Nini kitatokea Wabunge wakizuiwa kutoa misaada majimboni mwao?

Mwanakjjiji umenifikirisha sana. It is a very good idea. Kwa kuwa Mbunge hakusanyi kodi anapaswa kuwa msimamizi wa shughuli za serikali Jimboni na kuihoji inapoharibu Bungeni. Lakini kwa kuwa wamejigeuza waleta maendeleo ndo maana unawasikia kuwa wanataka mfuko wa maendeleo ya jimbo, mara posho zaidi. Haya yote jibu lake ni Katiba mppya.
 
Mwanakjjiji umenifikirisha sana. It is a very good idea. Kwa kuwa Mbunge hakusanyi kodi anapaswa kuwa msimamizi wa shughuli za serikali Jimboni na kuihoji inapoharibu Bungeni. Lakini kwa kuwa wamejigeuza waleta maendeleo ndo maana unawasikia kuwa wanataka mfuko wa maendeleo ya jimbo, mara posho zaidi. Haya yote jibu lake ni Katiba mppya.
Wakati wa mjadala bungeni kuanzisha hii mifuko ya maenndeleo majimboni, nilifadhaika sana baada ya kuona wabunge wa CDM, akiwemo Dr Slaa wakiunga mkono kuanzishwa kwa mifuko hii. Hii iliniacha nikijihoji kama na wao hawajui hata majukumu ya mbunge.
 
Tatizo ni sisi wananchi wenyewe huwa tunawapima wabunge wetu wa vigezo vipi? Kwa asilimia kubwa wabunge wanapimwa kutokana na maendeleo yaliyofanyika katika majimbo yao mfano ujenzi wa barabara, shule, zahanati, miradi ya maji n.k...
Vitu ambavyo ni juu ya wakuu wa mikoa na wilaya kuvisimamia na kuvitekeleza vinashushulikiwa na wabunge! Kuna wakati huwa najiuliza hivi wakuu wa mikoa na wilaya wana kazi gani haswa zaidi ya kupiga politiki! Na ndio hawa hawa wanatumika na CCM ktk kuhujumu chaguzi mbali mbali....thats why wameng'ang'ania maDC wawemo kwenye mchakato wa katiba!

Ndio maana wabunge hawajishughulishi kikamilifu ktk kujadili miswada sababu wanajua wananchi hawatawapima kwa hilo bali wamewajengea nini ktk majimbo yao na wamewapa misaada mingapi! Ndio maana mbunge hata akichapa usingizi mjengoni kwake ni poa tu anajua ataenda kutembeza faranga za misaada!

je nani walulaumiwa kwa wananchi kuwapima wabunge kwa viezo visivyostahili? je sisi wapenda mabadiliko ni kwa kiasi gani tumeshiriki kuwapatia wananchi elimu sahihi ili kuondo hii dhana potofu? je ni kwanini wabunmge wa vyama vya siasa nao wanaonekana kulikubali hili kirahisi ka maana ya kutochukua hatua zozote kuwaelimisha wananchi?
 
Mwanakjjiji umenifikirisha sana. It is a very good idea. Kwa kuwa Mbunge hakusanyi kodi anapaswa kuwa msimamizi wa shughuli za serikali Jimboni na kuihoji inapoharibu Bungeni. Lakini kwa kuwa wamejigeuza waleta maendeleo ndo maana unawasikia kuwa wanataka mfuko wa maendeleo ya jimbo, mara posho zaidi.
Haya yote jibu lake ni Katiba mppya
.


Maudhui ya Katiba mpya hayajiandiki yenyewe, ni lazima wananchi watoe maoni kuhus jambo fulani. Ni wananchi wangapi wanaliohili kama tatizo? Na wewe kama mjumbe wa Baraza Kuu la CDM umefanya nini binafsi na kupitia chama kuelimis umma uone dosari hii na kutaka irekebishwe?
 
Kuna tatizo kubwa sana la wananchi na wabunge wenyewe kufahamu ni nini wajibu, mamlaka na mipaka ya mbunge.
 
Lakini watu kama kina Rostam wangeweza vipi kuleta maendeleo kwenye majimbo yao?
Bila shaka ulimsoma marehemu Regia tathmini yake alipotoka kwenye uchaguzi mdogo wa Igunga. Igunga kama Tanzania nyingine hali ni hiihii. Nilikwenda Musoma Vijijini kwa Advocate Mkono baada kusikia akisifiwa sana. Nikakuta njia anayotumia ni misaada ya papo kwa papo. Misaada ambayo sio endelevu, aliyesaidiwa atarudi tena kuomba msaada.
Kwa staili ya akina RA, Mkono, Lowasa, Chenge wanajikuta wamemilikishwa majimbo. Angalia pia na namna utajiri wa hawa jamaa unavyopatikana. Tunataka Bunge na Wabunge watakaoisimamia serikali. Challenge iliyo mbele yetu ni kutafuta namna ya kuiondoa serikali BUNGENI ili kuonekane wazi tofauti ya mihimili hii miwili.
 
Kama wananchi wanakatazwa kutoa vizawadi kwa viongozi wao kwanini viongozi waruhusiwe kutoa vizawadi kwa wananchi bila kuonekana wananunua nafasi zao?
 
Kama wananchi wanakatazwa kutoa vizawadi kwa viongozi wao kwanini viongozi waruhusiwe kutoa vizawadi kwa wananchi bila kuonekana wananunua nafasi zao?
Kwa VIONGOZI zile wanazotoa haziitwi zawadi. Wanatekeleza AHADI walizoahidi wakati wa kampeni. Jana Rais wetu alikuwa Umasaini akiwapa wafugaji kile walichoita "kifuta machozi" cha ng'ombe watano kila mmoja baada ya kupotelewa na mifugo yao kwa wingi kwa ajili ya ukame. Kalianzisha hili kwa wafugaji nadhani na peasants nao watafutwa machozi.
 
Nashindwa kujua mantiki ya kuongezewa posho ili kutoa misaada.Sioni muunganiko wa moja kwa moja kati ya posho na misaada wanayotoa.Ni kauli ya kipumbavu na kijinga,na ujinga na upumbavu kuamini kuwa wabunge wanatumia posho kutupatia misaada.Kama ni hivyo basi wabunge watakuwa wanafanya juu chini kuhakikisha kuwa watanzania hatutoki kwenye umaskini.
 
Back
Top Bottom