Nini maana na chanzo cha msemo huu maarufu hapa JF?

SHIEKA

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
8,240
Reaction score
4,280
Ninaposoma thread mbalimbali hapa JF,baadhi ya michango kwenye thread hizo hutumia msemo ufuatao: "..........umekula maharage ya wapi........."

Ni nini maana ya 'kula maharage ya sehemu fulani?' Mtu anayekula hayo maharage anakuaje?

Na chanzo (asili) ya huu msemo ni nini?

Nitashukuru kwa msaada wa maelezo.
 
Imetoka kwa mchungaji Josephat Gwajima kipindi kile anamkashifu Kardinali Pengo!!
 
Pengine ulikuwa nje ya nchi, pengine ulikuwa sehemu isiyo na redio wala network, pengine umeona tu na wewe uanzishe thread.. Umekuwa kama mtoto wa secondari ambaye ulikwa bweni na sasa shule zimefungwa, unabwayabwaya, wasaidie wazazi kazi mzee, google mzee
 
Maneno meeengi ya kejeli ya nini? Ni dalili kwamba hata wewe hujui!
 
Ukila maharage ya mbeya lazima ujambe sana kwa hiyo mtu akikuuliza umekula maharage ya wapi anmaanisha kuwa umejamba sio kwamba umetoa hoja
 
Asante nitonye. Ninaelewa sasa maana ya huo msemo nikiunganisha dots!
 
Last edited by a moderator:
Ninaposoma thread mbalimbali hapa JF,baadhi ya michango kwenye thread hizo hutumia msemo ufuatao: "..........umekula maharage ya wapi........."

Ni nini maana ya 'kula maharage ya sehemu fulani?' Mtu anayekula hayo maharage anakuaje?

Na chanzo (asili) ya huu msemo ni nini?

Nitashukuru kwa msaada wa maelezo.
we utakuwa umekula kitu cha ARUSHA Hicho.
 
Back
Top Bottom