Nini kitatokea endapo Makonda atakaidi agizo la waziri?

pepsin

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
3,474
6,147
Kauli mbili za serikali,moja ya rais Magufuli ambaye amemsifu na kumhakikishia Makonda usalama,kwamba asiogope,achape kazi.
Pili ni kauli ya waziri mwenye dhamana na habari,kwamba ni kitendo cha kinyama na amekilaani.Halafu kaunda tume na kuipa muda mfupi,24hrs! Na matokeo yatakuwa hadharani!
Sasa ikitokea Makonda kaamua kufuata ushauri wa Rais,yaani asiogope na hivyo kukaidi wito wa tume ya waziri.
Nini kitatokea? Waziri atajiuzulu au atamtumia polisi kumkamata? What will happen?
 
Nimejaribu kuwaza sijapata jibu ndani wa wiki mbili tu baba mwenye nyumba amesha wadhihaki wasaidizi wake wawili tena kwa mbwembwe na kejeri ya hali ya juu,najiuliza nini kinawatesa hawa wasaidizi wake kutotoa maamuzi magumu ya kumfanya nae asifiri kidogo, je uchu wa madaraka wa wasaidizi wake au wanaogopa wakijiuzuru kufuatwa na mabomu,kwa maana kama bashite kaenda na bunduki kutishia I hope baba J atawafuata na vifaru.
 
Lazima atakaidi wito wa waziri!......believe me!
 
Attachments

  • tapatalk_1490033152870.jpeg
    tapatalk_1490033152870.jpeg
    39.1 KB · Views: 29
Kauli mbili za serikali,moja ya rais Magufuli ambaye amemsifu na kumhakikishia Makonda usalama,kwamba asiogope,achape kazi.
Pili ni kauli ya waziri mwenye dhamana na habari,kwamba ni kitendo cha kinyama na amekilaani.Halafu kaunda tume na kuipa muda mfupi,24hrs! Na matokeo yatakuwa hadharani!
Sasa ikitokea Makonda kaamua kufuata ushauri wa Rais,yaani asiogope na hivyo kukaidi wito wa tume ya waziri.
Nini kitatokea? Waziri atajiuzulu au atamtumia polisi kumkamata? What will happen?
Kwanza hiyo tume atakubali ikamuhoji
 
Hapa ni moja Nape ajiuzuru kwani hatapoteza sana kwa kuwa ni mbunge wa kuchaguliwa. Ni kijiuzuru tu.....
 
Hata mimi ningekuwa makonda nisingekubali kuhojiwa, waziri ndo nani sasa kama Mr. President ameshatoa go ahead. Sidhani kama atakuwa imani yangu hawezi.
 
Hakuna kitakachotokea zaidi ya hiyo tume ya Nape kunyimwa ushirikiano na kutimuliwa mbali. Nategemea kusikia Nape kajiuzulu.

Kwa lugha ya sanaa, msikilize JPM hapa chini kuhusu Makonda.

Hapa ni moja Nape ajiuzuru kwani hatapoteza sana kwa kuwa ni mbunge wa kuchaguliwa. Ni kijiuzuru tu.....

Asijiudhuru maana Magu atatuletea waziri dikteta balaa kwa vyombo vya habari, Nape abaki maana ameanza kubalance mambo ya kufungia vyombo vya habari kaacha sasa
 
Lakini ili kuweka rekodi sawa acha hiyo tume itoe matokeo yao ya uchunguzi hata ukipuuzwa
 
..wala msitegemee bashite aitikie wito wowote...yeye anamtumikia mtu anayetamba kuwa haamuliwi kitu na mtu...au mmesahau kuwa tayari bashite ameshakaidi wito wa mahakama...na pia bunge!.....lazima sasa umma utambue kuwa mihimili mingine ya dola imebakwa haswa.....na sitoshangaa hili la bashite likapita tu...maana wabongo wameshafanywa makondoo....wasiwe makondoo vipi wakati mtu anaweza kujiamulia kuchukua genge la wanajeshi akavamia kituo cha habari kama anaingia chooni kwake!...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom