DJkus
JF-Expert Member
- Nov 9, 2018
- 354
- 470
Habari wana jamvi!
Moja kwa moja nijikite kwenye mada.
Mosi, kumekuwa na heko kwa serikali kutokana na hizi Vehicle Tracking System (VTS) bila kujali utendaji kazi wake na namna unavyoweza kudhibiti mwendo.
Kazi yake ni kumtaarifu dereva anapopitiliza speed zaidi ya 85km/hr lakini sio kupunguza mwendo kama wengi wanavyodhani ndio maana vinapiga kelele.
Hii utaiona kwenye baadhi ya magari na madereva wanaokimbia bila kuzingatia hicho king'ora, mpaka abiria unasikia kukerwa sana na hizo kelele za mfululizo bila kukoma.
Hali ingekuwa tofauti kama wangetumia speed governor maana yenyewe inadhibiti mwendo kwenye speed iliyochaguliwa. Na hapa ingesaidia wahisani wote bila kujali ni nani kwa manufaa ya wote!
Pili, gharama; jamani kiuhalisia bila kumumunya maneno gharama ni kubwa sana na bado kila mwezi wanalipia token. Hivi kweli hizi gharama serikali haizioni? Au nao wako na mgao au ndiyo biashara ya serikali kupitia mgongo wa VTS, au ni kukandamiza wamiliki wa magari hasa mabasi bila kuwa na mbadala wa uchaguzi wa gharama!
Serikali na wahisani kwa ujumla fikirieni hili kwa maslahi ya kumnufaisha kila mmoja. Kwa hili ni wapi mmiliki anafaidika? Nafuu yake iko wapi?
Mbaya zaidi mfumo wake wa kukuwajibisha wahalifu wa speed, hauko intact dereva anafanya kosa leo anakuja letewa faini baada ya miezi mitatu. Kama ni maafa tayari yameshatokea na mhalifu ameshatokomea.
Unakuta hata dereva alishaacha kazi au alifukuzwa kutokana na mambo mengine hapo ndipo mzigo unaenda kwa mmiliki kama ulivyo. (Hapa lengo ni kumuonya dereva au mmiliki?).
Badala yake mfumo wa speed governor ni rafiki kwa umma na watumiaji wengine wa barabara.
Hili ni swala la dereva na mfumo wa gari hawezi kwenda zaidi maana gari imepangiwa speed yake na haiwezi kwenda zaidi ya hapo.
Kwa ucheche niishie hapa.
Karibuni.