Nini manufaa ya Tanzania Diaspora Conference hizi kwa Nchi ya Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini manufaa ya Tanzania Diaspora Conference hizi kwa Nchi ya Tanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zinedine, Oct 7, 2012.

 1. Zinedine

  Zinedine JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,189
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa nikiona delegation kubwa za high profile leaders wa Tanzania kwa maana ya Viongozi Watendaji wakuu wa Serikali (Wakurugenzi wa Mashirika, Idara na baadhi ya Makatibu Wakuu wakitumia fedha za wavuja jasho kwenda kwenye mikutano hii ya Diaspora nchi za Amerika na Canada. Ukifuatilia kinachofanyika kule ni kama aina flani ya siku ya furaha ambayo baadhi ya Watanzania wenye mamlaka katika Serikali wameamua kwenda kufurahika ughaibuni ilihali Watanzania walio wengi wanakosa kisima chenye thamani chini ya Tiketi ya mtu mmoja anayekwenda kwenye Diaspora Conference hizi.
  MICHUZI: Uhaba wa Maji kijiji cha Mkata
  Naomba kueleshwa yafuatayo wana JF
  1. Ni manufaa gani Tanzania imeyapata au inayapata kwa kupitia Diaspora Conference hizi
  2. Je ni vifungu gani vya fedha wanavyotumia Wakurugenzi na Makatibu Wakuu hawa kuhudhuria Conference hizi? Je Bunge la Tanzania limepitishaje vifungu hivyo? Na je fedha zinatoka wapi kwani tunasikia hata Mishahara nyie mlio Serikalini kupata mgogoro?
  3. Je hawa wanaokwenda kushiriki Conference hizo wanawatendea vyema Watanzania? tuwaweke kundi gani?
  4. Je kuna yoyote ambaye anaweza kutuma orodha kamili ya Watendaji Wakuu hao na gharama zao?
  matukio-michuzi: President Kikwete opens the Tanzania Diaspora Conference in Edmonton, Canada, October 5, 2012
  Plz naomba mchango wenu wana JF
   
 2. Mipangomingi

  Mipangomingi JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,719
  Likes Received: 980
  Trophy Points: 280
  Dah, yaani ukifungua hizo link mbili ulizoweka mkuu Zinedine, zinatia hasira na hapohapo unapatwa na mawazo ya ajabu sana. Yaani watu wanafurahika kwa kodi za watu waliochoka hivyo kwa ajili ya kutafuta maji, maji tena Tanzania? Aisey!!!!!!!? Haya
   
 3. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2012
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Mkuu Zidedine Swali lako ni gumu na si rahisi kumpata wa kulijibu sawasawa.Wazo hili la kuanzishwa Umoja wa Watanzania wanaoishi Diaspora liliibuliwa huko UK na Watanzania wanaoishi huko,Hii ilitokana na idadi ya Watanzania kuwa kubwa nje ya Nchi.Mpango huu ni wa kawaida tu kwa Nchi nyingi na mara nyingi matokeo yake ni kupata unafuu wa maisha na huduma haswa tunapoishi ugenini.Kwa kuzingatia hilo Watanzania wakaamua kushauriana na watu wa nyumbani (Tanzania) ili kuangalia uwezekano wa kuwatambua Watanzania waishio Nje.Sababu hiyo ndio imepelekea kuundwa kwa Jumuiya hizo za Tanzanaians in Diaspora.

  Jumuiya kama hiyo iliyokuwa Uingereza imekosa nguvu na nafikiri itakuwa imekufa kifo cha kimya kimya,Jumuiya kama hiyo ilianzishwa USA huko Houston mwaka 2008 na kuitwa jina la (DICOTA),Mara ilipoanzishwa Jumuiya hii ilionekana ina nguvu na ilikuja na agenda za nguvu na zenye mishiko kwa watu wanaoishi Amerika,baadhi ya mambo muhimu yaliyokuwa yanajadiliwa katika mkutano ule ni namna ya kuwatambua Watanzania wote wanaoishi Amerika kwa kuanzisha Jumuiya ndogo ndogo ktk miji mbalimbali yenye Watanzania,na idadi ya Watanzania hawa iwakilishwe Ubalozini kwa Utambuzi.Pia lilizungumzwa swala nyeti la Uraia wa Nchi mbili,suala hili lilifikishwa nyumbani (Tanzania) na kuanza kufanyiwa kazi.Mlezi wa Chama hichi kwa wakati ule alikuwa Balozi Ombeni Sefue (Kwa sasa ni katibu mkuu kiongozi).Kwa kupitia busara na hekima za Mzee huyu,Vyama hivi viliweza kutambulika nyumbani na kupelekea kuundwa kwa Idara maalum Wizara ya mambo ya Nje inayoshughulikia Watanzania waishio Nje.Idara hiyo inaongoza na Mama mwenye wadhifa wa Kibalozi.
  Baada ya kuundwa kitengo maalumu cha kuwasikiliza,kuwashauri na kuwataka Watanzania waishio Nje kushiriki moja kwa moja shughuli za nyumbani kama uwekezaji,serikali ilianza kuyashauri mashirika kama NSSF,BOT,CRDB,TRA na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuja kila mwaka kuwasikiliza,kushauriana na kuona nini kinaweza kufanyika Watanzania wa nyumbani na hawa waliopo Ughaibuni waweze kunufaika na ukaaji wao Nje.Kama ilivyo kwa Watanzania wengi,Ubinafsi,kutokuwajibika na udokozi ulianza kujitokeza ktk Jumuiya ya USA,Kwani Mkutano wake wa pili wa Minneapolis,MN ulikumbwa na kashfa ya Uizi na matumizi mabaya ya pesa ama zilizochangwa ama zilizotoka kwa Wadhamini.Mkutano ule wa pili ulikuwa na mafanikio makubwa kwani ulihudhuriwa na Watu wengi si kutoka ndani ya Marekani tu,bali hata watu wengi walikuja kutoka nyumbani,na ndio kulianzishwa mfuko wa Bima wa WESTADI.

  Baada ya mkutano wa Minneapolis,Uongozi wa Juu wa DICOTA ulianza kuparaganyika na kila mtu kuanza kutafuta umaarufu binafsi,ama kwa sababu ya kuwa na miradi nyumbani ama kutaka kujulikana na Viongozi mbalimbali Wizarani na kwenye Mashirika ili iwe rahisi kwao kufanikisha mambo yao.Chama hichi ndani ya USA kinaonekana kama cahama cha wajanja wachache wanaojitafutia maslahi yao binafsi.Wajumbe waliokuwa wanakuja kutoka nyumbani waliambiwa kuwa mnakwenda USA kuonana na watu wanaoweza kuwekeza,ukweli wa mambo watu wengi waliopo Nje hawana uwezo wa kuwekeza,wengi ni watu wa maisha ya kawaida na wanasaidiwa sana na system kuishi maisha mazuri,Majina kama Lawyer,Dr,Prof au Engineer sio kigezo cha uwekezaji.

  Mkutano wa Tatu wa DICOTA uliofanyika Washington DC ulipoteza lengo lake na kuonekana kuwa ni mahali watu wanakutana kwa ajili ya social gathering tu,session za asubuhi zilikuwa hazina watu wa kutosha,watu walionekana jioni kwenye chakula,vinywaji na disco.NSSF pia walisema wazi kuwa hawawezi kuhudhuria mikutano hiyo kwa sababu haina Tija kwao,NSSF walianzisha mpango wa Bima uitwao WESTADI baada ya kuitumia Dicota sasa wameanza kupita ktk miji mbalimbali kutafuta wanachama wenyewe.Watanzania waliopo California baada ya kuona kuzorota kwa Dicota wameanzisha umoja mwingine ambao unajulikana kwa jina la TIG (Tanzania Investment Group).Mkutano wa mwaka huu uliofanyika Chichago.Il ndio umekosa mvuto na nafikiri ndio utakuwa mkutano wa mwisho wa umoja huo.

  Mkuu Zidedine, Hizo picha zinaonesha ni kiasi gani,Viongozi wetu wanaoambatana na Rais wanavyotumia vibaya pesa za walipa kodi,ama kwa kutokujua ama kwa makusudi.Hakuna uwezekano wowote wa kuunda Jumuiya wa Watanzania yenye nguvu na manufaa bila kuwa na vyama vyenye nguvu vya watanzania katika majimbo mbalimbali.Fanya research yako mwenyewe na uliza Watanzania waishio Nje haswa States,"DICOTA ina malengo gani?" Utapata mlishonyuma mbaya.
   
 4. Zinedine

  Zinedine JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,189
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Asante sana mkuu Mwawado kwa maelezo ya kina ambayo kwa kiasi kikubwa yanatoa majibu ya maswali yangu. Kimsingi binafsi niko aware juu ya treatment za nchi mbalimbali kwa wananachi wao wanaoishi nje ya nchi, kilichonishtua ni jinsi Taasisi/Wizara zetu zinavyojaribu kujenga image kuwa hawa watu ni "typical tycoons" ambao wana uwezo mkubwa wa kuwekeza huge investment kule Tanzania. Bahati nzuri maelezo yako yameonyesha kuwa hilo sio sahihi kwani na wenyewe kwa kiasi fulani ni waganga njaa wanaotegemea kodi za Watanzania wenzao kuendesha ndoto zao, sio mbaya ni Watanzania ambao wana haki ya kutumia matunda ya Nchi yao, lakini je namna tunavyozifanya hizi conference ni sahihi? Je ni taasisi hizo tu ulizotaja ndizo zinazohudhuria mikutano hioyo? je matumizi ya kodi za Watanzania wengine wa kule Kigogo na Tandika zinatumiwa ipasavyo? Na ni sasa ushauri wako ili pawepo na win-win scenario ya Conference hizi provided katika uchanga ilizonazo, tayari private interests zina-outway public interest?
   
 5. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Mimi nilikuwepo kuanzia kuanzishwa kwa DICOTA hadi sasa na nimeenda mikutano yote. DICOTA haitaweza kufa lakini itabadilika kwani huwezi kuua nia nzuri hata simu moja. Kuna watu wengi DICOTA walio na mawazo mbalimbali na mpaka sasa imefanikiwa kwenye awamu ya kwanza ya lengo lake. DICOTA kwa sisi ambao hatupo kwenye uongozi lakini tunaandika Policy zake ilikuwa na nia mbili kuu kwenye stage tofauti (1) Kuunganisha DICOTA na Tanzania ili Watanzania na wapenda Tanzania waweze kupata mawasiliano ya moja kwa moja na serikali na sasa kuna nafasi tatu (a) Balozi wa Dispora (b) Mshauri wa Dispora wa waziri mkuu (c) Mshauri wa Dispora wa raisi wa Zanzibar. Hili nafasi ni sehemu muhimu ya kwanza ambayo ni lazima iwepo ili agenda na serikali iweze kusikia na kushauria moja kwa moja (2) Kuanza kufanikisha Policy ambayo ndiyo stage inayotakiwa kuwepo sasa na kwenda mbele. Kwa ufupi ni kwamba Je DICOTA tunataka nini?? hii stage inahitaji sera mpya na viongozi wapya kwani viongozi wa sasa mawazo yao yamefikia mwisho. Sisi na vijana wengine tunataka tukae chini na kuandika agenda mpya za DICOTA Mfano mkutano ujao tunafikiria uwe wa wawekezaji wa Oil and Gas hivyo tutaweka Kampuni zote zinawezoweka mafuta, watafuta kazi wote, wapenda Tanzania na kuwakutanisha ili watu wote wanaotaka kazi za oil na Gas wakutane na wewekezaji na wafanyabishara wengine waweze kukutana na wawekezaji. serikali inatakiwa kutuma maafisa wachache tu na hii mikutano ni Watanzania wa Dispora wanalipia wenyewe kufanyika. Ukweli ni kwamba inabidi DICOTA ianze kuwa ya agenda za manufaa ya moja kwa moja.

  Kuhusu uongozi Watu walioanzisha chama chao California ni kwasababu walikuwa wanataka kufungua kitu tofauti cha biashara na ili ni ya kibiashara na sio Non Profit Organization kama DICOTA ni vizuri walivyofanya kwani kama una nia ya biashara isiwe kitu cha siri bali fungua Org yako yeni nia ya uwazi.

  Mgogoro wa uongozi Watanzania wengi wanatabia ya kupenda sifa kwa mawazo yangu. Watu wengi wamesusia kwasababu wenyewe hawako kwenye uongozi lakini hao hao watanzania walikuwa hawajui agenda za DICOTA vizuri hivyo kwa jinsi ilivyokuwa hawa watanzania waliokimbia wasingweza kuongoza ni vyema kimeongozwa na waanzilishi kwa muda ili kiweze kufanikisha agenda ya kwanza iliyowekwa. DICOTA haina pesa na budget yake ni ya mkutano tu hivyo si kweli kwamba kunatatizo la ulaji wa pesa. Community ambazo zinakuwa na mikutano zinapewa fungu la BBQ na mziki hivyo kama kuna matatizo ya matumizi mara nyingi ni kwenye ngazi hiyo na siyo kwenye uongozi wa DICOTA.
  DICOTA itapata watu kwani cha maana ni Agenda kwani watu wakiona mkutano una faida kwao wataenda. Tanzania kwa kiasi kikubwa itabadilishwa na DIASPORA kwenye sera zake za miaka ijayo kama ujui hili basi bado hujui Tanzania inako enda na ndiyo maana vyama vya upinzania vinakuja huku kwa kasi. Seif wa Zanzibar alikuja kimya kimya North Carolina wakati wa mkutano wa Dicota Chicago maana kila mtu anajua hilo.
   
 6. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Watanzania tunapenda mafanikio ya haraka na mambo fasta fasta bila kufikiri kwa kina. So siyo ajabu tunakwama ndani na nje ya nchi!
   
 7. sunshine1

  sunshine1 JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2012
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 523
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 45
  http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/hotuba-ya-mhe-freeman-mbowe-washington-dc
  Hebu sikiliza hii clip labda utapata hapo some points. Diaspora ni muhimu sana na ina msaada mkubwa kwa nchi lakini inategemea na viongozi wa nchi husika wanaitumiaje!
  Wengine wanaitumia kama loophole yakufuja hela za wananchi badala yakuitumia kama njia ya kuongeza income ya nchi!


   
 8. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #8
  Oct 8, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Haina kitu chochote cha maana, hata hii inayoendelea nilialikwa ila ni sehemu tu ya kunywa pombe
   
 9. Kikarara78

  Kikarara78 JF-Expert Member

  #9
  Oct 8, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,164
  Likes Received: 514
  Trophy Points: 280
  Zinedine na Wana JF,
  Mimi sioni tatizo la Diaspora aka Dicota, ni chombo Muhimu kwa Ustawi wa Nchi,
  Ni chombo kinachowaunganisha Watanzania walioko Nje ya Nchi (Sio tu USA, Canada na Uingereza) na Serikali yao.
  Chombo hiki kinawapa Fursa ya kuendeleza Nchi yao kwa Njia aka Nyanza Mbali mbali.
  Nawakilisha.


   
Loading...