Nini maana ya kuweka mali "wakfu" kanisani?

Wakfu kwa Muktadha wa Imani ya Kikristo Kama ambavyo imeulizwa sifahamu Ila kwa Mujibu wa Imani ya Kiislam Wakfu ni Maelezo ya Mali itolewayo na Mwenye Mali kufahamisha kuwa Pindi akifariki au akiwa hai Mali yake iwe kwa ajili ya Jamii.

Mfano unaweza kusema Nyumba Yangu nikifa ikabidhiwe kwenye Madrasa au Taasisi Fulani kwa ajili ya kuihudumia taasisi hiyo.

Angalizo: Kwny Wosia Ili kulinda haki ya Warithi halali hairuhusiwi hata Kama utakuwa umeandika kukabidhi Mali ya Marehemu kwa ajili ya Jamii zaid ya theluthi moja ya Mali zako zote mfano Kama una Nyumba moja peke yake haitaswihi Nyumba hiyo kukabidhi Msikiti na kuacha Familia yako bila ya kitu chochote
 
Wakfu kwa Muktadha wa Imani ya Kikristo Kama ambavyo imeulizwa sifahamu Ila kwa Mujibu wa Imani ya Kiislam Wakfu ni Maelezo ya Mali itolewayo na Mwenye Mali kufahamisha kuwa Pindi akifariki Mali yake iwe kwa ajili ya Jamii.

Mfano unaweza kusema Nyumba Yangu nikifa ikabidhiwe kwenye Madrasa au Taasisi Fulani kwa ajili ya kuihudumia taasisi hiyo.

Angalizo: Ili kulinda haki ya Warithi halali hairuhusiwi hata Kama utakuwa umeandika kukabidhi Mali ya Marehemu kwa ajili ya Jamii zaid ya theluthi moja ya Mali zako zote mfano Kama una Nyumba moja peke yake haitaswihi Nyumba hiyo kukabidhi Msikiti na kuacha Familia yako bila ya kitu chochote
Ahsante Pohamba
 
Ahsante Pohamba

Nyongeza!

1) Wakfu Siku zote hutolewa ni kwa ajili ya Public Use mfano Shule na si kwa individual
2) Kwny Wakfu kuna Mtoaji, Msimamizi wa Ile Property na Wanufaika
3) Hairuhusiwi kubadili Matumizi ya ile Wakfu

Marekebisho ya andiko langu.

Wakfu inaweza kutolewa ukiwa hai au contingent kwa maana unaagiza baada ya kufa kwako!
 
Wakfu=Dedicated.
Kwamba kitu hicho kimetolewa rasmi kwa ajili ya kazi ya Mungu.
Kwa mfano kinanda kuwekwa wakfu=kitafanya kazi ya Mungu tu......na si vinginevyo kama kutumika kwenye singeli kwani chaweza leta...... madhara.
So nikiweka biashara au kazi yangu wakfu ni nini tafsiri yake?
 
Wakfu/Trusts asili yake ni shariah ya kiislamu ambapo mtu anatoa sehemu ya mali yake itumike kwa ajili ya kazi ya Mungu au msaada kwa wasiojiweza mara anapofariki (yaani anaacha kama wosia).

Kwa sheria zetu wakf hufanana sana na trusts ambazo ni mchakato fulani wa kisheria ambapo mtu huamua mali yake itumike vipi kupitia utaratibu wa kisheria ambapo huchaguliwa msimamizi wa mali hizo na huzisimamia kwa manufaa ya wanufaikaji na hazitatumika kwa matumizi mengine isipokuwa tu yale yaliyopangwa na haziwekwi kanisani (Hizi trusts kwa kiswahili huitwa wakfu).

Kwa hiyo ukikuta sehemu wanasema wakfu wa fulani ujue mtu huyo aliweka mali zake kisheria zitumike kwa ajili ya jambo fulani mara anapofariki (Tofauti na wosia wa kawaida). Kwa mfano wakf wa Nobel ambao hutoa zawadi kwa watu waliofanya mambo fulani makubwa katika kuleta amani kila mwaka.
 
Kwahiyo ukiagizwa na mchungaji uweke wakfu mali,kazi na biashara zako kanisani na wewe mwenyewe ungali hai ni sahihi?
 
Itategemea anamaanisha nini katika muktadha wake, si wafahamu maneno huwa na matumizi tofauti. Tukisema askofu fulani anawekwa wakfu hii bila shaka inakuwa tofauti na maana niliyoeleza hapo juu
 
So ni halali kuweka mali wakfu ktk kanisa ambalo lenyewe halijawekwa wakfu?
 
So nikiweka biashara au kazi yangu wakfu ni nini tafsiri yake?
Yaweza kuwa na maana kuwa mrejesho wake, matumizi yake, mapato yake na faida yake ni kwa ajili ya hisani. Hisani kusaidia watu wenye uhitaji ama kazi ya Mumgu kama vile kujenga makanisa, kusomesha wahubiri au watumishi wengine, ama kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
 
Kwahiyo utashi wa kuweka mali zako wakfu uko kwa mtu mwenyewe au ni "lazima" ashawishiwe na wachungaji/mashehe?
 
Back
Top Bottom