Nini maana ya hekima na ninawezaje kuipata?

Siyo tu kusoma maandiko matakatifu, Pia na kumwomba Mungu awaye yote akupe hiyo neema. Mfalme Suleiman alimwomba Mungu hekima na akatunukiwa; wakati mwingine hekima hukuzwa na experience ya mtu kwenye maisha aliyopitia.
Umemsoma vzr huyu Suleiman ww??

Kwanza huyu alikuwa na uwezo wa kukomand spirits na angels kwa taaluma maalum (secret knowledge)

Rudi shule
 
Simple tu. Fikiria jambo lolote unaloona la kipumbavu halafu ukilipata kaa kimya usiliseme.
 
Wakuu naona wengi mnajibu kwa mazoea Sana!!


Kwanza fatilieni WISEMEN walikuwa watu hapo zamani.

Wisemen ndo walikuja kuitwa PHILOSOPHERS baadae kidogo.

Naomba mfatilie CHIMBUKO LA WISEMEN/PHILOSOPHERS walikuwa watu wa namna gan na walikuwa na sifa gan na walizipataje hizo sifa za kuitwa WISEMEN/PHILOSOPHERS.

Tumia PYTHAGORAS Kama CASESTUDY
 
Habari wana JF,

Mimi ni mgeni hapa jamvini, nomba niende moja kwa moja kwenye mada kama hapo juu inavyosema.

Ninaomba kujua hekima maana yake nini na ninawezaje kuipata.

Karibuni wakuu.
Soma kwa makini kitabu cha methali/proverbs.

Uzuri kina chapter 31 ... Unaweza soma chapter moja kwa siku baada ya mwezi kitabu kizima kimeisha.
 
Hekima / busara, ni vile unavyo- changanua na kupapambua mambo, bila kutumia jazba wala mihemuko...

Vile unavyofikiri kabla ya kutenda... Hekima unaza rohoni...


Cc: mahondaw
 
Mkuu,Jaribu kumfuatilia Dr. Ellie VD Waminiani yupo Clouds TV kila Jumapili saa 2:30 Asubuhi. Huu ni mwezi wa pili sasa anafundisha kuhusu hekima.
Habari wana JF,

Mimi ni mgeni hapa jamvini, nomba niende moja kwa moja kwenye mada kama hapo juu inavyosema.

Ninaomba kujua hekima maana yake nini na ninawezaje kuipata.

Karibuni wakuu.
 
Hekima ni kujifunza kutokana na uzoefu wako wa mambo uliyoyapitia na kusahihisha pale ulipokosea kwa kufanya hivyo tu ndipo utakapokuwa na hekima zaidi..., kama mtu utakubali kujifunza na kubadilisha makosa yako kulingana na uzoefu wako.., kadri umri wako utakavyoongezeka ndivyo hekima yako itaongezeka.., ndio maana zamani watu walikuwa wanawafuata wazee kwa ushauri....
 
Be Real.. na sikiliza sana kuliko kuongea ili upate kujua mengi kwenye hii Dunia

Baada ya hapo maamuzi utayokuwa unafanya kupitia knowledge uliyonayo ndio hekima huzaliwa hapo..

"Akili kumkichwa na Ujinga pia kumkichwa" Elewa hilo pia
 
Hekima upatikana kwa mlolongo ufuatao; kwanza katika maisha ya kila siku watu hujifunza kwa makosa (mistakes) yao wao wenyewe au kwa makosa ya wengine, hili uzaa uzoefu (experience) na mwisho experience uzaa hekima (wisdom). Kiufupi huo ndio mlolongo wake na wengi wanaokuja kuwa na hekima hujifunza mengi toka makosa ya wengine kuliko makosa yao wenyewe. Hayo yote upatikana baada ya muda mrefu kidogo wa kuishi hapa duniani na si kitu cha ghafla au cha kupata darasani.
Dah! Nilikuwa naona uvivu wa kuandika na namna ya kuipangilia point yangu, lakini bahati nzuri umenisahidia maana nilikuwa na mawazo kama yakwako ila namna ya kuyaweka sasa. Ongera mkuu umeongea point ya msingi kama nilivyokuwa nawaza. Ila cha kuongezea kama ni mkristo ili kujua hekima inapatikanaje msome sana sulemani na upende sana kujifunza vitu tofautitofauti.
 
hekima
ni neno lenye heshima linalo mheshimisha mtu kulingana na matendo yake ama kuchangia kitu kizuri sehemu frani

hekima
huwezi kuipata moja kwa moja mienendo mda mwingine na matendo jinsi unavyowafanyia

hekima
neno lenye sifa ya kumheshimisha mtu kama mtu frani

unapopata na unapokosa inategemeana
huwezi kuipata hekima moja kwa moja
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom