serikali yao. inapokuja uchaguzi, mtu anayeishambulia serikali wala hapati wakati mgumu
 
Maneno yako haya ni matamu kuyasoma; ila ni machungu wakati mtu akifikiria uhalisi wake.
Natambua ni mjadala mgumu, kueleza 'disconnection' iliyopo kati ya umma 'kutambua" na umma "kuhukumu". Ushahidi upo wazi kila mahali unaoonyesha 'hukumu' haitolewi ipasavyo.
Pengine hili ndilo linalotutofautisha kwenye mada hii. Mimi ningependa hukumu ya wananchi wakiitoa ifanye kazi kweli kweli. Lakini hapo hapo natambua kutokuwepo kwa uwezekano huo na ndio maana yangu ya kuwasihi vyama vya upinzani walichambue vizuri hili ili hao watoa hukumu waone hukumu zao zikifanya kazi bila 'exception'.
 
Wanazidi kumtikisa ili ajiuzulu wapate kumweka kikaragosi chao kitakacho toa report za uongo. Kushabikia uongozi huu uwe na roho ngumu [emoji23][emoji23]
Mimi nasema Prof. hapo ni kukomaa tu hakuna kujiuzuru wala nini maana hao watu wanatumia mbinu hizo ili komdhoofisha hadi ajiuzuru mwenyewe ukitaka kujua hilo kama kweli rais huwa anajinasibu ni mtu wa haki na sisi wananchi tunajua CAG anasimamia haki na ni mteule wa rais kwanini asiseme jambo mpaka sasa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Kujiuzuru" CAG?

Hapana. Hiyo itakuwa ni kuwapa heshima wasiyostahili.

Njia nzuri ni kwake kufanya kazi yake bila ya kutetereka. Acha wahangaike na kutafuta njia zisizo halali kumwondoa ili wajipake matope wenyewe.

Rafiki yangu mmoja aliyekuwa akifanya kazi kwenye taasisi ya kimataifa alitengenezewa zengwe na watumishi wenzake Watanzania waliomuona mkali na hataki ubabaishaji wa Kitanzania. Baadhi ya watumishi walioshindwa kuhimili na waliamua kuacha kazi. Kabla ya kufanya hivyo walimtuhumu bosi kwa unyanyasaji wa kijinsia wakijua kwa shutuma hizi huyo bosi naye hatapona. Kweli hakupona. Alitakiwa naye aache kazi lakini alikataa katakata na kutaka mwajiri amfukuze kazi! Kwa shirika la kimataifa lenye maadili ilishindikana kumfukuza kazi na badala yake ilibidi kumuomba na kumpa package nzito. Bado alikataa hiyo package!
 
Maneno yako haya ni matamu kuyasoma; ila ni machungu wakati mtu akifikiria uhalisi wake.
Natambua ni mjadala mgumu, kueleza 'disconnection' iliyopo kati ya umma 'kutambua" na umma "kuhukumu". Ushahidi upo wazi kila mahali unaoonyesha 'hukumu' haitolewi ipasavyo.
Pengine hili ndilo linalotutofautisha kwenye mada hii. Mimi ningependa hukumu ya wananchi wakiitoa ifanye kazi kweli kweli. Lakini hapo hapo natambua kutokuwepo kwa uwezekano huo na ndio maana yangu ya kuwasihi vyama vya upinzani walichambue vizuri hili ili hao watoa hukumu waone hukumu zao zikifanya kazi bila 'exception'.
Mmmhhh... hapo nimekuelewa, nilifanya haraka kukujibu nikidhania wewe ndio hujaelewa. Uko sahihi kabisa. inaonekana kwamba mkakati wa Magufuli wa kuwa-freeze wapinzani umefanikiwa kwa kiasi fulani. Huwa hawaonekani kutumia nafasi kama hizi vizuri, ukiacha pengine Zitto Kabwe.

Lakini ni muhimu pia kukumbuka kwamba bado Tanzania mchango wa wananchi ni muhimu sana. Magufuli anafaulu pia kwa sababu akiwatisha au kuwaumiza hao wachache wanaochomoza, wengine wanatulia kimyaaaaa. na ndio maana ni muhimu sana kumuunga mkono Assad. Ni watu wachache sana Tanzania wenye msimamo na nia ya kuyasimamia wanayoamini, through to a destructive and bloody end, kama inavyoonekana Assad yuko tayari.

Kingine kinachoweza kuchombeza "Mahakama ya Wananchi" ni uwepo wa Kura za Maoni. Hii ndiyo ilimwokoa Bill Clinton kwenye ile kashfa ya Lewinsky. wamarekani kila wakihojiwa walikuwa consistently wakionesha imani na Bill. ikabidi republican warudi nyuma. sisi haka ka utafiti ka Twaweza kuhusu kushuka kwa umaarufu wa Magufuli kalileta kizaa zaa...
 
ha ha etizitto kabwe kafanya nini kushinda hao wanaolazwa magerezani kila sikuacheni upambe wa kipumbavu kutenganisha wapinzani wapinzani wameshakusanya evidance za kutosja kutoka kuuwa wawa kushambuliwa na marisasi na kufungwa litakapozuuka la kuzuka magufuli atafute nchi mchawi mwizi na fisadi mkubwa
 
Kwanza ni mhimu kuelewa kama 'Mahakama' hiyo ipo na ina uwezo wa kutoa maamuzi.
Kwa maoni yangu, 'Mahakama' hiyo haipo, au imevurugwa maksudi isijue kuwa inao uwezo wa kutoa maamuzi inapotakiwa kufanya hivyo bila ya kulubuniwa kwa njia yoyote.

Mbaya zaidi ni kuwa wahusika wanapata ujasiri wa kufanya wanayofanya wakijua 'Mahakama' si chochote, si lolote. Kwa hiyo uamzi wa mahakama hauwanyimi usingizi kabisa kwa yote wanayoazimia kuyafanya.

CAG hana sababu yoyote ya kuteteleka. Afanye kazi yake kwa uadilifu alionao siku zote. Haya ya watu pembeni, acha wahangaike na mzigo walioubeba. Wakiamua kufanya mambo nje ya taratibu ili azma yao ya kumwondoa CAG itimie, hilo lisimpe taabu. Kwani alapa kuwa CAG hadi kifo? Acha wajifedheheshe wenyewe, hilo sio tatizo lake.
Inavyoonekana CAG wala hatawapa nafasi wapumue. atapambana nao mpaka kieleweke
 
Rafiki yangu mmoja aliyekuwa akifanya kazi kwenye taasisi ya kimataifa alitengenezewa zengwe na watumishi wenzake Watanzania waliomuona mkali na hataki ubabaishaji wa Kitanzania. Baadhi ya watumishi walioshindwa kuhimili na waliamua kuacha kazi. Kabla ya kufanya hivyo walimtuhumu bosi kwa unyanyasaji wa kijinsia wakijua kwa shutuma hizi huyo bosi naye hatapona. Kweli hakupona. Alitakiwa naye aache kazi lakini alikataa katakata na kutaka mwajiri amfukuze kazi! Kwa shirika la kimataifa lenye maadili ilishindikana kumfukuza kazi na badala yake ilibidi kumuomba na kumpa package nzito. Bado alikataa hiyo package!

Huyo ni mTanzania?

Nina hakika kabisa bila ya wasiwasi yote kwamba kama ni mTanzania, hawezi kuwa mwanachama wa CCM ya sasa!

Watu 'principled' namna hiyo siku hizi wanajificha, hawataki kujitokeza na kulitumikia taifa letu.
Hawa wachache, kama akina Assad, wanapofichuka wanageuzwa kuwa maadui wa taifa. Huko ndiko tulikofikia kama nchi sasa!
 
ha ha etizitto kabwe kafanya nini kushinda hao wanaolazwa magerezani kila sikuacheni upambe wa kipumbavu kutenganisha wapinzani wapinzani wameshakusanya evidance za kutosja kutoka kuuwa wawa kushambuliwa na marisasi na kufungwa litakapozuuka la kuzuka magufuli atafute nchi mchawi mwizi na fisadi mkubwa
Sijui kama unanielewa ninachotaka kusema. Hata mimi Zitto Kabwe namtazama kwa umakini. hii ni kutokana na jinsi alivyokuwa enzi za JK, na pia hata baadhi ya tabia zake zinatia mashaka. Lakini wakati wa Magufuli mwenyewe ametambua kwamba gia ya wakati ule haitafaa kwa wakati huu wa Magufuli. kumbuka kwamba zitto alibaki bungeni wakati Magufuli anahutubia bunge kwa mara ya kwanza na wapinzani walitoka nje kupinga ishu ya uchaguzi wa Zanzibar, wakimtetea Maalim Seif. inashangaza kidogo kwamba ni chama cha Zitto Kabwe, ACT, ndicho Maalim ameamua kujiunga nacho!! ndio siasa. Lakini haikumchukua Zitto muda mrefu kutambua kwamba Magufuli siyo JK. sasa tunamuona Zitto ambaye "ameundwa upya". anapambana sana na anatoa matamko kila mara, na misimamo kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa yanayoihusu nchi yetu. hii ni muhimu sana kwa wapinzani. siyo lazima mtu yule yule aseme lakini inafaa wakiwa na kautaratibu ka kureact katika masuala ya kisiasa na kiuchumi yanayoigusa nchi yetu, na hata yale ya michezo na kijamii kwa ujumla. Si kwamba namwamini sana Zitto hata sasa, lakini ana mambo yanayoweza kusaidia. Maalim Seif anamjua sana Zitto lakini ameona aungane naye kwa sasa.

Ninachosema hapa ni kwamba viongozi wetu wa upinzani hawatumii sana fursa hizi kutoa matamko. licha ya matamko, kuna lile tukio la kuuwawa mwandishi wa habari kule Iringa, Mwangosi, na ile ripoti ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, wakati huo chini ya Jaji Amiri Manento. ripoti hiyo iliishambulia sana serikali na Polisi kwa kuvunja sheria kwa kuwazuia CHADEMA kufanya shughuli zao za kisiasa kwa kisingizio cha SENSA. hoja za Jaji Manento zingefaa sana hata katika hali ya wakati huu ambapo wapinzani wamezuiliwa kufanya mikutano. ningetarajia kungekuwa na MWANGOSI DAY ambapo CHADEMA na vyama vingine vya siasa wangeshirikiana kukumbuka tukio hilo na kumuenzi mwandishi huyo, pamoja na wengine, mfano MAWAZO DAY.

Siyaoni hayo, naamini pia ni wajibu wetu wananchi wa kawaida wenye kujali hali ya nchi yetu, kusaidia na kuwezesha hayo yatokee.
Natambua maumivu wanayopata wapinzani chini ya Magufuli. Mungu tu anajua namna ya kuwalipa, kwa kujitolea kuumia namna hiyo kwa ajili ya "NCHI". Wanaoshindwa WANAUNGA MKONO JUHUDI. Ni rahisi sana kumsifia Magufuli ili upate mradi wako. na ni maisha magumu sana kumpinga Magufuli. ni vema kuunganisha nguvu sisi wote ili tufanikishe lengo letu, kila mmoja akitoa mchango wake
 
Huyo ni mTanzania?

Nina hakika kabisa bila ya wasiwasi yote kwamba kama ni mTanzania, hawezi kuwa mwanachama wa CCM ya sasa!

Watu 'principled' namna hiyo siku hizi wanajificha, hawataki kujitokeza na kulitumikia taifa letu.
Hawa wachache, kama akina Assad, wanapofichuka wanageuzwa kuwa maadui wa taifa. Huko ndiko tulikofikia kama nchi sasa!

Mtanzania haswa. Alikuwa anajiamini na alijua hilo zengwe halikuwa na mashiko.
 
Kwanza ni mhimu kuelewa kama 'Mahakama' hiyo ipo na ina uwezo wa kutoa maamuzi.
Kwa maoni yangu, 'Mahakama' hiyo haipo, au imevurugwa maksudi isijue kuwa inao uwezo wa kutoa maamuzi inapotakiwa kufanya hivyo bila ya kulubuniwa kwa njia yoyote.

Mbaya zaidi ni kuwa wahusika wanapata ujasiri wa kufanya wanayofanya wakijua 'Mahakama' si chochote, si lolote. Kwa hiyo uamzi wa mahakama hauwanyimi usingizi kabisa kwa yote wanayoazimia kuyafanya.

CAG hana sababu yoyote ya kuteteleka. Afanye kazi yake kwa uadilifu alionao siku zote. Haya ya watu pembeni, acha wahangaike na mzigo walioubeba. Wakiamua kufanya mambo nje ya taratibu ili azma yao ya kumwondoa CAG itimie, hilo lisimpe taabu. Kwani alapa kuwa CAG hadi kifo? Acha wajifedheheshe wenyewe, hilo sio tatizo lake.
Sasahivi watu wanaenda mahakama ya A.mashariki......uliona yale ya muswada wa habari? Upinzani pia wameend huko kupinga sheria ya vyama vya siasa...washagundua zandani hamna kitu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasahivi watu wanaenda mahakama ya A.mashariki......uliona yale ya muswada wa habari? Upinzani pia wameend huko kupinga sheria ya vyama vya siasa...washagundua zandani hamna kitu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii Mahakama ni bora itumike vilivyo, hapo tunaweza kupenya na kupachika mabao. tayari la muswada wa habari ni bao. njiani hiyo hiyo. wakiziba hapa tunazibua pale
 
Back
Top Bottom