Nini Mkakati wa Rais Magufuli dhidi ya CAG?

Nini Mkakati wa Rais Magufuli dhidi ya CAG?

Hii ni wazi hili bunge hasa spika na naibu wake wanaendeshwa kwa remote kutoka jumba jeupe hapa mpango uliopo ni kwa magufuli kutumia hazina ya taifa kama apendavyo bila ya kufata sheria ya manunuzi wala nini hapa hawamkomoi cag wanawakomoa wananchi wasijuwe namna pesa zao zinavyotafunwa na hao waliowapa dhamana.
Dahhhh bunge hoi bin taaban.
Mahakama zinahemea juujuu.
HATUHITAJI KABISA MFUMO UNAOTAKA KULETWA KWA KISINGIZIO CHOCHOTE KILE.
UTAWALA BILA KUFUATA TARATIBU NI KUJITAKIA VITA NA HUKO NDIO TUNAPOELEKEA.
 
Watu wa majungu huona kila kitu fursa. Mmeibuka wasomi wengi wa saikolojia ya Rais. Hongereni. Mnamjua sana. Yani napenda niwapongeze sana. Ila nawashauri mkarudie masomo. Mana nashindwa hata kusema .
Sasa hapa umeandika nini, embu fikiri kidogo, na kwani yanayoongelewa hapa ni uongo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeupenda sana msimamo wa CAG, amekiri kwamba kweli hayo maneno kayatamka na amegoma kuomba msamaha, hiyo ndio maana ya weledi. Bunge haliwezi kumng'oa kisheria, na hata rais akitaka kumng'oa lazima aunde kamati itakayokuwa na majaji toka nje. Hapo ndio kikwazo kitakapotokea. Majaji wa nje hawawezi kutishwa na amri toka juu, na huu mchezo uko wazi kwa CAG kuibuka kidedea. Kama viongozi wengine wa taasisi za kimamlaka kama CDF, IGP, jaji Mkuu nk wangesimamia weledi kama huyu CAG leo hii utawala wa sheria ungeheshimiwa. Lakini hao wengine wameamua kuacha weledi na.kutii amri yake toka juu.
 
Hivi mnadhani CAG hajui kinachoendelea juu yake,hila na mbinu anzochezewa na kwa nini anachezewa? Anacho kufanya ni style ya Muongo nenda nae Hadi kwenye kitasa cha Mlango ili Sisi wananchi wa kawaida tujue Hali halisi inayoendelea dhidi ya nchi hii! Anaweza kujiuzulu mapema kabisa na wala si mfia madaraka kama wao walivyo Ila anakokaa nao Hadi mwisho ili Watanzania tuujue ukweli na kwa maslahi mapana ya nchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MAHAKAMA YA WANANCHI INASEMAJE? hilo ndio swali kubwa na muhimu kwa sasa.

Kwanza ni mhimu kuelewa kama 'Mahakama' hiyo ipo na ina uwezo wa kutoa maamuzi.
Kwa maoni yangu, 'Mahakama' hiyo haipo, au imevurugwa maksudi isijue kuwa inao uwezo wa kutoa maamuzi inapotakiwa kufanya hivyo bila ya kulubuniwa kwa njia yoyote.

Mbaya zaidi ni kuwa wahusika wanapata ujasiri wa kufanya wanayofanya wakijua 'Mahakama' si chochote, si lolote. Kwa hiyo uamzi wa mahakama hauwanyimi usingizi kabisa kwa yote wanayoazimia kuyafanya.

CAG hana sababu yoyote ya kuteteleka. Afanye kazi yake kwa uadilifu alionao siku zote. Haya ya watu pembeni, acha wahangaike na mzigo walioubeba. Wakiamua kufanya mambo nje ya taratibu ili azma yao ya kumwondoa CAG itimie, hilo lisimpe taabu. Kwani alapa kuwa CAG hadi kifo? Acha wajifedheheshe wenyewe, hilo sio tatizo lake.
 
Anaweza kujiuzulu mapema kabisa na wala si mfia madaraka kama wao walivyo

"Kujiuzuru" CAG?

Hapana. Hiyo itakuwa ni kuwapa heshima wasiyostahili.

Njia nzuri ni kwake kufanya kazi yake bila ya kutetereka. Acha wahangaike na kutafuta njia zisizo halali kumwondoa ili wajipake matope wenyewe.
 
Kwanza ni mhimu kuelewa kama 'Mahakama' hiyo ipo na ina uwezo wa kutoa maamuzi.
Kwa maoni yangu, 'Mahakama' hiyo haipo, au imevurugwa maksudi isijue kuwa inao uwezo wa kutoa maamuzi inapotakiwa kufanya hivyo bila ya kulubuniwa kwa njia yoyote.

Mbaya zaidi ni kuwa wahusika wanapata ujasiri wa kufanya wanayofanya wakijua 'Mahakama' si chochote, si lolote. Kwa hiyo uamzi wa mahakama hauwanyimi usingizi kabisa kwa yote wanayoazimia kuyafanya.

CAG hana sababu yoyote ya kuteteleka. Afanye kazi yake kwa uadilifu alionao siku zote. Haya ya watu pembeni, acha wahangaike na mzigo walioubeba. Wakiamua kufanya mambo nje ya taratibu ili azma yao ya kumwondoa CAG itimie, hilo lisimpe taabu. Kwani alapa kuwa CAG hadi kifo? Acha wajifedheheshe wenyewe, hilo sio tatizo lake.
Mahakama ya Wananchi maana yake ni kile ambacho watanzania kwa ujumla wanaamua kutokana na suala fulani. ni maoni yao. kwa mfano, Mahakama ya wananchi ilipitisha hukumu kwamba ni serikali ndio ilihusika katika utekaji wa MO.
 
Ukitafakari yanayoendelea dhidi ya CAG, juu juu inaonekana kwamba ni Bunge ndiyo lina mgogoro na CAG. lakini ukiangalia vizuri, mwenye mgogoro na CAG hasa ni Rais Magufuli.

Ukimwangalia Spika Ndugai siku ile alipotoa kwa mara ya kwanza agizo la CAG kutakiwa kufika mbele ya kamati ya Bunge, akatoa vitisho kwamba ataletwa hata kwa pingu, unaona kwamba hapa kuna kitu nyuma ya pazia. Ndugai aligeuza jambo la kanuni za bunge kuwa jambo la kisiasa. Tena siasa za CHUKI, zinazohatarisha misingi ya taifa letu. Vitisho vya Ndugai viliashiria kwamba tayari "kesi" ya CAG imeshasikilizwa na kutolewa hukumu na Spika mwenyewe. Hukumu ni kwamba CAG ametiwa hatiani tayari toka siku hiyo. kwa hiyo vile vikao vya kamati ya Bunge vilikuwa geresha tu, na pengine ndiyo maana iliamuliwa ripoti ya kamati hiyo iwasilishwe sasa hivi ili kuzuia watanzania wasione huo muunganiko wa "hukumu" ya Ndugai na hukumu ya kamati.

Lakini kubwa zaidi ni swali: Ni nani yuko nyuma ya Spika Ndugai? Maana siyo rahisi Mhimili mmoja uanze kubwata kuhusu mhimili mwingine, pasina "mkuu" wa "MIHIMILI" kujua. Na tulipata mwanga pale mkuu huyu, Rais Magufuli, alipotoa neno kuhusu "kesi" hiyo, kwamba mbona inacheleweshwa? ni siku ile alipoongelea kushangazwa na "upelelezi kesi ya MO". Ni kama alikuwa anataka hukumu itangazwe haraka. Lakini pia ni kama alitaka kujifanya yuko pembeni na jambo hili, wakati ndio hasa stelingi mwenyewe. ni kama alitaka kuonekana anapenda haki itendeke, kama alivyokusudia katika suala la MO. Katika suala la MO, najua mahakama ya wananchi ilishatoa maamuzi na hapo Rais alishachelewa.

Tunapata mwanga zaidi pale Rais alipoamua kupokea Ripoti ya CAG KIMYAKIMYA, wakati alipokea ripoti ya TAKUKURU kwa MBWEMBWE. na akatamba kwamba huyu bosi wa TAKUKURU ni TISS!!! sasa hapa kuna jambo kubwa sana. Tunaweza kuona kwamba ni Rais ambaye kamsusia CAG, na siyo hasa kwa sababu ya alichosema kule UN, siyo hicho tu, bali msimamo wa CAG kutotaka UJINGAUJINGA katika mambo ya matumizi ya Fedha za Serikali. Kwa hio hicho tunachokiona kama "hatua" za Bunge letu, ni hasa mkakati wa Rais Magufuli "kumkata miguu" CAG, akitafuta njia za "kumdhoofisha" CAG ili kukwepa vifungu vya katiba vinavyomlinda, lakini pengine kumfanya awe USELESS, kama ilivyo useless ile TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA. Maana kama ripoti ya CAG haijadiliwi Bungeni, na Rais ndiyo kazisusa, nguvu ya ripoti hizo itatoka wapi?

Lakini, kama katiba inamtaka Rais kuwasilisha bungeni Ripoti yake ndani ya siku 7 tangu kuipokea, ataiwasilisha? na bunge je, litafanya nini kwa ripoti hiyo? Je, uamuzi wa Bunge kumsusia CAG, UMEVUNJA KATIBA? Maana Katiba ndiyo inalielekeza bunge kufanyia kazi ripoti ya CAG. Bunge lina hiari ya kuacha kushirikiana na CAG? Mimi nadhani Bunge halina ubavu wa kumsusia CAG. Linaweza kufanya hivyo kwa KUVUNJA KATIBA, KWA KUSIMAMIWA NA RAIS AMBAYE HAOGOPI KUVUNJA KATIBA, KAMA AMBAVYO AMEFANYA MARA KADHAA.

Kitendo cha Bunge kumhoji CAG kwa kutumia haki yake ya kikatiba ya kutoa maoni, ni cha kuvunja katiba. kama ni hiyo kauli yake CAG, alishafafanua kwamba ni lugha ya kawaida ya kihasibu. NA NI UKWELI.

Sasa Bunge limefanya uamuzi, Magufui amefanya uamuzi, CAG naye kaamua kusimamia aliyoyasema. MAHAKAMA YA WANANCHI INASEMAJE? hilo ndio swali kubwa na muhimu kwa sasa.
Bado anaangalia upepo unakoelekea ......... Uzuri au Ubaya ni CAG inaelekea kaamua kuweka msimamo. Ndugai alijichomekea mwenyewe kwa kudai hawatafanya kazi na CAG with their FAKE resolution. Mtu wa kuinusuru hii aibu ni Prof. peke yake!!

Zaidi ya hayo inaelekea hana dalili za kung'atuka .... labda awe forced nyuma ya pazia ....!!
 
Mahakama ya wananchi ilipitisha hukumu kwamba ni serikali ndio ilihusika katika utekaji wa MO.
Heee, naona mimi hili lilinipita pembeni. Sikujua kuwa 'wananchi' walikwisha bainisha hilvyo. Enhee, hibu eleza zaidi, baada ya 'mahakama ya wananchi' kubainisha hivyo,Kama kweli usemavyo ni sahihi ni nini kilifuatia baada ya hapo?

Mi naona hukuelewa nilichoelezea katika bandiko uliloni'quote' hapo juu.
 
Mahakama ya wananchi tushasema kuwa tunataka report aliyoiandaa Bwana Assad iwasilishwe bungeni kwa majadiliano. #westandwithAssad
 
Nadhani mkakati hasa ndio huo. kwamba akishadhoofishwa, aondoke mwenyewe. je, CAG atakubali kuwapa HUO USHINDI WA MEZANI? au atapambana mpaka tone la mwisho la Damu yake? Mimi naona hii ni hatua muhimu sana kwa Prof. Mussa Assad. ameishi maisha ya kutafuta haki, kupambana, na kumwamini MWENYEZI MUNGU. ameshinda hatua mbalimbali mpaka amefika hatua ya FAINALI. amepambana na mafisadi wengine kama akina PROFESA MUKANDALA WA UDSM. sasa Fainali kaingia na DOKTA JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI, anayeshabikiwa na wapambe wengi tu kama akina Ndugai na wengine. Je, atatundika glovu na kujiuzulu pambano, au atapambana na huyu anayejiita MPIGANIA HAKI ZA WANYONGE na kumwonesha hasa ni mtu wa aina gani watanzania wanaye kama rais wao?

Mpaka sasa tushamjua mchawi ni nani hapa
 
Heee, naona mimi hili lilinipita pembeni. Sikujua kuwa 'wananchi' walikwisha bainisha hilvyo. Enhee, hibu eleza zaidi, baada ya 'mahakama ya wananchi' kubainisha hivyo,Kama kweli usemavyo ni sahihi ni nini kilifuatia baada ya hapo?

Mi naona hukuelewa nilichoelezea katika bandiko uliloni'quote' hapo juu.

Hapo kwenye nini kilifuata nikujuze tu kuwa mahakama ya wananchi iliazimia kuwa muda utaongea.. Hatukubali dhulma hizi ziendelee tena.
 
Back
Top Bottom