a sinner saved by Christ
JF-Expert Member
- Feb 19, 2017
- 2,217
- 2,412
Mit 3:5-6umetafsiri kwa usahihi kabisa
1.KIFUNGO cha kiroho ukiwa chini ya kifungo cha kiroho,unaishi maisha ya utumwa,au chini ya kiwango hatima yako au stahili yako..unakosa mafanikia ya kiroho na kimwili uliyostahili ukiyokusudiwa uliyoandikiwa hatima yako...
hati za mashitaka zinazoplekea kumuweka mwanadamu kifungoni moja wapo ni kuishi maisha ya dhambi ,dhambi za sirini au dhambi za matendo,mawazo na maneno..au hata maagano yaliyofanyika na wazazi wetu hata kabla sisi hatujazaliwa..makosa ya wazazi wetu yanaweza kuchangia roho zinazofuatilia hata kwenye familia zinazotembea kwenye damu ya ukoo...
mlango mmoja wapo unao mpa adui shetani na mawakala wake mapepo na washirikina kukushitaki na kukuweka kifungoni ni dhambi unazozifanya bila kutubu na kuziacha,
Kufanikiwa kutoka kifungoni na kukimbia kutok kifungoni..ni jitihada za kujinasua mwenyewe kutoka kifungoni..
njia ya giza ...ni pale jitihada zako binafsi na njia zako binafsi unazopitia za kujinasua mwenyewe kuwa na giza maana siyo njia sahihi mbele zina giza hazitasaidia..
lakini kupata msaada wa mtu mwenye nuru na kukuangazia nuru njia zako ,huyo ni YESU yeye ndiye nuru ya ulimwengu,na Yesu ndiye NJIA, KWELI NA UZIMA
NINI CHA KUFANYA.
Yesu ndiye nuru ya ulimwengu,njia ,kweli na uzima.
Yesu pia anaitwa NENO kama mtafsiri alivyotafsiri kuwa NURU ni NENO la Mungu ,ambao lina nguvu,lina uhai,lina ukali zaidi ya upanga unaokata kuwili.
TUBU dhambi zako na kuziacha
muombe Yesu aongoze hatua zako za miguu yako.
Yesu mkiri kuwa ndiye pekee aliyelioa gharama pale msalabani ili kutuweka huru kweli kweli tusiwe tena chini ya vifungo na utumwa wa dhambi.
Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.
Mit 16:25 SUV
Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu; Lakini mwisho wake ni njia za mauti.
Kut 33:15
Naye akamwambia, Uso wako usipokwenda pamoja nami, usituchukue kutoka hapa.