Nini maana ya shikamoo?

Sigara Kali

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2017
Posts
3,729
Reaction score
8,803
Salaam wana MMU

Nauliza nini maana ya neno shikamoo

Manake tangu nakua mkubwa nawasalimu watu kwa kuwaambia Shikamoo ila sijui maana halisi ya hili neno

Mnijuze.
 
Ungeuliza jukwaa la lugha/elimu ungejibiwa kwa ufasaha lakini humu i doubt.
 
Maana yake "niko chini ya miguu yako" au "nashika miguu yako"..salamu hii ilitumiwa sana na watumwa kuwasalimu mabwana zao wakati wa ukoloni,.lakini ikakua na kuchukuliwa kama salamu ya hesh'ma kutoka kwa mdogo kumsalimu mkubwa wake hasa aliyemzidi umri,.
 
Kwa mtu hasiye ndugu yako unatambuaje kama anastahili kupewa shikamoo ?
 
Kuna herufi hapo iliondolewa maana yake ni Shikamboo sasa anayesalimiwa lazima akutie adabu
 
Mke wangu:Shikamoo baba jey
Mimi. Salama tu.
In short hili lisalaam sijawahi kulipenda hata kidogo.
 
Duuuh salamu ya kishenzi kabisa hii na ya kiutumwa,yani nimwambie mtu nipo chini ya miguu yako hapanaa
 
Yep
nitajuaje kama ni mkubwa kwangu na anastahili shikamoo yangu ?

NB: sipendi kusalimiwa/kusalimia shikamoo.
Kama hupendi usiitumie wala nini na haidhuru kitu,.
Kila mtu ana namna yake ya kumtambua mtu aliyemzidi umri..
 
Kimsingi hiyo salamu ilishapitwa na wakati kitambo sema tu jamii imebaki kukariri tu!
Salamu zenye kufaa ni za kiimani Kama vile ;
" Asalam Alyekum " na
Tumsifu Yesu Kristo n. K
Salamu za hivyo ni nzuri sana na zinabeba ujumbe maridhawa !
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…