Nini mchango wa wasomi katika maendeleo ya nchi yetu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini mchango wa wasomi katika maendeleo ya nchi yetu.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Makene, Jul 22, 2012.

 1. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Yaweza kuwa nchi yetu inao wanaojiita wasomi kwa maana ya kuwa na vyeti vinavyoonyesha upeo wa kuhitimu elimu za kufundishwa darasani.
  Jambo la kujiuliza ni kitu gani hawa wasomi wamewezesha nchi yetu kujikwamua katika matatizo yanayowakabili wananchi katika nyanja mbali mbali.
  Je wasomi wetu wameweza kwenda mbele ya mafunzo yao,au wamekuwa watumiaji ya yale yalioandikwa na wasomi wengine.
  Je wanaojiita maprofesa wamefanya nini kuwapita wasiosoma katika kurahisisha utendaji na uboreshaji wa mbinu za kujikwamua kimaendeleo
  Bado tunategemea wataalam toka nchi za wenzetu, je sisi tumefanya nini na wavumbuzi wa mambo mbalimbali hapa nchini.
  Je tuendekeze mfumo wa wasomi wa vyeti bila kutokeza ugunduzi, uvumbuzi na uundaji wa mitambo na mifumo itakayosaidia kuboresha hali na maisha ya watanzania?
   
Loading...