Nini matokeo ya zuio kama Mbowe atatuhumiwa kwa kosa la mauaji?

Moja ya hukumu iliyotolewa na mahakama katika kadhia ya Freeman Mbowe ni zuio kwa polisi kumkamata mpaka hapo kesi yake ya msingi itakapomalizika.

Mwanasheria wake, Lissu alisikika akisema kwa sasa polisi hawaruhusiwi kumkamata Mbowe mpaka kesi yake ya msingi itakapomalizika.

Sijabahatika kupata andiko la hukumu lakini kama ndivyo ambavyo Lissu alisema, basi zuio la Mahakama linazua maswali mengi.

Je, Lissu alimaanisha kuwa hawezi kukamatwa kwa kosa lolote atakalofanya kabla ya kesi yake haijamalizika?

Kama hiyo ni kweli, nini kitafanyika kwa mfano iwapo kama Mbowe atatuhumiwa kwa kosa la mauwaji? Nieleweke kuwa hoja yangu imesimama kwenye nadharia tu.

Je, nini kitatokea kama akikataa kuitikia wito wa kuhojiwa na polisi kuhusiana na tuhuma za mauwaji?

Kama akikubali kuhojiwa na polisi lakini baadaye wakajiridhisha ametenda kosa la mauwaji, Je Polisi watasubiri mpaka kesi yake ya msingi imalizike kabla ya kumfikisha mahakamani? Ikumbukwe mahakama inasimama katika motto inayosema,’’ Justice delayed is justice denied’’.

Kama zuio linahusu pekee suala la madawa ya kulevya, kulikuwa na umuhimu gani wa mahakama kuweka zuio hili wakati polisi walishamkamata, wakamuhoji na kuzipekuwa nyumba zake kabla ya kumwachia usiku wa manane. Kwa mantiki hii zuio la mahakama ni ineffective and vain kwa sababu lilitakiwa litolewe kabla hajakamatwa lakini vile vile halimsaidii kukamatwa kwa tuhuma za makosa mengine.
Mbona povu sana wewe mtu..?
Haya mtuhumu sasa kwa kosa la kuua...
 
Unajua kama ukishakua haumkubali mtu, hata vtu vya kawaida utakua unaviona vya tofauti.
Hivi jf si kwaajili ya critical thinkers?
 
Hata mdogo wangu wa darasa la sita ambae anafahamu kesi aliyofungua Mbowe inahusu nini sidhani kama angeuliza swali kama hilo kwa sababu anafahamu, hata kama jana alisamehewa kula bakora kwa kutokwenda shule bado haimaanishi akifanya kosa lingine hatakula bakora!!
 
Yaan hata sababu ya yeye kuitwa polis huijui....
Rudi kalale.. ukiamka ndio uje tena kupost upya
 
Moja ya hukumu iliyotolewa na mahakama katika kadhia ya Freeman Mbowe ni zuio kwa polisi kumkamata mpaka hapo kesi yake ya msingi itakapomalizika.

Mwanasheria wake, Lissu alisikika akisema kwa sasa polisi hawaruhusiwi kumkamata Mbowe mpaka kesi yake ya msingi itakapomalizika.

Sijabahatika kupata andiko la hukumu lakini kama ndivyo ambavyo Lissu alisema, basi zuio la Mahakama linazua maswali mengi.

Je, Lissu alimaanisha kuwa hawezi kukamatwa kwa kosa lolote atakalofanya kabla ya kesi yake haijamalizika?

Kama hiyo ni kweli, nini kitafanyika kwa mfano iwapo kama Mbowe atatuhumiwa kwa kosa la mauwaji? Nieleweke kuwa hoja yangu imesimama kwenye nadharia tu.

Je, nini kitatokea kama akikataa kuitikia wito wa kuhojiwa na polisi kuhusiana na tuhuma za mauwaji?

Kama akikubali kuhojiwa na polisi lakini baadaye wakajiridhisha ametenda kosa la mauwaji, Je Polisi watasubiri mpaka kesi yake ya msingi imalizike kabla ya kumfikisha mahakamani? Ikumbukwe mahakama inasimama katika motto inayosema,’’ Justice delayed is justice denied’’.

Kama zuio linahusu pekee suala la madawa ya kulevya, kulikuwa na umuhimu gani wa mahakama kuweka zuio hili wakati polisi walishamkamata, wakamuhoji na kuzipekuwa nyumba zake kabla ya kumwachia usiku wa manane. Kwa mantiki hii zuio la mahakama ni ineffective and vain kwa sababu lilitakiwa litolewe kabla hajakamatwa lakini vile vile halimsaidii kukamatwa kwa tuhuma za makosa mengine.
Roho za kichawi
 
Hawawawezi kukuelewa mpaka jambo hili liwe kitendo na si nadharia.
Dunia uwanja wa fujo
 
Upumbavu mwingine huu,mi nikajua Mbowe ameua mtu kumbe ni shetani anamuombea mabaya
 
Wanadamu tumejisahau sana, na ~imagine aina ya kiumbe anayependa mwenzake yamkute haya, ndugu zangu hata kama huguswi lakini ipo siku lazima utapitia magumu, TUTOFAUTIANE KIITIKADI ILA TUJUE SISI NI WA MOLA NA KWAMBA UPO MWISHO WETU UWE MTWANA AU LAA !
 
Moja ya hukumu iliyotolewa na mahakama katika kadhia ya Freeman Mbowe ni zuio kwa polisi kumkamata mpaka hapo kesi yake ya msingi itakapomalizika.

Mwanasheria wake, Lissu alisikika akisema kwa sasa polisi hawaruhusiwi kumkamata Mbowe mpaka kesi yake ya msingi itakapomalizika.

Sijabahatika kupata andiko la hukumu lakini kama ndivyo ambavyo Lissu alisema, basi zuio la Mahakama linazua maswali mengi.

Je, Lissu alimaanisha kuwa hawezi kukamatwa kwa kosa lolote atakalofanya kabla ya kesi yake haijamalizika?

Kama hiyo ni kweli, nini kitafanyika kwa mfano iwapo kama Mbowe atatuhumiwa kwa kosa la mauwaji? Nieleweke kuwa hoja yangu imesimama kwenye nadharia tu.

Je, nini kitatokea kama akikataa kuitikia wito wa kuhojiwa na polisi kuhusiana na tuhuma za mauwaji?

Kama akikubali kuhojiwa na polisi lakini baadaye wakajiridhisha ametenda kosa la mauwaji, Je Polisi watasubiri mpaka kesi yake ya msingi imalizike kabla ya kumfikisha mahakamani? Ikumbukwe mahakama inasimama katika motto inayosema,’’ Justice delayed is justice denied’’.

Kama zuio linahusu pekee suala la madawa ya kulevya, kulikuwa na umuhimu gani wa mahakama kuweka zuio hili wakati polisi walishamkamata, wakamuhoji na kuzipekuwa nyumba zake kabla ya kumwachia usiku wa manane. Kwa mantiki hii zuio la mahakama ni ineffective and vain kwa sababu lilitakiwa litolewe kabla hajakamatwa lakini vile vile halimsaidii kukamatwa kwa tuhuma za makosa mengine.
Maneno mengi bila hoja ya msingi yanachosha! Unauliza kitu kisicho na logic! Context ya zuio inajieleza!
 
Akili zako zote ndiyo hizohizo? Au nyingine umezipeleka kuzihifadhi Kule kwenye jukwaa la wakubwa
 
Back
Top Bottom