Habari wana JF,
Mimi ni mgeni hapa jamvini, nomba niende moja kwa moja kwenye mada kama hapo juu inavyosema.
Ninaomba kujua hekima maana yake nini na ninawezaje kuipata.
Karibuni wakuu.
Labda nikujibu mkuu kwa uelewa wangu.
HEKIMA ni neno dogo sana kimatamshi, lakini ndani yake limebeba ujumbe mpana katika maisha ya mwanadamu.
Hekima pia, ni uwezo wa kutambua Jambo/ mambo yanayofaa na yasiyofaa.
Mtoto mdogo anapozaliwa, anajifunza kutamka/kuongea kabla hajafundishwa shule. Anakuwa na uwezo wakupambanua mambo mfano kwa jambo baya utamuona akilia kumaanisha ni dalili ya hatari ( Jambo lisilo faa kwake).
Kwa maana nyepesi hapo nikwamba HEKIMA mtu anazaliwa nayo.
Asilimia kubwa ya watu walioishi miaka mingi, hujawa na hekima kutokana na mapito yakimaisha walio yapitia.
Mtu alie jawa na hekima, aendeshwi katika maisha badala yake hekima inamuongoza katika kila hatua anayoiwaza kuichukua.
Ukijawa na hekima, utatenda mambo baada ya kufikiri na ndio maana utaona mtu mwenye kushikilia jambo moja alilokusudia kulifanya! Ndiye mwenye nafasi kubwa yakufanikiwa kuliko yule mwenye kuunga unga mambo.
Itaendelea maana hekima ni somo pana