Nini maoni yako kuhusu Utendaji wa Spika wa kwanza mwanamke Tanzania

Old ManIF

Senior Member
Dec 1, 2010
104
2
Baada ya Tanzania kumpata spika mwanamke wa kwanza na kuandika historia mpya ya bunge la nchi hii unaweza kusema nini juu ya utendaji wake so far. Kuna matumaini yeyote ya kupata ufanisi wabunge letu kwa kuzingatia jinsi anavyo liendesha bunge mpaka sasa na uwezo wake au matumaini ya ufanisi wa bunge yana fifia.
 
Kwa uelewa wangu mdogo kutokana ufuatiriaji wangu wa bunge hili la kumi, imejidhihirisha kuwa Spika huyu kwel alitumwa na watu fulani kwa atili ya maslah yao binafsi. Hamna umaana wowote wa kuwa na bunge kwa jinsi anavyoliendesha, hastahil kuwepo mahal alipo ni hayo tu.
 
Bado ni mapema sana, tumpe muda kidogo! Kumbuka hata Sita alivyokoroga enzi za akina Zito na Buzwagi, lakini baadae akajirekebisha!
 
Kwa udhaifu aliouonesha mpaka sasa, mimi naona hatafaa kabisa. Ni bora jiwe lingewekwa kwenye nafasi yake. Kwa nini nasema hivi,
1. Amekataa kurudisha suala la Richmond bungeni.
2. Kuongoza bunge kama vikao vya wamama wa salooni. Yaani anaruhusu mipasho bungeni ambayo haina maslahi kwa Watanzania.
3. Anaitetea serikali wazi wazi kwa masuala ambayo ni maafa kwa taifa, mfano suala la Lema na waziri mkuu. Halijadaliwa na badala yake amelifanya lake peke yake.
4. Alikataa kujadili suala la Gongo la mboto kama suala la dharua. Na kwa sababu hiyo hatuelewi mustakabali wa maghala ya silaha nchini kwani baada ya hapo hali kama hiyo ilitokea shinyanga tena.
5. Katika kipindi chake ameshindwa kulisaidia taifa kutoka katika mgao mkubwa kabisa wa umeme ambao umedumu kwa mda mrefu mno.
 
Maoni yangu ni kwamba Mama Anne Makinda amewaangusha wanawake wa Tanzania kwa udhaifu mkubwa anaouonyesha katika utendaji wake, anaonyesha jinsi asivyoamini kuwa bunge ni chombo ambacho kina haki sawa na serikali (executive) na anataka kutuambia kuwa mawaziri wa Tanzania ni malaika hivyo hawawezi kusema ukweli. Kwa mara ya pili amepindisha kanuni za bunge kuwakandamiza wabunge pale ambapo alitakiwa kutoa ufafanuzi amemkandamiza mbunge badala ya kumwajisha waziri aliyesema uongo... sasa wakosaji wanalindwa!
 
Mnafiki tu hana lolote kaahidi UMOJA lakini naona yeye ndie anayewagawa watanzania....:rip:CCM na viongozi wake.
 
Baada ya Tanzania kumpata spika mwanamke wa kwanza na kuandika historia mpya ya bunge la nchi hii unaweza kusema nini juu ya utendaji wake so far. Kuna matumaini yeyote ya kupata ufanisi wabunge letu kwa kuzingatia jinsi anavyo liendesha bunge mpaka sasa na uwezo wake au matumaini ya ufanisi wa bunge yana fifia.

Rekebisha kauli yako. Ulipaswa kuanza hivi..........

"...Baada ya Mafisadi kumpata spika mwanamke wa kwanza na kuandika historia mpya ya namna ya kulidhibiti bunge la nchi hii ........."

maoni yangu:
mchakato uliotumika kumpata is a total failure; so she is as well a total failure. i don't expect nothing from this old woman.
 
Baada ya Tanzania kumpata spika mwanamke wa kwanza na kuandika historia mpya ya bunge la nchi hii unaweza kusema nini juu ya utendaji wake so far. Kuna matumaini yeyote ya kupata ufanisi wabunge letu kwa kuzingatia jinsi anavyo liendesha bunge mpaka sasa na uwezo wake au matumaini ya ufanisi wa bunge yana fifia.

Hakuna matumaini kabisa,sababu kubwa inayomponza ni ushabiki wa kisiasa anaotumia kwa asilimia mia moja badala ya hali halisi na taaluma ya uongozi ambavyo kwake havipo,mpaka sasa bunge halina ufanisi kabisa ni bunge la enzi ya chama kimoja na kwake ni heri ya lile bunge la chama kimoja la enzi ya Nyerere.
hii ni athari ya watanzania kuchagua wabunge wengi wa chama kimoja.
 
Bado ni mapema sana, tumpe muda kidogo! Kumbuka hata Sita alivyokoroga enzi za akina Zito na Buzwagi, lakini baadae akajirekebisha!

Hakuna dalili zozote za huyu mama kujirekebisha! Ameaingia tu, kabadili Kanuni ili kuikandamiza CHADEMA, amekuwa anaitetea Serikali waziwazi na kuukandamiza upinzani! Kwa ujumla yupo pale si kwa maslahi ya taifa bali kwa maslahi ya CCM na Serikali! Pia hafuati Kanuni za Kudumu za Bunge, kwa mfano, Waziri Mkuu ndiye aliyetakiwa kutoa maelezo kuthibitisha kauli yake kuhusu mauaji na uchaguzi wa meya wa Arusha, lakini Spika akakimbilia kudai eti "Waziri Mkuu hawezi kulidanganya Bunge kwa kuwa aliapa mbele yake" na akamtaka Lema, mtoa hoja ndiye atoe maelezo juu ya uwongo wa Pinda! Wewe unayedai "ni mapema" umechelewa ndugu, huyu mama yuko pale strategically!
 
Makinda kawafanya wanawake wasiaminike tena nchi hii.
Hata wakiwezeshwa hawawezi kwani mafisadi walimwezesha lakini wapi.
 
Hana kitu , ni kilaza tu huyu mwana fisadi. Spika wa nec taifa
 
Wapo Wanawake wengi waliofanya mambo makubwa na wakayasimamia,huyu ni wa aina yake haijapata kutokea
Ana mihemuko ya hasira unamuona kabisa anakunja hata uso wake anapojibu hoja za baadhi ya wabunge haswa wale wanaotoka upinzani
Hangoji mbunge amalize hoja yake yeye anaakatisha tuu kama alivyofanya kwa Tundu Lissu na G.Lemma
Anavyoendesha bungu anaendesha huku akiwaza waliomtuma wanamwangalia,nina amini atakuja kufa kwenye kile kiti kwa sababu hafanyi yale yanayopaswa na spika bali anatekeleza ya watu
hataki mawaziri wajibu maswali anawaambia jibuni harakaharaka
Kwa kweli Spika asipobadili jinsi anavyo liendesha bunge lake atakuja kutoka kuwa spika aliendesha bunge vibaya zaidi kuliko spika yeyote
 
Badili title yako isomeke, NINI MAONI YAKO KUHUSU UCHAFU WA UTENDAJI WA HUYU SPIKA WA KWANZA MWANAMKE TANZANIA.
 
Hovyo kabisa huyu "supika" ameshindwa kuonesha maana ya kuongoza kkikao yuko bias kiasi kwamba sasa mtu anasema uongo halafu yeye anatetea tu na kusema leta ushahidi tuupeleke kamati ya maadili wakati uongo umesemwa hadharani sasa kuuhamishia kamatini si Ufisadi mwingine

AMESHINDWA KUFIKIA KIWANGO NA AMEWAANGUSHA WANAWAKE WENZIE KUWA HAWAWEZI!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mh. Anna Makinda ni nyapala wa mtandao, sasa inategemea wewe unawakilishwa na watu gani, kundi gani kutoa maoni yako..

Na zaidi ya yote haipendi Chadema na wawakilishi wake isipokuwa ktk maswala yasiyohusu Mtandao..
 
Siku zote mtu anapokuwa na uwezo wakushughulikia masilahi yake binafsi tu huyo ni mtumwa(SLAVE) na yule anaehangaika na yake na kuwasaidia wengine kutatua matatizo yanayowakabili huyo ni mtu huru.(FREEMAN).
Huyu mwanamke bwana hastahili kuwa hapo maana kaonesha udhaifu anaficha ukwali anawalazisha watu kung'ata ndimi zao kunakuwa hakuna right decission. "uamuzi wakwanza ni bora kuliko wapili"
makosa yake ya awali ni kipimo tosha kuwa hasitahili.
 
Bahati nzuri namfahamu mama huyu nimefanya naye kazi ni mama mzuri kwa maana ya uelewa wa mambo na kichwani ni mzima sana. Tatizo ni pale aliporubuniwa na mafisadi akahama tumu ya wapambanaji na kujiunga na mafisadi, kiukweli mama huyu hakutegemea kama kuna siku atakuwa spika na mafisadi walilijua hilo wakalitumia akaingia. Ni sawa na mchezaji mwenye mapenzi na Simba anapohamia Yanga kwa sababu ya dau. Mama makinda ni mtu aliyekuwa anachukia sana ufisadi na viongozi wasiowajibika. Kwa hali nimuonayo nayo sasa amepewa kazi ya kuwazibiti wapinzani na kuandaa kusafisha watu ndani ya chama sitegemei chochote kizuri kutoka kwake mpaka mwisho wa bunge hili.
 
The positive side of "madam Chairman" kama rais alivomuita wakati anafungua bunge, ni kwamba ameweza kutudhihlishia kuwa bado wananchi tuna kazi kubwa kuleta mabadiliko dhidi ya wanyonyaji. Pia, ameonesha dhairi kuwa waongo na wasanii ktk mambo ya kitaifa bado wanalindwa, tatu, analeta utata kwetu wanaume kuendelea kuwaamini wanawake kama wanaweza kujisimamia , pia ameonesha kuwa Tanzania hamna SEPERATION OLF POWERS,HAPA BUNGE LINAONGOZWA KUTOKEA KWA RA IGUNGA NA MAGOGONI,mwisho: yupo kwa kuwa yupo na kwa kuwa hakuna mtu mwingine wa kumpa uspika!
 
Back
Top Bottom