Nini maana ya serikali?

i411

JF-Expert Member
Mar 23, 2011
906
290
Huu ni matazamo wangu tuu, nimeona katika habari nyingi wabunge wengi wanailalamikia serikali imefanya vile ikapanda ikashuka. Sasa mimi nauliza hivi ni nani serikali? Nazani kunawengine wanavyo sema serikali wanamaanishaa ni JK tuu, Labda wengine ni CCM tuu na wabunge wao. Mimi nazani wabunge wa upinzani ni serikali pia manake wanakutana pamoja huko bungeni na wabunge wote wanalipwa mara 40 ya kima cha chini cha mtanzania.

Mimi naona serikali ni wale watu wote ambao wananafasi katika kufanya maamuzi juu ya mambo ambayo yanaweza kunufaisha umaa. Kwa maana hii serikali inaweza kuwa kuanzia mwalimu wa shule ya msingi, kama anatatizo anapeleka kwa bosi wake "Mwalimu mkuu" yeye atapeleka kwa bosi wake huko wizarani alafu hilo tatizo litapanda mpaka litatuliwe kwa yule aliye na uwezo wa kutatua.

Sasa iwaje wabunge na viongozi wa vyama vya siasa wailaumu serikali wakati wao ni serikali au hawajui wadhifa wao. wanatakiwa watutatulie matatizo yetu siyo watuambie tofauti zao na watendaji wengine wa kazi kila siku.
 
Hiyo unayotaja wewe si serikali, serikali ni wale wenye kutoa maamuzi yanayosimamiwa na rais mwenyewe
na waziri mkuu wake. Maamuzi ambayo mara nyingi yanapingana na bunge na mahakama. Kuwaita wengine
kuwa ni serikali inaweza kukubalika kinadharia lakini si kivitendo.
 
Hiyo unayotaja wewe si serikali, serikali ni wale wenye kutoa maamuzi yanayosimamiwa na rais mwenyewena waziri mkuu wake. Maamuzi ambayo mara nyingi yanapingana na bunge na mahakama. Kuwaita wenginekuwa ni serikali inaweza kukubalika kinadharia lakini si kivitendo.
Maana ya serikali ni kutoa maamuzi.Lakin nmekufaham mkuu!Iwapo hao viongozi wakuu wa serikali wasiposimamia hizo hukum au utawala vizuri tunawafanyaje?Maana huu ni mchezo kwa viongozi wengi hapa Tz...hupewi ifafanuzi au utatuzi kuanzia sehem husika hadi uende juu zaid...sasa hao uliowataja ni viongoz wa juu...tutawalalamikia wapi?
 
Hiyo unayotaja wewe si serikali, serikali ni wale wenye kutoa maamuzi yanayosimamiwa na rais mwenyewe
na waziri mkuu wake. Maamuzi ambayo mara nyingi yanapingana na bunge na mahakama. Kuwaita wengine
kuwa ni serikali inaweza kukubalika kinadharia lakini si kivitendo.
Hapo kwenye red mimi naona kinachotuangusha ni kutokuwepo na vitendo na watu husika kutojua wao ni serikali wanao iwakilisha uma kwa nafasi zao, wanabaki wakiwaambia wananchi serikali imepanda ikashuka wakati wao ni serikali.
 
Maana ya serikali ni kutoa maamuzi.Lakin nmekufaham mkuu!Iwapo hao viongozi wakuu wa serikali wasiposimamia hizo hukum au utawala vizuri tunawafanyaje?Maana huu ni mchezo kwa viongozi wengi hapa Tz...hupewi ifafanuzi au utatuzi kuanzia sehem husika hadi uende juu zaid...sasa hao uliowataja ni viongoz wa juu...tutawalalamikia wapi?

Tupate katiba nzuri itakayoweza kuwawajibisha, hapo ndo kile unachokisema kuwa serikali ni watu kitatimia.
 
Back
Top Bottom