Nini kitatokea Wabunge wakizuiwa kutoa misaada majimboni mwao? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini kitatokea Wabunge wakizuiwa kutoa misaada majimboni mwao?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Feb 17, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Feb 17, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Mojawapo ya sababu ambazo zilitolewa kuhalalisha posho za wabunge ni kuwa wanahiatji kutoa misaada kwenye majimbo yao. Na miaka nenda rudi tumeona wabunge na wale wanaotaka kugombea ubunge wakitoa misaada mbalimbali kwenye majimbo yao. Jambo hili limezoeleka sana kiasi kwamba ni kawaida sasa. Najiuliza hata hivyo misaada hiyo kweli ni ya lazima?

  Jimbo hupata fedha kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo
  Jimbo linakuwa kwenye Wilaya au hata wilaya zaidi ya moda zinazotengewa fedha katika wizara na idara mbalimbali
  Jimbo hilo hilo huweza kuwa na manispaa au halmashauri ya manispaa hata zaidi ya moja inayotengewa fedha na kukusanya fedha
  Jimbo hilo hilo hupata fedha kutokana na utekelezaji wa kazi za wizara/idara fulani za serikali

  Kwa ufupi, hakuna jimbo ambalo linakosa pesa kabisa kwa kipimo chochote hasa zinazohusiana na shughuli za maendeleo.

  Najiuliza hata hivyo itakuwaje kama:

  a. Wabunge mara baada ya kuchaguliwa watapigwa marufuku kutoa msaada wowote jimboni kwao unaozidi sema shilingi laki moja kwa mwaka?

  b. Watu ambao wanataka kugombea ubunge kwenye jimbo fulani wawe hawajatoa misaada yenye thamani ya zaidi ya shilingi laki tano katika miaka mitatu inayotangulia uchaguzi?

  c. Waziri yeyote haruhusiwi kutoa msaada wowote wa fedha au wenye thamani isiyozaidi shilingi laki tano katika jimbo lake.

  Ninachojiuliza kama kwenye sheria ya maadili ya viongozi ikipigwa marufuku kwa viongozi kutoa misaada ya namna hiyo itakuwa na matokeo gani? Kama wananchi wanakatazwa kutoa misaada au kuwalipa viongozi wao na kuwapatia zawadi za aina mbalimbali kwanini viongozi nao wasikatazwe? Fikiria kiongozi mwenye fedha nyingi sana anavyoweza kutoa misaada mbalimbali kutoka mfukoni mwake bila kujaribu kulobby au kusababisha serikali ilete huduma au wananchi wenyewe wajipatie vitu fulanifulani kwa kukunganisha nguvu zao n.k

  Ni wazo baya au zuri?
   
 2. k

  king11 JF-Expert Member

  #2
  Feb 17, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Umasikini si siasa safi, si kwamba ukitaka kuwa mbunge au diwani kukunyime haki ata ya kusaidia ndugu zako. je mtu akiwa ametoa msaada wa kumjengea ndugu yake nyumba au kumsaidia kwa namna yeyote abanwe kugombea?
   
 3. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #3
  Feb 17, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Siyo kazi ya mbunge kutoa msaada wa fedha jimboni mwake....
  Kwahiyo kigezo hiki lazima kiwe nullified from the gets go!
   
 4. morenja

  morenja JF-Expert Member

  #4
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 3,516
  Likes Received: 1,049
  Trophy Points: 280
  mbunge ni kuja na mipango na kusimamia utekelezaji wake ,mbunge anaekuja na kugawia watu misaada ya fedha ya maandazi .huyo ni fisadi ni mpinga maendeleo ya umma wake .tena mwizi .na hafai kuongoza huyo ,mfundishe mtu kuvua samaki sio kumpa samaki ili aje kukuomba kila siku .mbunge wa aina ya kutoa samaki hafai ,
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Feb 17, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Unafikiri posho wanazodai zinasaidiakutoa misaada majimboni mwao wanazungumzia misaada kwa ndugu zao? Ni mfanyakazi gani wa Tanzania mbaye hajikuta akitoa msaada kwa ndugu zake na haongezewi posho kwa ajili hiyo?
   
 6. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #6
  Feb 17, 2012
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Hivi ni wapi palipoandikwa kisheria kuwa kazi mojawapo ya Mbunge ni kutoa misaada jimboni anakotokea? Wabunge wetu wamelemaaa na ****** huo wa kishenzi unaozalilisha wanainchi maskini wa kitanzania wakiamini kuwa wanainchi wanafurahia hiyo missaada, mbunge kuchangia shule ni personal na same kama mzazi anavyochangia madawati sasa iweje mzazi alime shamba na achangie toka jasho lake na mbunge akaombe posho bungeni then aje eti achangie madawati, huu ni wizi wa mchana kweupe bila soni....shame on CCM Mps mnaong'ang'ania Posho ili mkahonge wapiga kura
   
 7. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #7
  Feb 17, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Tatizo hapa sio kukosekana kwa sheria bali tatizo ni sisi watanzania na dependency syndrome tuliyojengewa over the yeras under TANU and CCM. Nimetafuta sana mahali ilipoandikwa kuwa ni jukumu la mbunge ni kuleta maendeleo kama vile maji, barabara, shule n.k jimboni kwake lakini sijapapata bado ile nimeona katika ibara ya 63 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa jukumu la mbunge ni kuisimamia na kuishauri serikali.

  Mantiki ya ibara hii ni msemo "Government by the people and for the people" Yaani Serikali huundwa na wananchi kwa ajili ya manufaa yao. Ili Serikali iliyoundwa na wananchi iweze kutimiza majukumu yake ipasavyo wananchi walioiunda wana wajibu mkubwa sana wa kuisimamia katika utekelezaji wa shughuli zake za kila siku kwa kuwa Serrikali huundwa na binadamu ambao wana madaifu mbali mbali ya kibinadamu.

  Dunia nzima mfumo ulipo wa kuisimamia serikali ni kuwa na bunge ambalo huundwa na idadi fulani ya wananchi iliyotajwa katika katiba na ambao huitwa wabunge. Katiba hufafanua namna hawa wabunge watakavyo patikana na mara nyingi Katiba huigawa nchi husika katika majimbo ambao wananchi katika kila jimbo hupatiwa haki ya kuwakilishwa katika Bunge kupitia idadi ya wabunge wanaotamkwa na Katiba, hapa nchini kila jimbo la uchaguzi hupatiwa nafasi moja ya uwakilishi bungeni.

  Hivyo basi utaona mbunge ni mwakilishi wa wananchi wa jimbo fulani katika kuisimamia serikali ambayo chini ya katiba hiyo hioyo ina madaraka ya hushika raslimali za taifa kama vile kodi, mbunga za wanyama, madini n.k ili kuzitumia kuwaletea wananchi maendeleo.

  Kwa hali hiyo utagundua mbunge sio tarishi wa kuleta maendeleo katika jimbo atokalo kama CCM walivyowaaminisha watanzania. Ili mbunge aweze kupata upendeleo toka kwa mawaziri wa serikali kwa kupata miradi ya maendeleo katika jimbo lake kwa lengo la kuchaguliwa tena ni lazima awapigie magoti mawaziri walioko serikali na ambao kwa mujibu wa ibara 63 ya katiba anatakiwa kuwasimamia.

  Na ili mbunge aweze kutimiza wajibu wake wa kuisimamia serikali ipasavyo ni lazima atumie muda mwingi kusoma machapisho mbali mbali ya utendaji wa serikali katika ngazi mbali mbali kama vile ripoti za utekelezaji, ripoti za ukaguzi wa mahesabu, kujielimisha kuhusu uendeshaji wa uchumi ili aweze kuishauri serikali n.k hivo mbunge anayetimiza kweli wajibu wake kwa mujibu wa ibara 63 ya Katiba hawezi kupata muda wa kutafuta maendeleo ya jimbo moja moja husuan jimbo atokalo.

  Kinachotokea hapa nchini baada ya watanzania kuwageuza wabunge wao matarishi wa kuleta maendeleo ya jimbo moja moja ni kuwa wabunge wanalazimika kujipendepekeza kwa serikali yaani Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri, Makatibu Wakuu, Maafisa wa ngazi za juu Serikalini n.k ili waweze kupata upendeleo katika jimboyao kutoka mgawanyo wa mapato ya Serikali.

  Kutokana na kujipendekeza huku kwa wabunge, anayepaswa kuwa mlinzi kugeuka omba omba Serikali imekosa usimamizi na hivyo kukithiri kwa wizi, ubadhirifu na wizi Serikalini na matokeo yake mapato ya Serikali yamekuwa yakishuka mwaka hata mwaka kutokana na uchumi kutosimamiwa ipasavyo. Matoeko yake watanzania wote tumekuwa tukiugalagala katika lindi la umasikini katika nchi yenye neema tele.

  Ili tuweze kutoka hapa tulipo ni vyema tukatumia kipindi hiki cha kubadilisha Katiba kuelimsiha watanzania wenzetu kuhusu athari za Serikali kukosa kusimamiwa na bunge kwa lengo la kuondoa kabisa ubinafsi wa sisi wapiga kura kupenda zaidi majimbo tutokayao badala ya kuweka maslahi ya taifa mbele kwa maana ya kutaka mbunge atutumikiwa zaidi katika jimbo kuleta maendeleo ya jimbo badala ya kulitumiakia taifa kwanza.

  Nimekuwa nikishangazwa sana na wanaojiita Great thinkers humu ndani ambao nao hudai maendeleo ya jimbo moja moja kutoka kwa wabunge, dhana hii ya wananchi kudai maendeleo ya jimbo moja moja inafanya wananchi washindwe kuutambua mchango wa wabunge wachache hususan wa CDM ambao wanatimiza wajibu wao wa kuisimamia Serikali at the expense ya maendeleo ya majimbo yao.
   
 8. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #8
  Feb 17, 2012
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Hakiwezi kutokea kama serikali ikijaribu kufanya hivyo itaambiwa kwanza iache kupokea misaada kutoka capitals mbalimbali.
   
 9. F

  FJM JF-Expert Member

  #9
  Feb 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Ninaamini kwa dhati kabisa kama wabunge watazuiwa kutoa misaada majimboni mwao ufanisi/uwajibikaji serikalini utaongezeka. Wabunge watafanya kazi yao ya kusimamia serikali katika ukusanyaji/matumizi ya serikali kwa sababu wanajua fika bila serikali kutekeleza kazi zake vema basi na wao watakosa kura. Kwa sasa wabunge wamegueka kama serikali ndogo ndani ya majimbo yao.

  Ukiongea na mabolozi wa nchi za nje hapa Tanzania utashtuka kusikia kwamba wamechoshwa na hodi za omba omba, mara madarasa, mara zahanati etc. Kwa sasa serikali imekazania kwamba kila anayetaka kuongea na balozi wa nje lazima kwanza a-report foreign affairrs. Lakini hii haijaondoa tatizo.Na sasa wabunge wanashirikiana na wafanyabishara ili watoe misaada. Mfanyabiashara na mfanyabiashara lazima atataka something in return.

  Lakini kama wabunge wangeacha kujigeuza serikali na badala yake wakaisimamia, EPA, Meremeta, ukwepaji kodi unaofanywa na makampuni makubwa na mengine yangeshughulikiwa kwa nguvu zote. Na sasa hivi makampuni makubwa yamegundua hilo kwa kwa hiyo wanawekeza kwa wabunge hivyo kama hawakulipa kodi hakuna mtu wa kuwasema! Kaeni macho wakati wa bunge la bajeti mwaka huu muone utitiri wa 'warsha' na vyakula jioni vinavyoandaliwa na makampuni kwa wabunge! Mfano Vodacom hawapo hata kwenye list ya makumpuni makubwa 15 yanayoongoza kwa kulipa kodi. Lakini bunge limekaa kimya! Tazama Vodacom wanavyotoa madawati kwenye majimbo ya hawa wabunge!

  Kuna haja kabisa ya kuangalia tena huu mtindo wa uotaji misaada kama tunakata salama. Wabunge wanatumia muda mwingine kutafuta hela za kusaidia majimbo wakati hela zipo.
   
 10. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #10
  Feb 17, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 796
  Trophy Points: 280
  Well said Watababe na muanzisha mada!
  Hiki kitu kimekuwa kikinitatiza sana, na nakubaliana nanyi kuwa ili kukiondoa lazima kuwepo na kifungu cha sheria kuthibiti hali hiyo; hii si itawafanya wabunge wawe more responsible ktk kusimamia serikali lkn itabadilisha fikra za watanzania badala ya kuendelea kuomba kusaidiwa wataanza kudai haki zao!
   
 11. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #11
  Feb 17, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Tatizo ni sisi wananchi wenyewe huwa tunawapima wabunge wetu wa vigezo vipi? Kwa asilimia kubwa wabunge wanapimwa kutokana na maendeleo yaliyofanyika katika majimbo yao mfano ujenzi wa barabara, shule, zahanati, miradi ya maji n.k...
  Vitu ambavyo ni juu ya wakuu wa mikoa na wilaya kuvisimamia na kuvitekeleza vinashushulikiwa na wabunge! Kuna wakati huwa najiuliza hivi wakuu wa mikoa na wilaya wana kazi gani haswa zaidi ya kupiga politiki! Na ndio hawa hawa wanatumika na CCM ktk kuhujumu chaguzi mbali mbali....thats why wameng'ang'ania maDC wawemo kwenye mchakato wa katiba!

  Ndio maana wabunge hawajishughulishi kikamilifu ktk kujadili miswada sababu wanajua wananchi hawatawapima kwa hilo bali wamewajengea nini ktk majimbo yao na wamewapa misaada mingapi! Ndio maana mbunge hata akichapa usingizi mjengoni kwake ni poa tu anajua ataenda kutembeza faranga za misaada!
   
 12. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #12
  Feb 17, 2012
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Wazo zuri ,
  Ni muda muafaka kukawekwa sheria inayoweka kiwango maalum cha kutoa msaada kwa wananchi na isiishie kwa wabunge bali kiongozi yoyote wa umma na kama sio mtumishi wa umma basi kuwepo na mamlaka inayo wasimamia watoa misaada na kuchunguza vyanzo vya hiyo misaada..
   
 13. Mtafiti1

  Mtafiti1 JF-Expert Member

  #13
  Feb 17, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 264
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hiyo misaada wanawapa watu wao - marafiki, ndugu na jamaa.Mimi sijawahi kuona msaada kutoka kwa Mbunge wangu hata siku moja.Sijawahi kusikia kamsaidia mtu ninayemfahamu.Kama anarudisha fadhila kwa waliomsaidia kwenye kampeni mimi inanihusu vipi?

  Huo msaada wanaoutoa ni hiari au sadaka.Kwanini wafanyakazi wasidai mishahara iongezwe kwa kigezo cha kulipa zaka, sadaka, michango ya ujenzi wa misikiti, makanisa, kuchangia vyama vya mikoa na makabila yao na sote tunajua michango imezidi. Pia kuna michango ya harusi, kitchen party, send-off, vipaimara, kumcheza mwali, mkole, kesha ..............and the list goes on!
   
 14. c

  chuwaalbert JF-Expert Member

  #14
  Feb 17, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 3,049
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  Wabunge (HASA wa CCM) wanafurahia UMASIKINI wa wananchi kwenye majimbo yao, eti Ooh ntawasomeshea watoto wenu kwenye shule za Kata (ambazo nazo zilianzishwa kama bomba la kutiririsha misaada yao). Wanaweka hii kama mitaji ya kupata KURA! Wananchi waelimishwe KUJITEGEMEA, elimu waipatayo iwaweke HURU! Elimu ya watu wazima isisitizwe.
   
 15. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #15
  Feb 17, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  mbunge kazi yake ni kusimamia miradi yote vizuri,

  pia ni muhimu muda mwingi kufikia kwenye field na kujua kinachoendelea kwani yeye sio KARANI kwamba muda wote yupo ofsini,

  mkbunge sio kazi yake kutoa misaada,hivo mfuko wa jimbo utumike ipasavyo.
   
 16. Mwasi

  Mwasi JF-Expert Member

  #16
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 12, 2010
  Messages: 249
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Ni wazo zuri, ni bora tukawa na sheria ya namna hii. Maana wabunge wakitoa msaada inawezekana kabisa wanatumia hiyo misaada kama njia ya kujipigia kampeni kwa ajili ya chaguzi zinazofuata. Kwa maana nyingine hii misaada ni rushwa kwa wapiga kura, kwa kuwa siyo jukumu lao kutoa msaada.
   
 17. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #17
  Feb 17, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kimsingi ni kwamba hakuna maendeleo yanaweza patikana jimboni kwa mbunge kuwapatia wananchi msaada wa fedha ya mfukoni isipokuwa kwa kuweka mikakati ya maendeleo endelevu! hoja ya wabunge kutoa fedha kwa wapiga kura ni mfu na haina maana hata kidogo!
   
 18. H

  Haika JF-Expert Member

  #18
  Feb 17, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Mie ningekuwa wa kwanza kuunga mkono,
   
 19. W

  WildCard JF-Expert Member

  #19
  Feb 17, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  -Hata ikitungwa sheria ya kuwazuia kutoa misaada hiyo itatekelezwa? Sheria za nchi hii ni kama Amri 10 za Mungu! Watu hawataacha kuzini.
  -Ubunge wenyewe unapatikana kwa kutoa "misaada". Utaacha kuendelea kutoa ukiupata Ubunge wenyewe?
  -Jinsi Wabunge hawa wanavyokwapua kila mahali, tuwaachie wale wenyewe! Acha tuambulie hayo makombo.
   
 20. muonamambo

  muonamambo JF-Expert Member

  #20
  Feb 17, 2012
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Well said by most of contributors!!!. Tatizo la Tz ni elimu ya uraia na ndio mtaji wa CCM . kwao watu kukosa uelewa wao ndio wanapopatia na naomba kuwaambia kama hatutafuta mavumbi haya machoni pa wa Tz. hata tukibadili katiba mara 10. tukaingia kwenye chaguzi mnazoita huru mara 100. Tz haiwezi kombolewa tutabaki kuwa maskini milele dumu.

  Pale kampuni kubwa inapokwepa kulipa kodi na kuja kutoa misaada ya kijinga kupitia migongoni kwa wabunge huku wananchi tukiyapigia makofi kana kwamba tumepewa bure wakati tulistahili zaidi kupata zaidi kupitia kwenye kodi na Serkali yetu ndio ingewajibika kutujengea shule, madawati, maji , barabara nk....

  Tz safari bado ni ndefu....
   
Loading...