Nini Mkakati wa Rais Magufuli dhidi ya CAG?

Nini Mkakati wa Rais Magufuli dhidi ya CAG?

Mindi

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2008
Posts
3,523
Reaction score
4,998
Ukitafakari yanayoendelea dhidi ya CAG, juu juu inaonekana kwamba ni Bunge ndiyo lina mgogoro na CAG. lakini ukiangalia vizuri, mwenye mgogoro na CAG hasa ni Rais Magufuli.

Ukimwangalia Spika Ndugai siku ile alipotoa kwa mara ya kwanza agizo la CAG kutakiwa kufika mbele ya kamati ya Bunge, akatoa vitisho kwamba ataletwa hata kwa pingu, unaona kwamba hapa kuna kitu nyuma ya pazia. Ndugai aligeuza jambo la kanuni za bunge kuwa jambo la kisiasa. Tena siasa za CHUKI, zinazohatarisha misingi ya taifa letu. Vitisho vya Ndugai viliashiria kwamba tayari "kesi" ya CAG imeshasikilizwa na kutolewa hukumu na Spika mwenyewe. Hukumu ni kwamba CAG ametiwa hatiani tayari toka siku hiyo. kwa hiyo vile vikao vya kamati ya Bunge vilikuwa geresha tu, na pengine ndiyo maana iliamuliwa ripoti ya kamati hiyo iwasilishwe sasa hivi ili kuzuia watanzania wasione huo muunganiko wa "hukumu" ya Ndugai na hukumu ya kamati.

Lakini kubwa zaidi ni swali: Ni nani yuko nyuma ya Spika Ndugai? Maana siyo rahisi Mhimili mmoja uanze kubwata kuhusu mhimili mwingine, pasina "mkuu" wa "MIHIMILI" kujua. Na tulipata mwanga pale mkuu huyu, Rais Magufuli, alipotoa neno kuhusu "kesi" hiyo, kwamba mbona inacheleweshwa? ni siku ile alipoongelea kushangazwa na "upelelezi kesi ya MO". Ni kama alikuwa anataka hukumu itangazwe haraka. Lakini pia ni kama alitaka kujifanya yuko pembeni na jambo hili, wakati ndio hasa stelingi mwenyewe. ni kama alitaka kuonekana anapenda haki itendeke, kama alivyokusudia katika suala la MO. Katika suala la MO, najua mahakama ya wananchi ilishatoa maamuzi na hapo Rais alishachelewa.

Tunapata mwanga zaidi pale Rais alipoamua kupokea Ripoti ya CAG KIMYAKIMYA, wakati alipokea ripoti ya TAKUKURU kwa MBWEMBWE. na akatamba kwamba huyu bosi wa TAKUKURU ni TISS!!! sasa hapa kuna jambo kubwa sana. Tunaweza kuona kwamba ni Rais ambaye kamsusia CAG, na siyo hasa kwa sababu ya alichosema kule UN, siyo hicho tu, bali msimamo wa CAG kutotaka UJINGAUJINGA katika mambo ya matumizi ya Fedha za Serikali. Kwa hio hicho tunachokiona kama "hatua" za Bunge letu, ni hasa mkakati wa Rais Magufuli "kumkata miguu" CAG, akitafuta njia za "kumdhoofisha" CAG ili kukwepa vifungu vya katiba vinavyomlinda, lakini pengine kumfanya awe USELESS, kama ilivyo useless ile TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA. Maana kama ripoti ya CAG haijadiliwi Bungeni, na Rais ndiyo kazisusa, nguvu ya ripoti hizo itatoka wapi?

Lakini, kama katiba inamtaka Rais kuwasilisha bungeni Ripoti yake ndani ya siku 7 tangu kuipokea, ataiwasilisha? na bunge je, litafanya nini kwa ripoti hiyo? Je, uamuzi wa Bunge kumsusia CAG, UMEVUNJA KATIBA? Maana Katiba ndiyo inalielekeza bunge kufanyia kazi ripoti ya CAG. Bunge lina hiari ya kuacha kushirikiana na CAG? Mimi nadhani Bunge halina ubavu wa kumsusia CAG. Linaweza kufanya hivyo kwa KUVUNJA KATIBA, KWA KUSIMAMIWA NA RAIS AMBAYE HAOGOPI KUVUNJA KATIBA, KAMA AMBAVYO AMEFANYA MARA KADHAA.

Kitendo cha Bunge kumhoji CAG kwa kutumia haki yake ya kikatiba ya kutoa maoni, ni cha kuvunja katiba. kama ni hiyo kauli yake CAG, alishafafanua kwamba ni lugha ya kawaida ya kihasibu. NA NI UKWELI.

Sasa Bunge limefanya uamuzi, Magufui amefanya uamuzi, CAG naye kaamua kusimamia aliyoyasema. MAHAKAMA YA WANANCHI INASEMAJE? hilo ndio swali kubwa na muhimu kwa sasa.
 
Wanazidi kumtikisa ili ajiuzulu wapate kumweka kikaragosi chao kitakacho toa report za uongo. Kushabikia uongozi huu uwe na roho ngumu 😂😂
Nadhani mkakati hasa ndio huo. kwamba akishadhoofishwa, aondoke mwenyewe. je, CAG atakubali kuwapa HUO USHINDI WA MEZANI? au atapambana mpaka tone la mwisho la Damu yake? Mimi naona hii ni hatua muhimu sana kwa Prof. Mussa Assad. ameishi maisha ya kutafuta haki, kupambana, na kumwamini MWENYEZI MUNGU. ameshinda hatua mbalimbali mpaka amefika hatua ya FAINALI. amepambana na mafisadi wengine kama akina PROFESA MUKANDALA WA UDSM. sasa Fainali kaingia na DOKTA JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI, anayeshabikiwa na wapambe wengi tu kama akina Ndugai na wengine. Je, atatundika glovu na kujiuzulu pambano, au atapambana na huyu anayejiita MPIGANIA HAKI ZA WANYONGE na kumwonesha hasa ni mtu wa aina gani watanzania wanaye kama rais wao?
 
tabu ya wanasisa ni watu wa kujiinua sana wanakuwa kama wachungaji lakini katika siasa! hawaoni thamani ya kazi ya mtu mwingine na kuithamini bali wanachokiona ni wao kuumizwa na ukweli kuwa ni dhaifu kitu ambacho ni kweli tupu.
 
,-
IMG-20190402-WA0082.jpeg


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
KUPAMBANA NA FISADI mwenye mbawa ngumu sana..
Ila kama katiba inavyosema Rais hatashitakiwa kwa maamuzi aliyofanya kama Rais na sio kwa maamuzi aliyofanya akiwa Rais.. Muda ni katili sana lazma utasema.
 
Mwanafalsafa Socrates aliwahi kutembea mchana wa jua kali akiwa amebeba Taa iliyokuwa inawaka na kutoa mwanga, alipoulizwa na baadhi ya watu waliomuona akiwa anatembea na hiyo Taa haya ndiyo yalikuwa majibu yake "Pamoja na mwanga huu wa jua tulionao bado kuna Watu wako gizani hivyo nawamulikia wapate kuona".
 
Watu wa majungu huona kila kitu fursa. Mmeibuka wasomi wengi wa saikolojia ya Rais. Hongereni. Mnamjua sana. Yani napenda niwapongeze sana. Ila nawashauri mkarudie masomo. Mana nashindwa hata kusema .
 
Mwanafalsafa Socrates aliwahi kutembea mchana wa jua kali akiwa amebeba Taa iliyokuwa inawaka na kutoa mwanga, alipoulizwa na baadhi ya watu waliomuona akiwa anatembea na hiyo Taa haya ndiyo yalikuwa majibu yake "Pamoja na mwanga huu wa jua tulionao bado kuna Watu wako gizani hivyo nawamulikia wapate kuona".
Kuna watu hata wakimulilkiwa na jua, taa, bado hawaoni tu. labda tuwaombee.
 
Watu wa majungu huona kila kitu fursa. Mmeibuka wasomi wengi wa saikolojia ya Rais. Hongereni. Mnamjua sana. Yani napenda niwapongeze sana. Ila nawashauri mkarudie masomo. Mana nashindwa hata kusema .
Lakini si ni kweli? KILA KITU NI FURSA! Yaani umeongea vizuri sana. Ila ulichokosea SISI SIYO WATU WA MAJUNGU. Shida yenu mmekaririshwa kwamba NI KOSA KUKOSOA SERIKALI. Hiyo ni haki yetu kikatiba. kama unaona inakwama kooni achana nayo.
 
Mwanafalsafa Socrates aliwahi kutembea mchana wa jua kali akiwa amebeba Taa iliyokuwa inawaka na kutoa mwanga, alipoulizwa na baadhi ya watu waliomuona akiwa anatembea na hiyo Taa haya ndiyo yalikuwa majibu yake "Pamoja na mwanga huu wa jua tulionao bado kuna Watu wako gizani hivyo nawamulikia wapate kuona".
Umetisha bro. Bro unanikumbusha mbali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni wazi hili bunge hasa spika na naibu wake wanaendeshwa kwa remote kutoka jumba jeupe hapa mpango uliopo ni kwa magufuli kutumia hazina ya taifa kama apendavyo bila ya kufata sheria ya manunuzi wala nini hapa hawamkomoi cag wanawakomoa wananchi wasijuwe namna pesa zao zinavyotafunwa na hao waliowapa dhamana.
 
Back
Top Bottom