MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Moja ya hukumu iliyotolewa na mahakama katika kadhia ya Freeman Mbowe ni zuio kwa polisi kumkamata mpaka hapo kesi yake ya msingi itakapomalizika.
Mwanasheria wake, Lissu alisikika akisema kwa sasa polisi hawaruhusiwi kumkamata Mbowe mpaka kesi yake ya msingi itakapomalizika.
Sijabahatika kupata andiko la hukumu lakini kama ndivyo ambavyo Lissu alisema, basi zuio la Mahakama linazua maswali mengi.
Je, Lissu alimaanisha kuwa hawezi kukamatwa kwa kosa lolote atakalofanya kabla ya kesi yake haijamalizika?
Kama hiyo ni kweli, nini kitafanyika kwa mfano iwapo kama Mbowe atatuhumiwa kwa kosa la mauwaji? Nieleweke kuwa hoja yangu imesimama kwenye nadharia tu.
Je, nini kitatokea kama akikataa kuitikia wito wa kuhojiwa na polisi kuhusiana na tuhuma za mauwaji?
Kama akikubali kuhojiwa na polisi lakini baadaye wakajiridhisha ametenda kosa la mauwaji, Je Polisi watasubiri mpaka kesi yake ya msingi imalizike kabla ya kumfikisha mahakamani? Ikumbukwe mahakama inasimama katika motto inayosema,’’ Justice delayed is justice denied’’.
Kama zuio linahusu pekee suala la madawa ya kulevya, kulikuwa na umuhimu gani wa mahakama kuweka zuio hili wakati polisi walishamkamata, wakamuhoji na kuzipekuwa nyumba zake kabla ya kumwachia usiku wa manane. Kwa mantiki hii zuio la mahakama ni ineffective and vain kwa sababu lilitakiwa litolewe kabla hajakamatwa lakini vile vile halimsaidii kukamatwa kwa tuhuma za makosa mengine.