Nini maana ya kulala chini unapofiwa?

Nini maana ya kulala chini unapofiwa?

Kwa sisi waxaramo unapofiwa kuanzia siku ile ya kwanza ya msiba mtalala chini kwenye mkeka siku tatu hii tunaita kukaliza maiti siku yatatu asubuhi na mapema tunaamka kwa pamoja tunafagia uwanja pamoja na vyumba vyote walivyolala wafiwa takataka zote tunaweka kwenye sufulia tunachanganya na majivu bibi au shangazi atahusika kubeba kichwani tunaongozana wote kwa pamoja aliebeba sefulia akiwa ametangulia mbele hadi makabulini anatupa sefulia pamoja na uchafu wake haraka sana tunageuza na kuludi nyumbani hiii humaanisha maladh yoyote aliyougua marehemu yasijiludie kwa mwanafamilia mwingine.

Nimeupenda huo utamaduni, una maaana kubwa!
 
hii nayo ni aina ya ushirikina.

Makame umenichekesha kweeelikweli. Mimi nilikwenda katika msiba wa hao jamaa nikaona pachafuuuu nikachukua ufagio nisaidie kazi. Lahaula, niliporwa ufagio kama kibaka anayemkwapua mtu simu! Hawafagii siku 3 na hawaogi pia. Just imagine. mh watu na mila zao...
 
Kwa sisi waxaramo unapofiwa kuanzia siku ile ya kwanza ya msiba mtalala chini kwenye mkeka siku tatu hii tunaita kukaliza maiti siku yatatu asubuhi na mapema tunaamka kwa pamoja tunafagia uwanja pamoja na vyumba vyote walivyolala wafiwa takataka zote tunaweka kwenye sufulia tunachanganya na majivu bibi au shangazi atahusika kubeba kichwani tunaongozana wote kwa pamoja aliebeba sefulia akiwa ametangulia mbele hadi makabulini anatupa sefulia pamoja na uchafu wake haraka sana tunageuza na kuludi nyumbani hiii humaanisha maladh yoyote aliyougua marehemu yasijiludie kwa mwanafamilia mwingine.

Lakini kiukweli hayo maradhi yanajirudia ..ama sivyo?
 
nadhan ni issue ya vitanda kutotosha tu nothing special
 
Kwa sisi waxaramo unapofiwa kuanzia siku ile ya kwanza ya msiba mtalala chini kwenye mkeka siku tatu hii tunaita kukaliza maiti siku yatatu asubuhi na mapema tunaamka kwa pamoja tunafagia uwanja pamoja na vyumba vyote walivyolala wafiwa takataka zote tunaweka kwenye sufulia tunachanganya na majivu bibi au shangazi atahusika kubeba kichwani tunaongozana wote kwa pamoja aliebeba sefulia akiwa ametangulia mbele hadi makabulini anatupa sefulia pamoja na uchafu wake haraka sana tunageuza na kuludi nyumbani hiii humaanisha maladh yoyote aliyougua marehemu yasijiludie kwa mwanafamilia mwingine.

Eeennnh! Wazaramo mna mambo nyie duh.
 
Hahahahaha una utani wa ngumi wewe.

Mkuu,hii ni hatari ujue.....!

Assume mme kaenda kwa ukimwi halafu baada ya mazishi wakabeba sufuria kama kawaida na wakirudi wanaanza kumgombania mjane..! Hapo hamjaandaa masufuria mengine ya kwenda kutupa...! Maradhi yanaondolewa kwa taratibu za usafi wa kawaida pamoja na tiba na si msululu wa watu kumsindikiza mtu nmoja aliyebebeshwa sufuria kichwani.
 
Hapo kwenye ndugu wakirudi, hawalali chini?
Me Mila yangu ni Uislam, tofauti na hapo sina mila ingine,
Mtu akifa, azikwe siku ile ile labda km kafa ucku au jion sana, kumsengenya maiti,

Unapokufa ndio unapozikiwa,
Kulia ruksa ila kuomboleza haifai kwan unakufuru, mf. "baba/mama umeondoka, nitaishi vipi mimi jamani, nani atanitunza, bora tungeenda wote...."
"mume wangu jaman, umeniacha kwanini, nimeumbuka jaman uwiii, Mungu ungenichukua mimi ukamuacha yeye, watoto hawa watatu nawalea vp mimi maskini...."
Baada ya kuzika majiran warudi makwao wabaki ndugu kujadili mustakabali mzima.
Na mengineyo.
 
Kwa sisi waxaramo unapofiwa kuanzia siku ile ya kwanza ya msiba mtalala chini kwenye mkeka siku tatu hii tunaita kukaliza maiti siku yatatu asubuhi na mapema tunaamka kwa pamoja tunafagia uwanja pamoja na vyumba vyote walivyolala wafiwa takataka zote tunaweka kwenye sufulia tunachanganya na majivu bibi au shangazi atahusika kubeba kichwani tunaongozana wote kwa pamoja aliebeba sefulia akiwa ametangulia mbele hadi makabulini anatupa sefulia pamoja na uchafu wake haraka sana tunageuza na kuludi nyumbani hiii humaanisha maladh yoyote aliyougua marehemu yasijiludie kwa mwanafamilia mwingine.

haya Latifa
kama shangazi au bibi hawapo nani anabeba sefulia? je shangazi au bibi akifa atabeba nani?
sefulia sufuria
kujirudia @kujiludia
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom