Nini maana ya maisha?

Yenga08

JF-Expert Member
Jul 7, 2019
464
891
Habari wana janvi,

Naomba mwenye kujuwa maana halisi ya maisha anijuze maana nimekuwa nikifikilia sana kuhusu maisha lakini sipati maana halisi.

Unakuta mtu anasema huyu atakuja kuwa na maisha magumu sana au maisha marahisi sana. Je, maisha ni uhai anaokuwa nao mtu, au maisha ni zile kazi za kila siku zimuwezeshazo mtu kupata riziki, au maisha ni maendeleo anayokuwa nayo mtu.

Mwingine utamsikia inapotokea ajali na kuuwa watu anasema daaah hawa jamaa wamekatishwa maisha.

Je,

Maisha ni kazi?

Maisha ni Uhai?

Maisha ni Maendeleo?

Maisha ni vita?

Maisha ni uzima?

Maisha ni furaha?

Maisha ni shida?

Au Maisha ni nini

Ahsanteni sana.
 
maisha yenyewe kwa ujumla haya maana yoyote, ni jukumu lako kuyapa maisha maisha maana
kile unachofanya kila siku
unavyo waza
matamanio yako ya kila siku n.k
hivi ndo vitakupa wewe maana ya maisha

Au shortly tusema maisha ni wewe
 
Hii dhana nakubaliana nayo mkuu.

Maisha ni vile utaamua,na lengo la maisha unajipangia wewe.

Mtu anazaliwa anakua hata hajui kaja kufanya nini hapa duniani najabu zaidi mtu huyu hata hakuomba yeye aje ni hamu na mapenzi ya wazazi wake tu waliamua wawe na mtoto ndo akazaliwa mtu huyu.
 
M.A.I.S.H.A ni dubwana fulani hivi ambalo huwa linaisha sasa kwa wingi ndio linaitwa MAISHA umoja linaitwa ISHA
 
Acha maswali mengi utachizi wewe chukua k vant yako ndogo,kajike au kitu cha value piga tafuta pic kale kamalize mambo kijana mdogo huna hata mvi moja unaanza kujiuliza maswali magumu hivyo utachizi shauri yako
 
Maisha kibinadamu ni kipindi cha muda kutoka kuzaliwa mpaka kufa

Uzuri na ubaya wa hiki kipindi ni mfululizo wa matukio kuanzia kuzaliea mpaka kufa

Sasa ikitokea ndani ya kipindi hiki matukio yanayojitokeza kwako sio yale uliyoyategemea au yasiyo kufurahisha hapo ndipo unapata maisha mabaya
Kama utapitia matukio yanayokufurahisha hapo ndipo utapata maana ya maisha mabaya

Uzuri n ubaya utaujua wewe
 
Maisha hayana maana
Kwakweli....
Huwa nawaza sababu ya haya maisha ni nini sasa?!! Tunazaliwa tunaishiii wengine tunaoishi kwa tabu basi ni tabu weee, tunakutanishwa na wapendwa wetu (watoto) tabu inaendelea kisha tunakufa....

Maisha hayana maana, nikiwaza kuna siku nitakufa mwili unaishiwa nguvu.
 
Habari wana janvi,

Naomba mwenye kujuwa maana halisi ya maisha anijuze maana nimekuwa nikifikilia sana kuhusu maisha lakini sipati maana halisi.

Unakuta mtu anasema huyu atakuja kuwa na maisha magumu sana au maisha marahisi sana. Je, maisha ni uhai anaokuwa nao mtu, au maisha ni zile kazi za kila siku zimuwezeshazo mtu kupata riziki, au maisha ni maendeleo anayokuwa nayo mtu.

Mwingine utamsikia inapotokea ajali na kuuwa watu anasema daaah hawa jamaa wamekatishwa maisha.

Je,

Maisha ni kazi?

Maisha ni Uhai?

Maisha ni Maendeleo?

Maisha ni vita?

Maisha ni uzima?

Maisha ni furaha?

Maisha ni shida?

Au Maisha ni nini

Ahsanteni sana.

Maisha ni vile unavyoishi
 
Habari JF

Maisha ni nini? Starehe kubwa duniani ni ipi? Furaha ya mwanadamu ni ipi? Kwanini tunaishi? 🤔
 
Tunaishi ili tule, na tunakula ili tuishi,
Hivyo tunaishi ili tuwepo, na tunakuwepo ili tuishi, hata hivyo tuna kuwepo ili tuone yaliyopo, mbaya zaidi tunazaliwa ili tuishi na kikubwa zaidi tunaishi ili tufe over!!!!
 
Kwa hiyo tunaishi ili tule aise🤷‍♂️
 
Back
Top Bottom