Nini Maana ya Philosophy?

Umemsahau na Jason derulo
 
Hata mwl julius kambarage nyerere ni mmoja kati ya wana falsafa wa dunia hii ktk karne hii tokea afrikaa.
 
Hivi ni kwa nini tunasema Nyerere ni mwanafalsa? Je vipi Kikwete au Ben Mkapa wao siyo wanafalsafa? Kwa nini? Nisaidieni tafadhali
 
Anajiita tu jina afu hajui maana yake
Salam Ndugu,
Kwenye falsafa Kujiita si kitu, pasi na kuishi dhana husika, Ukijiita hivyo pasipo kuishi kanuni hakuna madhara. Moja wapo ya hitajio la falsafa ni Uhuru, Uhuru wa kila kitu, Kuzungumza, Kufikiri, Kutoa changamoto kwenye mawazo ya wengine na vifananavyo.
Hivyo usipate shida, wanafalsafa wote duniani hawajiiti, bali wanaitwa kwa sababu wanaishi falsafa. Tofautisha kuna Kujiita na Kuitwa.

Nije kwenye mada, Falsafa ni Hekima maalumu iliyochanganyika na Upendo, ambao mtu anautoa kwa Mtu kwa Njia ya Maelekezo kwa mtu mwingine, ili mtu huyo aweze kupona (zingatia kupona si ugonjwa tu, ni hali ya Kunusurika kwenye shida yoyote inayomkabilia mwanadamu)
Ieleweke Hekima hiyo inamsaidia mtu yeyote ambaye atapokea maelekezo hayo na Kuyaishi, pasi na kujali Mlengo wa Dini anayotokea. Mwanafalsafa anatakiwa asiwe Mbinafsi wa mawazo, matendo, ndio sababu ya Uwepo wa Upendo na Hekima kwenye falsafa.

Nawasilisha.
 
Hata Wao Pia Ni Wanafalsafa.
Kuwa Mwanafalsafa Sio Lazima Ujue Logic, Metaphysics Au Cosmology.
Ukiwa Na Hekima Ya Kuweza Kutatua Au Kuonesha Njia Ya Kutatua Matatizo Katika Jamii Yako; Kuikosoa Inapokosea Na Kuishauri Namna Bora Ya Kufanya; Kutathmini Mwenendo Wao Wa Sasa Na Kuona Kama Utawafanya Kuwa Jamii Bora Au Duni Miaka Ijayo Na Kuwashauri Njia Mbadala; Wewe Pia Ni Mwanafalsafa.
Ndio Maana Kuna Makundi Mawili Ya Wanafalsafa, Mojawapo Ni Wale Ambao Hawakusoma Falsafa Katika Mfumo Wa Elimu Rasmi (Philosophers By Default)
severinembena
 
Hivi ni kwa nini tunasema Nyerere ni mwanafalsa? Je vipi Kikwete au Ben Mkapa wao siyo wanafalsafa? Kwa nini? Nisaidieni tafadhali
Kwanini tunasema Mwl Nyerere ni mwanafalsafa,
Siku moja tenga muda wako, kaa chumbani kwako sikiliza hotuba zake mbali mbali tena msikilize kwa makini kama ni mtu 'shiiii' basi sikiliza huku unaipiga taratiiibu utapata jibu la swali lako.
 
Falsafa (kutoka Kigiriki φιλοσοφίαfilosofia = pendo la hekima) nijaribio la kuelewa na kueleza ulimwengu kwa kutumia akili inayofuata hoja za mantiki.

Falsafa huchunguza mambo kama kuweko na kutokuweko, ukweli,ujuzi, uzuri, mema na mabaya,lugha, haki na mengine yoyote.

Tofauti na dini, imani au itikadi, njia ya falsafa ni mantiki inayoeleza hatua zake ikiwa tayari kuchungulia upya kila hatua iliyochukua. Kwa hiyo falsafa ni njia ya kuuliza maswali na kutafuta majibu.

Katika lugha ya kila siku neno "falsafa" mara nyingi linachukuliwa kutaja jumla ya mafundisho au imani ya mtu au kundi la watu, kwa mfano "falsafa ya chama fulani", "falsafa ya maisha yangu" na kadhalika. Lakini kwa jumla fikra hizo hazistahili kuitwa "falsafa". Ila tu kuna makundi ya wanafalsafa wanaopendelea mielekeo tofauti na kuhusu haya inawezekana kutumia neno "falsafa ya fulani" kwa kutaja matokeo ya kazi yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…