Maana yake ni kwamba ule ni mnada so wanunuaji ndio mnataja bei. Ukiangalia utakuta kuna muda unacount down kwa ule mnada kwisha. Muda utakapoisha ambaye atakua ameweka bei ya juu ya mwisho ndio anakua ameshinda. Kama hujaelewa uliza nifafanue zaid mkuu
Chukulia uko mnadani na mnadi anaanza kuuza ngombe wake kwa kutaja bei ya kianzio labda shilingi 500 wanunuzi mpo zaidi ya 20hivi sasa mnaanza kupambana na bei mwingine atasema 600 mwingine 1000 mwingine 1200 na kuendelea mwenye pesa nyingi atakabidhiwa bidhaa kulingana na utaratibu ...so hiyo ndo place a bid ...sijui kama ntakuwa nimekusaidia?
Nawashukuru wakuu kidogo mmenipa mwanga. Lakini samahani utakuta watu wameplace bid lakin pemben kuna maneno yameandikwa reserve not met. Yanamaanisha nn nayo???
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.