Nini Maana ya Transcendental Meditation (Tafakuri inayopita mipaka ya akili)?

Ni mara ya kwanza kuandika katika sehemu hii kama sijakosea. Kuna mambo mengi ambayo huwa nayasoma kupitia uwanja huu ambayo yanafikirisha kwelikweli. Nine wahi kusoma wengi wakielezea kuhusu tahajudi (meditation). Nikawa napenda kujisomea kujua angalau A,B,C lakini katika kusoma nilikutana na hili jambo ambalo linasema liko juu kabisa ya Tahajudi na watu wa tahajudi wanaweza wasilifanye nalo ni Tafakuri inayopita mipaka ya akili. Nataka kujua maswala yafuatayo mwenye ujuzi katika haya mambo?

1. Transcendental Meditation ni kitu gani hasa kwa lugha rahisi?

2. Kinafanyikaje na faida yake ni nini?

3. Hapa Tanzania au Afrika mambo haya yapo? Maana nimeona Marekani kuna Taasisi fulani wanafundisha haya maswala.

Naomba kuwasilisha.

Ahsanteni.
NAAM NAOMBA MNIWIE RADHI NADHANI HUO NI UWANJA WANGU BILA SHAKA MNIPE SEKUNDE KADHAA KUJA KUWAPA A-Z;)
 
Meditation ni pale unapokuwa mmoja ni kile unachokifanyia meditation, zipo schools nyingi tu za meditation.pia kuna dhumuni la kila meditation. Mfano kupata tulizo la ndani(stillness),kukuza ufahamu, ku-manipulate maumbile nk.
Transcendental meditation(MT) dhumuni lake haswa ni kupata tulizo la ndani(stillness or relaxation) ambapo mara nyingi wanatumia mantra meditation.

Meditation ni nini mkuu maana bado hujajibu hapo.
 
Meditation ni nini mkuu maana bado hujajibu hapo.
Kwa mfano,ukiwa umetulia na kuelekeza ufahamu wako wote kwenye sehemu moja labda tuseme kwenye pumzi vile inavyotoka na kuingia,hatimaye ukawa mmoja na pumzi,una kuwa upo kwenye hali ya kumeditate, hivyo njia hii ya kuwa mmoja na pumzi ikaitwa breath meditation au meditation ya pumzi, lakini pia unaweza kuwa mmoja na maneno fulani au silabi ambazo unakuwa unazirudia rudia kichwa huku ufahamu wako unakuwa umeulekeza kwenye hizo silabi mpaka unakuwa mmoja na hzo silabi,hapa unakuwa una meditate kwa kuwa mmoja na silabi,hii inaitwa mantra meditation.hivyo hivyo kuna kuwa mmoja na mshumaa,yani ufahamu unauelekeza kwenye mshumaa hii ni wale wanaotumia mshumaa kumeditate,zote hizi ni meditation.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom